
Kundi la kwanza la
wahamiaji limewasili nchini Croatia ,ambayo ni njia mpya ya kuelekea
mataifa ya Ulaya yaliopo kaskazini ,siku moja baada ya Hungary kufunga
mpaka wake na Serbia.
Takriban wahamiaji 150 walivuka na kuingia katika mataifa ya muungano wa Ulaya kutoka Serbia.Croatia inasema kuwa iko tayari kuwapokea moja kwa moja ama kuwaelekeza kule wanakotaka kwenda.
Wahamiaji wengi kutoka Syria wana matumaini ya kuelekea Ujerumani.
Mamia ya wahamiaji waliokwama walingojea nje usiku kucha ama katika mahema karibu na mpakawa Serbia na Hungaryc

No comments:
Post a Comment