Tuesday, October 13, 2015

Wasifu wa Edward Lowassa



 Wasifu wa Edward Lowassa      7 Oktoba 2015  Mshirikishe mwenzako Image caption Edward Lowassa alizaliwa August 26 mwaka 1953 kijijini Ngarashi Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.  Edward Ngoyai Lowassa anatoka katika ya jamii ya wafugaji Kaskazini mwa Tanzania.  Alizaliwa August 26 mwaka 1953 kijijini Ngarashi Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.  Kitaaluma Lowasa ni msomi , akiwa na shahada kwanza kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam na shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Bath huko Uingereza (1983-1984).  Uzoefu katika siasa  Edward Lowasa ni mtoto wa tatu wa Mzee Ngoyayi.  Ingawa baba yake alikuwa mfugaji aliwahi pia kufanya kazi kama tarishi katika serikali ya wakoloni. Image caption Licha ya kuwa mwanachama wa CCM kwa miaka 38, bwana Lowassa aliwashangaza wanachama wa CCM kwa uamuzi wake wa kukihama chama hicho.  Alijiunga na chama cha CCM mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka wa 1977.  Kabla ya kugombea ubunge , aliwahi kutumikia jeshi la Tanzania na hata kupigana katika vita kati ya Tanzania na Uganda vilivyopelekea Idd Amin kuondolewa madarakani.  Baada ya hapo alikuwa mtumishi wa umma kwa miaka kadhaa kabla kuteuliwa kuwa mbunge kuwajilisha vijana na kujiunga rasmi na siasa.  Mwaka wa 1990 alijitosa ulingoni kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la uchaguzi la Monduli.  Alifanyikiwa kwa miaka yote hii Lowassa ameendelea kulishikilia jimbo hilo la uchaguzi hadi sasa anapolazimika kuliachia ili kuwania Urais.  Hii si mara yake ya kwanza kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,kwani mwaka 1995,alikuwa miongoni mwa watangaza nia 15, hata hivyo nafasi ikachukuliwa na Benjamin William Mkapa. Image caption Ni mshika bendera wa UKAWA ambao ni muungano wa vyama vinne vya upinzani  Hata hivyo tofauti na matarajio ya wafuasi wake, Mwaka 2005, Lowassa hakuwania nafasi hiyo, badala yake aliunga mkono rais anayemaliza muda wake Jakaya Kikwete.  Je Lowassa huyu wa sasa amewahi kuwa nani katika nyadhifa alizozipitia kiserikali?  Edward Ngoyayi Lowassa amewahi, kuwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo, Ardhi na Maendeleo ya Makazi pamoja na nafasi nyinginezo.  Lakini pia nafasi za juu alizowahi kuzipata ni pamoja na kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania kuanzia mwaka 2005 mpaka Febuari 7 mwaka 2008, alipolazimika kujiuzulu baada ya madai ya kuhusishwa katika kashfa ya rushwa ya Kampuni ya Richmond, Madai ambayo bwana Lowassa aliyakanusha hadi sasa.  Katika siasa,Lowassa anafahamika kama mtu wenye misimamo mikali,kwa kile anachokiamini mwenyewe kama siasa zinazo ambatana na maamuzi magumu.  Licha ya kuwa mwanachama wa CCM kwa miaka 38, bwana Lowassa aliwashangaza wanachama wa CCM kwa uamuzi wake wa kukihama chama hicho. Image caption Kufuatia uamuzi wake wa kubadili chama, Edward Lowasa amelazimika pia kubadili msimamo wake wa kisiasa  Hatua iliyochangiwa na yeye kutoridhrishwa na jinsi uteuzi wa wagombea urais wa kilichokuwa chama chake ulivyoendeshwa.  Alijiunga na chama cha kikuu cha upinzani cha CHADEMA.  Hiki ni mojawapo ya vyama vinne vya upinzani vinavyounda umoja uitwao,UKAWA.  Kufuatia uamuzi wake wa kubadili chama, Edward Lowasa amelazimika pia kubadili msimamo wake wa kisiasa na kuwa mpinzani wa chama tawala na sera aliziunga mkono na kuzitumikia awali, jambo ambalo linawatatanisha wakosoaji wake .  Hii ni mara yake ya pili kujaribu kuingia ikulu. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako      Facebook     Twitter  Rejea mwanzo wa ukurasa Habari kuu Ripoti:Thoma

Milioni waondolewa kwenye daftari la wapiga kura Tz



Tume inayosimamia uchaguzi nchini Tanzania (NEC), imefuta majina ya wapiga kura zaidi ya milioni moja kutoka kwenye orodha ya watu waliojiandikisha kupiga kura.
Awali tume hiyo ilikuwa imetoa idadi ya wapiga kura milioni 23.7 waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu kupitia kwa mfumo wa kielektroniki (BVR).
Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema idadi hiyo imepigwa kalamu kufuatia shughuli ya kuhakiki majina ya watu wote waliojiandikisha.
Image caption Watu 181,452 walijiandikisha zaidi ya mara moja.
Majina ya watu milioni moja, 1,031,769 waliopatikana kuwa na makosa moja au zaidi yaliondolewa.
Jaji Lubuva alisema kuwa wengine waliojiandikisha zaidi ya mara moja, wengine hawakutimiza vigezo vya kuitwa Watanzania huku waliosalia wakiwa watu waliokosa sifa nyingine muhimu.
Kufuatia shughuli hiyo , Jaji Lubuva alisema wapiga kura watakaoruhusiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao watakuwa ni watu milioni 22,251,292.
Image caption Jaji Lubuva alisema wapiga kura watakaoruhusiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao watakuwa ni watu milioni 22,251,292.
Kisiwani Zanzibar wapiga kura wapatao laki 503,193 wataruhusiwa kushiriki uchaguzi mkuu tarehe 25.
Watu 181,452 walijiandikisha zaidi ya mara moja.
Wengine 845,944 waliandikishwa na wahudumu 74,502 waliokuwa kwenye mafunzo kabla ya kuanza shughuli kuu ya uandikishaji
Image caption Vituo vya kupigia kura 63,525 vitakuwa Tanzania bara huku Kisiwa cha Zanzibar kikitengewa vituo 1,580
Aidha majina ya watu 3,870 yalibainika kuwa watu waliokosa sifa za Mtanzania.
Wakati huohuo idadi ya vituo vya kupigia kura pia vimetangazwa.
Kutakuwa na vituo 65,105 vya kupigia kura katika uchaguzi ujao.
Vituo vya kupigia kura 63,525 vitakuwa Tanzania bara huku Kisiwa cha Zanzibar kikitengewa vituo 1,580 vya kupigia kura.

RIPOTI ,RAIS WA BUKINAFASO ALIUWAWA

 
Matokeo ya ukaguzi wa kimatibabu uliofanyiwa mabaki ya mwili wa aliyekuwa rais wa Burkina Faso marehemu Thomas Sankara miaka 28 baada ya kuuawa,yanaonyesha kuwa mwili wake ulijaa risasi kulingana na wakili aliyekuwa akiwakilisha familia yake kulingana na mtandao wa facebook wa kituo cha habari cha Burkina 24.
Familia yake ilikuwa ikingojea matokeo ya DNA kuthibitisha kwamba mabaki hayo yalikuwa ya bwana Sankara,wakili Benewende Sankara aliviambia vyombo vya habari nchini humo.


 
 
Mariam Sankara mkewe marehemu Thomas Sankara
Bwana Sankara aliuawa katika mazingira ya kutatanisha akiwa na umri wa miaka 37 na kundi la wanajeshi mwezi Octoba mwaka 1987,na alizikwa kwaa haraka kufuatia mpainduzi yalioongozwa na mrithi wake Blaise Compaore.

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad