Mwishoni mwa wiki hii, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, akishirikiana na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni, walizindua ujenzi wa bomba la mafuta ghafi, litakalojengwa kutokea Hoima nchini Uganda hadi kijiji cha Chongoleani, mkoani Tanga.
Hata hivyo, akiwa njiani kuelekea Tanga kuhudhuria tukio hilo kubwa, rais Magufuli, alilazimika kusimama njiani baada ya wananchi kuusimamisha msafara wake, wakitaka aongee nao, jambo ambalo alilitekeleza, kama inavyoonekana katika video hii
No comments:
Post a Comment