na Berensichina,bunda,sept20,2017,Rpc
Mara ahidi ushirikiano na askari wa hifadhi ya Serengeti.
kamanda wa
polisi mkoa wa mara kamishina msaidizi wa polisi jafari mohamed amesema jeshi
la polisi mkoani mara litahakikisha linashilikiana na askari wa hifadhi ya
taifa ya serengeti katika kuhakikisha wanakomesha vitengo vya ujangili katika
hifadhi hiyo,
kamanda
jafari ameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi kilichofanyika
wilayani bunda ambacho kimewahusha wahifadhi toka hifadhi ya taifa ya serengeti
waendesha mashitaka wakuu wavitengo vya
ulinzi wa wanyamapori na ofisi ya mwandesha mashitaka mkoa wa mara lengo likiwa
ni kuweka mkakati namna ya kupambana na ujangili,
akizungumza
kwa niaba ya wahifadhi wa hifadhi hiyo,mhifadhi emanuel matungwa amesema
changamoto ya ujangili katika hifadhi hiyo ni kubwa kwani kila kukicha
majangili wanabuni mbinu mpya hivyo jitihada za pamoja zinahitajika katika
kupambana na vitendo hivyo,
kwa upande
wake wakili wa serikali mwandamizi toka
wa mkoani mara anisus kahindura,amesema ofisi yake imejipanga ili
kuhakikisha kesi za nyara zinamalizika mapema ili kuondoa msongamano wa kesi
hizo mahakamani
No comments:
Post a Comment