Thursday, August 3, 2017

Watoa huduma katika hifadhi ya Serengeti

Miongoni mwa mamvo yanayoifanya hifadhi ya Serengeti, kuwa ya kwanza kuiwaza unapofikiri mahali pa kwenda kutalii, ni pamoja na watoa huduma mbalimbali, ambao wamesheheni vifaa na ukaribu wa kutosha.

Blogi hii, ilipata fursa ya kutembelea hifadhini humo hivi karibuni na kushuhudia baadhi ya wageni waliokuwa wametembelea mahali hapo wakiwa wanafurahia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za uhakika ambazo walizipata kutoka kwa makampuni ya usafiri yenye kutoa huduma za usafiri ndani ya hifadhi hiyo.


 Watoa huduma hususan za usafiri ndani ya hifadhi ni wenye magari ambayo yanakidhi mahitaji ya hali zote za hewa katika mwaka mzima, pamoja na hali ya barabara zote katika eneo la hifadhi

Miongoni mwa watia huduma za usafiri waliobobea katika shughuli hiyo, ni pamoja na kampuni ya Zara Tanzania Adventures, kama magari yao yanavyoonekana pichani. Ni yenye ubora wa hali ya juu



Wengine ni kampuni ya Altezsa, ambao nao wana magari ya uhakika miongoni mwayo yakiwa haya yenye kuonekana katika picha hizi hapa juu

No comments:

Post a Comment

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad