MKUU WA GEREZA AACHIWA HURU
NA Berensi Alikadi -Bunda
MAHAKAMA ya wilaya ya Bunda jana ilimuachia huru mkuu wa gereza la Matongo wilayani Bariadi mkoani Shinyanga,Maiko Maziku baada ya upande wa mashitaka kushindwa kutoa ushahidi wa kujitosheleza.
Hakimu mfawidhi mwandamizi wa mahakama ya wilaya hiyo Joacimu Tiganga alisema kuwa mshitakiwa huyo alikuwa miongoni mwa washitakiwa sita ambao walikamatwa tarehe 2/12/2009katika mbuga ya mihama iliyopo ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti ambapo walikuwa wanakabiliwa na makosa sita ya kesi ya uhujumu uchumi.
Aliyataja makosa hayo kuwa ni kula njama kwa nia ya makosa,kukutwa na nyara za serikali, kuwinda ndani ya hifadhi kwa kutumia silaha zilizokatazwa,kuingia hifadhini bila kibali, kujwindas wanyama waliokatazwa na kukutwa na silaha hifadhini bila kibali.
Hakimu alidai kuwa miongoni mwa walikamatwa alikuwemo askari wake mmoja na kwamba yeye alikamtwa kwa kile kilichodaiwa kuwa huenda yeye ndiye aliyempa ruhusa na sailaha ya kwenda kuwindia.
Alifafanua kuwa baada ya upande wa mashitaka kufunga ushahidi wake mahakama ilipitia ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na kuona kuwa wakati tukio hilo linatendeka mkuu huyo wa gereza hakuwepo na kwamba walalamikaji wameshindwa kuonyesha kama kweli mkuu huyo ndiye aliyemtuma na kumpa silaha hivyo mshitakiwa hakuwa na kesi ya kujibu.
Kufutia hali hiyo mahakama ilimuachia huru mshitakiwa huyo ambapo wenzake wanaendelea na kesi hiyo ambayo itaanza kusikilizwa tarehe 12/12/ mwaka huu.ambapo washitakiwa wengine wako nje kwa dhamana.
Kesi hiyo ilikuwa inaongoza na mawakili wa serikali,Pius Hilla toka ofisi ya mwanasheria wa serikali Mwanza na Meredi Rweyemamu toka Dare-salaam wakisaidiana na mawakili Prochas Longomba toka kikosi cha kuzuia ujangili na Elias Benjamini,na Maiko Laizer toka Tanapa.
Kwa upande wake mkuu huyo alikuwa akitetewa na mawakili, Hezron Foka na Kweka ambao ni mawakili wa kujitegemea toka jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment