HOJA YANGU
NANI KAWATUMA GREEN-GUARD KUVAA MIKANDA YA JESHI?
NA Berensi Alikadi-Bunda
Niliwahi kuandika makala katika gazeti hili kuhusu hatari ya raia kuvaa nguo zinazofanana na sare za jeshi, makala ambayo naamini ilileta mabadiriko makubwa maana niliona baada ya makala hiyo kutoka watu wengi wakikamatwa waliokuwa wamevaa nguo hizo.
Pengine unaweza kujiuliza ni kwanini niliandika makala hiyo, niliamua kuandika makala hiyo baada ya kuona vitendo vingi vya ujambazi vimekithili na wale waliuokuwa wakikamatwa walikuwa wakikutwa na nguo za jeshi hali ambayo ililivunjia sana heshima ya jeshi letu la wananchi.
Wapo wengi waliojenga dhana kuwa huenda vitendo hivyo vilikuwa vikifanywa na askari wetu wa jeshi la wananchi, lakini kumbe ni kundi la watu wachache ambao walikuwa wakitumia nguo hizo kwa kufanyia uharifu.
Leo tena sitaki kuzungumzia tena suala la nguo hizo nina imani kuwa wahusika walisikia ujumbe huo na waliwashughulikia wananchi waliokuwa wanavaa mavazi hayo na kwa vile sheria ipo na amini kuwa jambo hilo halitarudia tena.
Katika makala hii leo nataka kuzungumzia suala la hawa askari wa chama cha mapinduzi maarufu kama Green Guad ambao wanavaa mikanda ya jeshi la wananchi na viatu maarufu kama buti.
Nimekuwa nikijiuliza sana kwa muda mrefu kuhusu uvaaji huu wa hawa vijana ambao wanajiita askari wa chama kwa kuruhusiwa kuvaa mavazi haya ya kijeshi huku serikali ikiwaangalia.
Green Guad hawa wamekuwa wakivaa mikanda hii katika matukio tofauti hasa kunapokuwepo na sherehe mbalimbali za kichama na pengine mara nyingi katika ziara za viongozi wakubwa mfano rais, waziri mkuu na viongozi wa juu wa chama cha mapinduzi.
Kinachonishangaza ni kwamba katika hafla hizo huwa wapo viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo wakuu wa majeshi na wa polisi ambao wanajua kuwa ni makosa kwa mtu asiye askari kuvaa sare yeyote ya kijeshi na hilo ni kosa la jinai lakini hawawachukulii hatua yeyote.
Katikasiku za hivi karibuni green guad hawa wamekuwa wakitumia mikanda hiyo kwa kupigia wananchi na kuwaumiza na hata wananchi wakienda kushitaki polisi huwa hawachukuliwi hatua.
Hivi karibuni katika mkutano mmoja wa kampeni katika jimbo la Sumve mwandishi mmoja wa habari wa gazeti la mwananchi alipigwa na green guad hawa kwa baada ya kupewa amri na mmoja wa viongozi wa chama hicho sijui kesi hii kama imeenda polisi na ni hatua gani waliyochukuliwa.
Pengine watanzania wanataka kufahamu kama hilo nao ni jeshi na kama ni jeshi liko katika ibara gani ya katiba ya Tanzania na kama siyo jeshi kwanini liruhusiewe kuvaa mikanda ya jeshi hivi wanajeshi wetu leo wamekwenda likizo?
Wakati leo hawa wanaruhusiwa kuvaa mikanda ya jeshi wapo baadhi ya askari wanavaa viatu vikiwa vimeshonwa viraka na hata wengeine wanavaa mikanda ikiwa imechanika, lakini hawa green guad leo wanamikanda mipya buti mpya sasa sijui nani kati ya hawa anastahili kuvaa sare hizo.
Mimi leo nataka wanajeshi wanijibu na wawajibu watanzania kuwa tangia lini wameanza kuvaliana nguo na green guad au ni kwa vile wao wako chama twawala hivi kweli chama kama CUF au Chadema leo vijana wake wangevaa mikanda ya jeshi sijui kama wangekuwa na hali gani
Jeshi la wananchi linapaswa kuwaeleza wananchi kuhusu uharali wa vijana hawa wa chama cha mapinduzi kuvaa sare hizi na nani iliwapa mikanda hiyo na hivyo viatu, na pia liwaambie wananchi kuwa limeanza kugawa sare zake ovyo.
Lakini pia mkuu wa majeshi atauambie kuwa green guad ni jeshi la nani na linawajibika kwa nani na linalipwa mshahara na nani na kama siyo jeshi kiharali nani analiruhusu kuvaa mikanda hiyo.
Kama jeshi letu haliwezi kuwanyang’anya vijana hawa mikanda hii basi tufahamu kuwa wao ndio wanawasapoti na kuwapa mikanda na viatu hivyo ambavyo ndivyo wanatumia katika kuwapigia wananchi hasa katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi.
Tanzania ni nchi yenye amani na inatawaliwa kwa majeshi yalikatika katiba ya jamhuri hatutaki kuona kundi la chama Fulani linajifanya kuwa na jeshi ambalo linawatisha wananchi kwa kuvaa mikanda ambayo inanuliwa kwa kodi yetu ni vema jeshi letu lifahamu hivyo na liwanyanga’nye hawa green Guad.mikanda na hizo buti.
No comments:
Post a Comment