Tuesday, August 28, 2012

Mwandishi wa habari Chanel 10 ajitosa kuwania UNEC

Mwandishi ajitosa NEC-CCM

na Sitta Tumma, Bunda

MWANDISHI wa habari, Cyprian Musiba aliyewahi kufanya kazi katika Televisheni ya Channel Ten, amechukua fomu ya kugombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) ya CCM na Mkutano Mkuu wa chama hicho ngazi ya taifa wilayani Bunda mkoani Mara.
Musiba ambaye amechukua fomu juzi mchana na kurudisha jana asubuhi Makao Makuu ya Ofisi ya CCM Bunda, amesema dhamira yake ya kuomba nafasi hizo mbili ni kwenda kukijenga chama katika nyanja zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Alisema atapambana kwa nguvu zake zote kudhibiti rushwa, siasa za chuki, fitna na makundi ndani ya chama chake hicho tawala.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu, Musiba alisema moja ya mambo yanayokichafua chama chake mbele ya umma wa Watanzania, ni vitendo vya rushwa, siasa chafu yakiwemo makundi na fitna.
Musiba alimuomba Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hoseah kuwapanga vema makamanda wake kwa ajili ya kuwakamata wagombea na watu watakaobainika kutoa rushwa ili wachaguliwe kwenye ngwe hiyo ya kuwania uongozi.
"Nimechukua fomu hii kwa lengo la kwenda kupigania maendeleo ya chama changu tawala. Nitapambana kuhakikisha rushwa, siasa chafu ndani ya CCM vinaondoka, maana ndiyo vitu vinavyokiharibu kabisa chama.
"Kwa maana hiyo, kuanzia sasa naiomba Takukuru ianze kuwafuatilia na kuwakamata wagombea wote watakaoonekana kutoa rushwa wakati huu wa uchaguzi," alisema.
Musiba ni miongoni mwa wanachama 13 waliochukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya NEC kupitia wilaya hiyo.


No comments:

Post a Comment

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad