Tuesday, August 28, 2012

Wakati zoezi la sensa ya watu na makazi likiendelea mwenyekiti wa kitongoji cha Makongoro.B wilayani Bunda mkoani Mara Musa Masenza 42 amefikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo kwa kosa la kumpiga karani wa sensa na kumzuia kufanya kazi


MWENYEKITI  wa kitongoji  cha Makongoro B kilichoko wilayani Bunda mkoani Mara,Mussa Masinza 42  jana amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Bunda kwa tuhuma za kumpiga karani wa Sensa na kumzuia asifanye kazi yake.

Mbele ya hakimu wa wilaya hiyo Safina Simfukwe na mwendesha mashitaka mkaguzi msaidizi wa polisi Masoud Mohamedi kuwa mnamo agost 26 mwaka huu majira ya saa 8 mchana huko katika kijiji cha Makongoro B mwenyekiti huyo alimshambulia karani wa sensa aitwaye Nicholaus Ayega kwa kumpiga.

Mwendesha mashitaka huyo huyo alieeleza mahakama hiyo kuwa wakati mwenyekiti huyo anampiga alikuwa pia akimuzuia asifanye kazi ya kuhesabu watu kwa madai kuwa yeye kama mwenyekiti hana taarifa na zoezi hilo na pia hajaripwa pesa hivyo zoezi hilo haliwezi kufanyika katika kitongoji  ambacho yeye ni kiongozi.

Masoud aliendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa baada ya karani huyo kufanyiwa unyama huo na mwenyekiti huyo alitoa taarifa polisi ambapo pia kamati ya sensa ya wilaya iliyokuwa  katika kijiji hicho ilifanikiwa kumkamata mwenyekiti huo na kumfikisha kwenye kituo cha polisi ambapo alifunguliwa  mashitaka kwa mjibu wa sheria  ya takwimu namba 1 ya mwaka 2002.

Baada ya kusomea shitaka hilo mwenyekiti huyo alikana na kuomba dhamana  ambayo hata hivyo ilipingwa na mwendesha mashitaka kwa madai kuwa kiongozi huyo amekuwa na historia ya matukio ya mara kwa mara na pia kupewa dhamana kutaharibu upelelezaji wa kesi hiyo ambao bado unaendelea  sambamba na kudhoofisha zoezi la sensa linaloendelea hivi sasa kijijini hapo.

Mshiatakiwa huyo amepelekwa mahabusu hadi Sept 10 mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena mahakamani.

Hata hivyo baadhi ya watu waliokuwepo mahakamani hapo wamelipongeza jeshi la polisi kwa kumfikisha kiongozi huyo mahakamani ambapo wamesikika wakidai kuwa huenda akawa mfano kwa wale wote wenye nia ya kuharibu zoezi zima la Sensa linaloendelea hivi sasa nchini kote.

MWISHO

No comments:

Post a Comment

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad