Sunday, October 27, 2013

MIFUGO 184 YAPIGWA RISASI TARIME


Na Berensi Alikadi,Tarime
27.10.2013.
MIFUGO 184 kutoka kaya 22 za Kijiji cha Kegonga kata ya Nyanungu wilayani Tarime mkoani Mara imepigwa risasi na kuawawa  na  askari wanaosadikiwa kutoka kikosi cha kupambana na ujangili katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 7  mchana ambapo mifugo iliyopigwa risasi ni  ng’ombe 67, mbuzi 113 na kondoo wanne waliokuwa wakichunga katika bonde la Nyanungu karibu na hifadhi hiyo na kwamba miili mingine ya mifugo hiyo tayari imeliwa na fisi.

Imeelezwa kuwa kabla ya kufanya unyama huo askari hao waliwakamata watu watatu, Maria Chacha, Matinyi kemore na Bhoke Tarage waliokuwa wakichunga  mifugo hiyo na kutokomea nao ndani ya hifadhi huku wakitelekeza mifugo hiyo ikiwa imekufa.

Akiongea na gazeti jana na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kegonga Chacha Tugara  alieleza kuwa askari hao walikuwa wamevaa sare za askari wa hifadhi ya wanyama pori.
alidai kuwa askari hao ambao idadi yao haikufahamika mara moja walianza kuswaga mifugo hiyo kuwatoa walipokuwa wakichunga katika mwinuko mmoja na kuzielekeza katika bonde hilo kabla ya kuzifyatulia risasi.

Hata hivyo mwenyekiti huyo alikanusha mifugo hiyo kuingia ndani ya hifadhi na kwamba mifugo hiyo ililazimishwa huku akifafanua kuwa hata kama ingekuwa imeingia ndani ya hifadhi lakini si haki kuipiga risasi na kwamba mifugo ilipokuwa ikiingia ndani ya hifadhi kwa bahati mbaya wahusika walikuwa wakitozwa faini na  walikuwa wakilipa faini hizo na kuchukua mifugo yao.

“Kwakweli nisema  tu kwamba serikali itambue kuwa hii nchi ni yetu sote hivyo kuwatendea wananchi vitendo hivi vya kinyama si haki na huu ni uvunjaji wa haki za binadamu na wanyama” alisema Mwenyekiti Huyo.
Alisema pamoja na mifugo hiyo kupigwa risasi hadi jana hakuna vyombo vya usalama vilivyofika katika eneo hilo kwa uchunguzi licha ya taarifa hizo kupelekwa polisi

Alitaja majina ya idadi kaya na ng’ombe zao zilizopigwa risasi kwenye mabano kuwa ni Magaiwa Kemore(7), Ryoba Nyamohanga(2), Mwita Ryoba(3), Daniel Giboswa(2), Chacha Marwa(5), Nchaguru Mokami(3), Buraga Buraga(1).

Wengine ni Mtatiro Marwa(3),Mwita Nyamohanga(3), Charles Petro(4), Chacha Keroka(3), Matiko Wantahe(5), Chacha Matiko(2), Sasi Marwa(1), Mwita Gugura(6), Getaro Teroge(4), Chacha Paulo(3).

Alitaja wengine ni pamoja na Marwa Mwera(2), Juma Kemore(3), Makuru Chacha(2), wambura Nyamhanga(1) na Waisiko Mwita(2) na kwamba wote ni wakazi wa Kijiji cha Kegonga.
Tanzania daima jana imemtafuta mkurugenzi wa Tanapa,Allan Kijazi ii aweze kuzungumzia tukio hilo lakini ambapo alisema yuko nchini China kikazi na kutaka suala hio ailizwe mkuu wa hifadhi ya Serengeti
Mkuu wa hifadhi ya Serengeti aliyejitambulisha kwa jina la Mwakilema alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema kuwa yeye hana taarifa na kwamba taarifa za doria inayoendeshwa hivi sasa yupo msemaji wake ambaye ni meja wa jeshi ambaye hakutaka kumtaja.
Tukio hili linatokea miezi michache baada ya tukio lingine linataka kufanana na hilo kutokea katika Kijiji cha Mariwanda wilayani Bunda ambapo askari kutoka hifadhi ya Serengeti kuswaga mifugo zaidi 50 ndani ya mto Rubana na kufia majini.
…………………………….mwisho………………………………………..

WACHIMBAJI WAFA KWA KUFIKIWA NA KIFUSI.


NA  Berensi Alikadi-Bunda
23/10/2013
WACHIMBAJI wawili wa madini katika mgodi ulioko katika kijiji cha Kamukenga wilayani Bunda mkoani Mara wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo diwani wa kata ya Kiwasi mahali kilipo kijiji hicho,Lawi Nyamajeje alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na mbili alifajili.
Alisema kuwa siku hiyo ya tukio wachimbaji hao waliingia katika shimo hilo kwa ajili ya kuchimba dhahabu na kwamba wakiwa wanaendelea na kazi hiyo ghafula walipolomokewa na kifusi.
Diwani huyo alifafanua kuwa baada ya kufukiwa na kifusi hicho jitihada za kuwaokoa zilishindikana na kwamba walipofanikiwa kuwatoa tayari walikuwa wameshakufa.
Aliwataja waliokufa kuwa ni,Paskali Wiliam 16 mkazi wa kijiji cha Kamukenga na Robert Kamoga 18 mkazi wa wilayani Serengeti mkoani Mara.
Aidha aliongeza kuwa katika tukio hilo watu wawili walijeruhiwa vibaya na kwamba walikimbizwa katika hosptali ya wilaya ya Bunda kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo diwani huyo alisema kuwa baada ya tukio hilo waliweza kukaa na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya Bunda pamoja na wachimbaji ili kuona namna ya usalama wa migodi hiyo ya wachimbaji wadogo wadogo kuendeshwa kwa usalama zaidi.
Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kutokana na tukio hilo
Mwisho




                                                       

Saturday, October 5, 2013

Mamia ya wahamiaji wa Afrika wamekufa maji kisiwani Lampesuda

Mamia ya wahamiaji wa Afrika wamekufa maji kisiwani Lampedusa katika pwani ya Utaliana wakijaribu kukimbilia Ulaya

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad