WADAU WA AFYA
SIMIYU WARIDHIA KUTUMIKA MFUMO WA TIBA KWA KADI.
Na Berensi
Alikadi. Simiyu,
Wadau
wa afya katika halmshauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, wameridhia kutumika kwa mfumo mpya wa utoaji
wa huduma za afya kwa njia ya tiba kwa kadi (TIKA), mfumo unaolenga kupunguza
kero ya upatikanaji wa dawa pamoja na vifaa tiba katika vituo vya afya na
hospitali.
Wadau
hao wamefikia uamuzi huo kwenye washa iliyofanyika kwenye ukumbi wa kanisa
katoliki mjini Bariadi.
Mbali
na kuridhia kutumika kwa mfumo huo mpya, ambao uko chini ya Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya ( NHIF), wadau hao wamedai kuwa ili kupatikana mafanikio ya kutumika kwa
mfumo huo ni vema kuwepo kwa usimamizi
mkubwa wa fedha za zitakazotokana na huduma hiyo.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti walisema uanzishwaji wa mfuko wa afya ya jamii Mjini
(TIKA), kutasaidia wananchi kuweza
kutibiwa kwa uarahisi kuliko ilivyo sasa ambapo wananchi hao uangaika katika
kutafuta fedha za matibabu.
Walifafanua
kuwa mfumo huo wa tiba kwa kadi malengo
yake yana faida kubwa kwa wananchi ambao hawana uwezo wa kuweza kumudu gharama
za matibabu, ambapo walieleza kuwa usimamizi wa fedha za wanachama wa huduma
hiyo ni lazima kuwa mkubwa.
“
tunipongeza serikali kwa kuleta mfuno huu, sisi hatuna shaka ikiwa utaletwa kwa
wananchi wetu, kwani unalenga kutatua kero waliyonayo ya kila siku katika
kupata huduma za afya, pamoja na hayo ni lazima usimamizi wa fedha za wananchi
wetu watakao kuwa wananchama katika mfumo huu, unatakiwa kuwa mkubwa sana ili
fedha zao zisitafunwe na wachache” Alisema Selina Deusi.
Akitoa maelezo ya juu ya faida ya mfumo huo
Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Bima ya Taifa ya Afya Elltruder Mbogolo,
alisema kuwa lengo la kuletwa kwa mfumo huu, itasaidia kupungua kwa kero za
upatikanaji wa dawa pamoja na vifaa tiba katika vituo vya afya na ospitali.
Semina
hiyo iliyokuwa imeudhuliwa na wadau mablimabli wakiwemo, viongozi wa dini,
wazee maarufu, viongozi wa vyama vya siasa, vijana, madiwani wa halmshauri ya
mji, wanawake, pamoja na waremavu, ambapo mfumo wa Tiba kwa Kadi (TIKA)
umelenga kutumika katika halmshauri za miji, manispaa pamoja na jiji.
Akifungua
washa hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Simiyu,Katibu Tawala wa mkoa
huo,Mwanvua Jirumbi amewataka viongozi wa halimashauri zote za mkoa huo
kuhakikisha wanasiamia ipasavyo mradi huo ili mradi huo uweze kuwanufaisha
wananchi.
Washa
hiyo ya siku moja iliwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi madhehebu
ya dini,makundi ya walemavu na vyama vya siasa.
MWISHO