BERENSICHINA,SERENGETI,JULAI
12,2016,.
,Hifadhi ya
Serengeti yakanusha kutowapiga wafugaji,
SIKU CHACHE
BAADA YA WAFUGAJI WILAYANI BARIADI MKOANI SIMIYU KUDAI KUPIGWA NA ASKARI WA
HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI WAKATI WA ZOEZI WA UKAMATAJI MIFUGO INAYOINGIA
HIFADHINI KINYUME CHA SHERIA,HIFADHI HIYO IMEKANUSHA TAARIFA HIZO NA KUSISITIZA
HAKUNA MFUGAJI ALIYEPIGWA NA KAMA YUPO AJITOKEZE HADHARANI,
AKIONGEA NA
WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE MKUU WA HIFADHI HIYO ,WILLIAM MWAKILEMA
AMESEMA HAKUNA MTU YEYOTE ALIYEPIGWA BALI KILICHOKAMATWA NI MIFUGO KUTOKANA NA
WAFUGAJI HAO KUBUNI MBINU MPYA YA KUINGIZA
MIFUGO USIKU NDANI YA HIFADHI KWA AJILI YA KUCHUNGA NA KWAMBA WAO WATAENDELEA
KUWAKAMATA WAFUGAJI HAO KWA SABABU WANAVUNJA SHERIA YA TANAPA,SURA NAMBA 282
KAMA ILIVYOFANYIWA MAREKEBISHO MWAKA 2002
KWA UPANDE
WAKE MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAFUGAJI KANDA YA ZIWA MLIDA MSHOTA AMBAYE
AMEONEKANA KUTOKUWA NA MSIMAMO KUHUSU SUALA HILO ALIPOHOJIWA NA ITV KUHUSIANA
NA MADAI HAYO YA WAFUGAJI AMEKIRI KUWA KUTOKANA NA UHABA WA MALISHO WAFUGAJI
HAO WAMEKUWA WAKIINGIZA MIFUGO HIFADHINI KWA AJILI YA KUCHUNGA KAMA
ANAVYOELEZA,.
BAADHI YA
VIJANA WALIOKUTWA NA CAMERA YA ITV NDANI YA HIFADHI HIYO WAMEKIRI KUTUMWA NA
WAZAZI WAO KUCHUNGIA NDANI YA HIFADHI NA KWAMBA WANAPOJARIBU KUKATAA HUPIGWA NA WAZAZI NA WALIOAJILIWA KUCHUNGA
MIFUGO HUTISHIWA KUFUKUZWA KAZI,
HIVI
KARIBUNI MAKAMU WA RAIS SAMIA SURUHU ALIWAAGIZA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA
KUHAKIKISHA WANAONDOA MABOMA YOTE YA WAFUGAJI YALIYOKARIBU NA HIFADHI ZA TAIFA
HAPA NCHINI.
Mwisho
No comments:
Post a Comment