BERENSICHINA,SIMIYU,JULAI
12,2016,
,wanunuzi wa
pamba wanaotia maji waonywa,
HABARI YA BIASHARA
SERIKALI MKOANI SIMIYU
HAITAPOKEA PAMBA ILIYOWEKEWA MAFUTA YA KENGE KWA MADAI YA KUONGEZA KILO
,PAMBA INAYOWEKEWA MCHANGA NA MAJI KWANI KUFANYA HIVYO KUNAPUNGUZA UBORA WA
PAMBA KATIKA SOKO LA DUNIA NA BADALA YAKE BEI KUENDELEA KUSHUKA NA HIVYO
WAKULIMA KUKATA TAMAA KULIMA ZAO HILO NA KUJIKITA KATIKA MAZAO YA CHOROKO NA
DENGU ..
AGIZO HILO LIMETOLEWA
NA MKUU WA MKOA WA SIMIYU ANTHONY MTAKA WAKATI WA MKUTANO BAINA YA WANUNUZI
WA PAMBA NA WENYEVITI WA HALMASHAURI ZA WILAYA KUELEKEA MSIMU WA
UNUNUZI WA ZAO LA PAMBA AMBAPO BAADHI YA MAKAMPUNI YAMEANZA KUNUNUA
,ILI KUJUA BEI ELEKEZI IWAPO INAZINGATIWA .
AMESEMA KUWA MKOA WA
SIMIYU UNAZALISHA ZAO LA PAMBA NCHINI KWA ASILIMIA 60 AMBAPO MWAKA JANA
ZILINUNULIWA KILO MILIONI 70 ZA PAMBA HIVYO KAMA MKOA HAWATAKUBALI KUONA ZAO
HILO LINATOWEKA KUTOKANA NA WATU WACHACHE KUJENGA MAZOEA YA KUIWEKEA
MAJI PAMBA,MAFUTA YA KENGE NA MAWE LAZIMA HATUA ZICHUKULIWE DHIDI YAO
KURUDISHA UBORA WA ZAO HILO KATIKA SOKO LA DUNIA.
AIDHA MKUU HUYO WA
MKOA AMETUMA SALAAM KWA WANUNUZI WA
ZAO HILO WANAOHARIBU MIZANI NA KUWAIBIA WAKULIMA NA KUWATAKA WAACHE MARA MOJA
KWA UPANDE WA WADAU WA
PAMBA WAMEYATAKA MAKAMPUNI YA UNUNUZI KULIPA USHURU WA AWALI KATIKA
HALMASHAURI HUSIKA KABLA YA KUANZA UNUNUZI.
MWISHO,
|
No comments:
Post a Comment