Tuesday, September 19, 2017

Kamanda wa Polisi Mara akiwa katika picha na washiriki wa kikao kazi,kilichofanyika mjini Bunda

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ,Jafari Mohemdi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kikosi kazi toka hifadhi ya serengeti na ofisi ya wakili wa serikali ,mkoani Mara, picha na Berensi china

NGO'MBE 345 WAPIGWA MNADA MEATU



Na Berensichina,sept 17,2017,ngombe 345 wapigwa mnada,
hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa simiyu john nkwabi ameamuru kutaifishwa na kipigwa mnada jumla ya  ngombe 345 waliokamatwa wakichunga katika pori la akiba la maswa kinyume cha sheria ya wanyamapori
akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mnada huo uliofanyika wilayani meatu meneja wa pori la akiba la maswa lusato masinde amesema wameamua kuuza mifugo hiyo baada ya mahakama kutoa  amri kulingana na sheria ya wanyama pori namba 5,2009 kifungu cha 111.
aidha meneja huyo amewaonya wafugaji ambao watakaidi agizo la mhe.rais la kuondoa mifugo yao kwa hiyari na kuacha kuchungia katika pori hilo  kwani msako wa kukamata mifugo hiyo ni endelevu na mifugo itakayokamatwa itaendelea kutaifishwa kwa mjibu wa sheria
kwa upande wake darali aliyesimamia zoezi la kuuza ngo’mbe hao kutoka kampuni ya abajaja christopher kabenga amewataka wanunuzi wote kuhakikisha wanatembea na stakabadhi halisi waliyopewa wakati watakapo kuwa wanasafirisha mifugo hiyo ili kuepuka usumbufu njianii

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mara Jafari Mohemed akiongea mara baada ya kikao kazi kumalizika


RPC MARA AHIDI USHIRIKIANO NA ASKARI WA SERENGETI



na Berensichina,bunda,sept20,2017,Rpc Mara ahidi ushirikiano na askari wa hifadhi ya Serengeti.
kamanda wa polisi mkoa wa mara kamishina msaidizi wa polisi jafari mohamed amesema jeshi la polisi mkoani mara litahakikisha linashilikiana na askari wa hifadhi ya taifa ya serengeti katika kuhakikisha wanakomesha vitengo vya ujangili katika hifadhi hiyo,
kamanda jafari ameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi kilichofanyika wilayani bunda ambacho kimewahusha wahifadhi toka hifadhi ya taifa ya serengeti waendesha mashitaka  wakuu wavitengo vya ulinzi wa wanyamapori na ofisi ya mwandesha mashitaka mkoa wa mara lengo likiwa ni kuweka mkakati namna ya kupambana na ujangili,
akizungumza kwa niaba ya wahifadhi wa hifadhi hiyo,mhifadhi emanuel matungwa amesema changamoto ya ujangili katika hifadhi hiyo ni kubwa kwani kila kukicha majangili wanabuni mbinu mpya hivyo jitihada za pamoja zinahitajika katika kupambana na vitendo hivyo,
kwa upande wake wakili wa serikali mwandamizi toka  wa mkoani mara anisus kahindura,amesema ofisi yake imejipanga ili kuhakikisha kesi za nyara zinamalizika mapema ili kuondoa msongamano wa kesi hizo mahakamani

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad