Na Berensi
Alikadi.
30/8/2013
LEO ni mwaka
mmoja tangia kifo cha aliyekuwa mwandishi wa kituo cha chanel ten mkoani Iringa
Marehemu Daudi Mwangosi.
Kama
tunavyofahamu Mwangosi aliuwawa na polisi sept 2mwaka 2002 akiwa kazini huko
katika kiijiji cha Nyaroro wilayani Mfindi mkoani Iringa ambako alikuwa
amekwenda kuandika habari za mkutano wa chama cha demkorasia na maendeleo
[Chadema].
Siku hiyo
Mwangosi alikwenda pale kijijini akiwa katika majukumu yake ya kikazi ambako
alitaka kuwahahabarisha wananchi kilichosemwa katika mkutano huo lakini maskini
hakuweza kutimiza lengo lake na badala yake polisi kwa amri ya Kamuhanda
walimugeuza uji.
Hakuna
ubishi katika hilo kuwa mwandishi huyo hakuuwawa na polisi kwani taarifa za
awali toka kwa waandishi wenyewe wa mkoa wa Iringa zinasema kuwa aliyekuwa
kamanda wa polisi mkoa huo Michael Kamuhanda ambaye bado serikali inamkumbatia
aliitisha mkutano na waandishi wa habari ofisini kwakwe na katika mkutano huo baada ya kueleza adhima
yake ya kuuzuia mkutano wa chadema,marehemu mwangosi alionekana kuumuliza
maswali mengi ambayo yalionekana kumukera kamanda huyo.
Maswali ya
Mwangosi kwa kamanda huyo wa polisi
huenda ndiyo yaliongeza chuki nap engine kuongeza hasira ya siku nyingi ambayo
alikuwa nayo dhidi yake na hivyo akamuweka kiporo.
Taarifa
zinaonyesha kuwa mara baada ya mkutano huo baadhi ya askari polisi waliwazuia
waandishi wasiende kwenye mkutano huo jambo ambalo kwa mwandishi ni kosa kwani
yeye pia anatakiwa kutimiza majukumu yake kama polisi walivyokwenda kwenye
mkutano huo.
Habari
zilieleza kuwa baada ya waandishi wa habari kufika katika eneo la kijiji cha
Nyaroro na kufanikiwa kukusanya habari
walielekea kwenye eneo la kusini mashariki kupitia barabara kuu Dar-Tunduma mahali ambalo ndipo alipouwawa
mwangosi
Katika eneo
hilo polisi waliwapiga waandishi wa habari na viongozi wa chadema pasipo sababu
waandishi waliopigwa ni pamoja wale waliokuwa wakiandikia magazeti ya
nipashe,mtanzania,Tanzania daima lakini adhima yao kuu ilikuwa kumua Mwngosi
jambo ambalo walilitimiza pasipo kuacha shaka.
Siku hiyo ya
tukio wakati baadhi ya waandishi walipokuwa wakipigwa na polisi, Mwangosi
alimukimbilia kamanda Kamuahanda na kumuomba awamuru polisi wake waache kumpiga mwandishi wa gazeti la
nipashe Godfrey Mushi lakini hakumuelewa wala kumusikiliza na badala yake walimushika na kumugeuzia
kibao na kuanza kumpiga hadi askari mwingine alipomupiga na bomu tumboni
lililosambaza mwili wake huku kamanda Kamuahanda akishuhudia na huo ndio ukawa
mwisho wa maisha ya Daudi Mwangosi.
Leo
tunapotimiza mwaka mmoja tangia kifo cha mwandishi huyo hatuna budi kutafakali
vitendo vya kikatili vinavyofanyiwa waandishi wa habari huku serikali
ikiangalia pasipo kuchukua hatua.
Hivi ndugu
msomaji hata wewe una kila sababu ya kujiuliza kulikuwa na sababu gani ya
kuwazuia waandishi wa habari kwenda kwenye huo mkutano ,walikuwa na kosa gani
hata kama wangepiga picha.
Katika hali
ya haraka Napata picha kuwa siku hiyo polisi walikuwa na ajenda yao ya siri
kama kawaida yao na ndio maana hawakutaka waandishi wafike huko na pingine
huenda walipanga kabisa kuwauwa viongozi wa chadema na kuwepo kwa waandishi
kulizima adhima hiyo na ndio maana hasira zao walimalizia kwa kuwapiga na
kumuua Mwangosi.
Waandishi wa
habari siku zote wako kazini kwa kufuata taratibu zao na namna walivyofundishwa
kufanya kazi na wala hawafanyi kazi zao kwa kuamuliliwa na polisi lakini cha
kushangaza sasa polisi wamekuwa wakiwakiwaingilia na hata kuwazuia kufanya kazi
jambo ni ukiukwaji wa katiba ya nchi ibara ya 18.
Kwa miongo
mingi sasa wananchi wamekuwa wakishuhudia namna waandishi wanavyonyanyaswa na
jeshi la polisi,wako waliowahi kupigwa,kungo’lewa kucha,kumwagiwa tindikali
kuporwa vifaa vyao vya kazi kama kamera na sasa mwaka jana dunia imeshuhudia
waziwazi jeshi hili chini ya kiongozi aliyekabidhiwa kuuongoza mkoa akisimamia mwandishi
anauwawa kwakweli inatisha na inaumiza sana.
Ni waandishi
hawa hawa ambao kila siku polisi wanapokamata majambazi wale wasiowapa rushwa
na vitu vile ambavyo huwa hawana mgawo huwaita na kuuza sura zao ili jamii
iwaone kama kweli wanafanya kazi kumbe wengi wao ni mafisadi wakubwa.
Kilichonishangaza
zaidi ni pale serikali hadi leo imemukingia kifua Kamuahanda huku kesi hiyo
akipewa askari mdogo ambaye pia kila kukicha polisi wenzake wamekuwa
wakimfanyia maagizo hata wakati wa kumpeleka mahakamani jambo linaloonyesha
dhahili kuwa mauaji ya Daudi Mwangosi yalipangwa na wala si vinginevyo.
Nilitegemea
sana rafiki yangu Nchimbi atamuchukulia hatua ya kinidhamu Kamuahanda lakini
matokeo yake akahamishiwa makao makuu ya polisi ili kumficha huko wananchi
wasifahamu kinachoendelea zaidi na hadi leo imekuwa kimya hakuna hata kiongozi
wa polisi wala serikali wanaoweza kuzungumzia suala hili licha ya tasinia hii
pia kuwa na wizara kamili.
Jeshi la
polisi liliundwa kwa ajili ya kulinda
raia na mali zao wakiwemo waandishi wa habari lakini cha kushangaza leo jeshi
hili limekuwa kinala wa kuuwa na wa kwanza pia kukimbilia kukanusha kwa kutumia
vyombo vyao vya serikali kama vile TBC na magazeti ya uhuru na mzalendo ili
kuwapoteza wananchi pasipo kufahamu kuwa wananchi leo hawadanganyiki.
Wakati leo
wanahabari hapa nchini wanaungana na watanzania wengine katika kukumbuka mauji
haya ya kinyama aliyofanyiwa Mwangosi hatuna budi kulaani kwa nguvu zetu na
kulitaka jeshi la polisi liache kutumika kiasiasa.
Hatuna budi
kuitaka serikali itamuke ni lini itawalinda waandishi wa habari wawapo kazini
na ni lini polisi wataacha uhasama na waandishi wa habari maana kila kukicha
chuki kati ya waandishi na jeshi hili inazidi kuongezeka kutoka na vitendo vya
uonevu wanavyofanyiwa wakiwa kazini.
Polisi
watambue kuwa waandishi ni sehemu ya jamii ya kitanzania nayo ina haki sawa
katika nchi hii na pia inafahamu maovu mengi na kama siku ikiamua kumwaga mboga
basi hapo ndipo kutakapokuwapo kilio na kusaga meno.
Waache
vitisho na kuingailia uhuru wa habari waache waandishi wafanye kazi zao kama
tasnia uhuru wakumbuke hayo mabomu waliyotumia kumuua Mwangosi ni kodi yetu
wananchi wakiwemo waandishi wa habari.
Leo familia
ya Daudi Mwangosi inataabika lakini Kamuhanda anaishi maisha mazuri tena
ameongezewa cheo kumbe polisi akiuwa mwandishi anaongezewa cheo na gari zuri la
kiyoyozi hakuna hatua zilizochukuliwa na lakini naamini mungu yupo na damu ya
Mwangosi itaendelea kumulilia siku hadi siku.
Waandishi wa
habari leo hawana uhuru wa kufanya kazi katika nchi yao,hawana uhuru wa
kuhudhulia hata mikutano ya kisiasa hususa ni ile ya vyama vya upinzani kasoro
ya chama cha mapinduzi ambacho hata kama kikikosea polisi husema amina’’.
Ndiyo maana
waandishi sasa tunaomba katiba ijayo waandishi watambuliwe na uwe mhimili
kamili kama mihimili mingine kwani wana mchango mkubwa katika nchi hii na
tunataka tuachwe huru na hatutaki kuingilia na polisi na kupigwa mabomu pasipo
sababu.
Tunataka
polisi waache kutugeuza kama kiti moto bali watautambue na watuheshimu kama
wanavyoheshimu hao wanaowatuma kutupiga mabomu na wafahamu kuwa hiyo kazi ina
mwisho na mwisho wao siku zote huwa ni mbaya na wengi wao wamekuwa wakikimbilia
kuomba msaada kwa waandishi ili waweze kuandikiwa mambo yao pindi wakwamapo
kulipwa mafao yao ya kusitaafu uhamisho nk.
Sisi wote ni
watanzania wala polisi wasijione wao wako juu ya sheria na kutukandamiza lazima
waandishi wote tuungane kwa nguvu zetu na tukatae biashara hii ya polisi
kutufanya sambusa kila mtu ana haki ya kutimiza wajibu wake kikazi hivyo hata
mwandishi kuhudhulia mkutano ni haki yake na tunataka polisi msituchagulie cha
kuandika nyie milisomea mguu pande na sisi tulisomea kuandika hivyo tuacheni
tulivyo na kalamu zetu na nyie na bunduki zenu lakini mkijua hiyo ni kodi ya
walalahoi na siyo ya kwenu.
Tunayo kila
sababu ya kulaani vitendo viovu dhidi ya polisi wanavyofanyiwa waandishi
kumbukeni haya manyanyaso hayakuanzia kwa Mwangosi tu bali wako wengi akina
Katabalo na wengine mnaowafahamu sasa lazima tusema manyanyaso ya polisi dhidi
ya wanahabari sasa basi.
Damu ya
Mwangosi iliyomwagika akiwa anatetea kazi yake iwe chachu kwa waandishi wote
hapa nchini,tutafakali kwa pamoja juu ya maisha yetu ya kila siku na namna
tunavyowindwa ili roho zetu ziondoke,lazima tumukumbuke mwenzetu kwa uchungu
mkubwa na tuongeze msikamano katika kudai haki yetu ya kupata habari mahali
popote.
Kamwe
ushujaa wako hautasaulika katika tasinia ya habari kila kizazi naamini kitasoma
historia yako ambayo itaandikwa kila kukicha na wapenda haki sisi tunaamini
ulikufa katika haki na tutaendelea kukumbuka kila siku na mchango wako katika
habari utakumbukwa daima siku zote.
Lakini kwa
jeshi la polisi hususa ni kamanda Kamuhanda lazima atatmbue kuwa kila kukicha
damu ya Mwangosi itaendelea kumulilia kila siku maana bila yeye Mwangosi bado
tungekuwa naye.
Tunasema
Mwangosi amepumzika lakini tuliobaki tutaendeleza mambano ya kutetea uhuru wa
kupata habari pasipo kuogopa vitisho vya polisi.
Pumzika kwa
amani Kamanda Mwangosi.