Thursday, May 22, 2014

Mkuu wa mkoa wa simiyu Paschal Mabiti akikata utepe kuzindua kampeni ya uzazi wa mpango mkoani simiyu,kwenye viwanja vya sabasaba mjini Bariadi,jana.mei 21

Mkuu wa mkoa wa simiyu,Paschal Mabiti akipeana mkono na katibu tawala wa mkoa huo,Mwanvua Jirumbi mara baada ya kuzindua kampeni ya uzazi wa mpango mkoani humo iliyofanyika katika uwanja wa sabasaba mjini Bariadi jana

UZAZI WA MPANGO WAZINDULIWA SIMIYU



NA BERENSI ALIKADI,SIMIYU
MEI 22,2014,

Imeelezwa kuwa wanawake tkribani 454 kati ya vizazi  100,000 hufa kila mwaka kutokana na uzazi.
Mganga mkuu wa mkoa wa simiyu,Dr,Mageda Kihurya mjini Bariadi kwenye uzinduzi wa kampeni ya uzazi wa mpango ngazi ya mkoa iliyojulikana kama nyota ya kijani.
Alisema tafiti zinaonyesha kuwa upo uhusiano mkubwa  kati ya matumzi ya uzazi wa mpango na afya ya mama na mtoto na kwamba matumizi haya yanawez kupunguza vifovitokanavyo na  na uzazi kwa asilimia 44 na kupunguza vifo vya  kupungza vifo vya watoto kwa asilimia 10-12.
Dr Mageda alisema  hiyo ni kwa sababu ya uzazi wa mpango humuwezesha mama kupumzika kati ya mimba moja hadi nyingine na pia humsaidia  mama kuepuka  mimba zisizotarajiwa na hivyo kupunguza tatizo la utoaji mimba holela
Aidha alifafanua kuwa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012 inaonyesha kuwa nchi yetu ina idadi ya  ya watu milioni 45 ikiwa ni ongezeka la  kasi,idadi isiyowiana na ongezeko la pato la kiuchumi la nchi yetu hali inayotulazimu sisi sote kuongeza juhudi katika kuwekeza kwenye huduma za jamii kama vile elimu na afya.
Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la misaada la Marekani USAID  kupitia chuo  kikuu cha John Hopkins,,Dr Rose Madida aliwataka wanawake kuzaa kwa kufuata uzazi wa mpango na kuachana na mila potofu kuwa kuzaa watoto wengi  utajili.
Baadhi ya wananchi wanaotumia uzazi wa mpango mkoani hapa wamelitoa ushuhuda wao na kueleza kuwa uzazi wa mpango ni njia sahihi ya kumsaidia mtu kujua namna atakavyoweza kuituza familia aliyonayo.
Akizindua mpango huo mkuu wa mkoa wa Paschal Mabiti pamoja na kuupongeza mpango huo ameziagiza halimashauri za wilaya mkoani humo kupanga bajeti kwa ajili ya kuusaidia mpango huo na kwamba hata serikali kuu itahakikisha inafanya hivyo.
Uzinduzi huo ulioenda sambamba na upimaji wa virusi,ufungaji wa uzazi na mafunzo ya uzazi salama toka katika mashirika mbalimbali kama vile umati,Amreef na Ingenderheath.
mwisho

Sunday, May 18, 2014

Shirika rasmi la habari nchini Uchina Xhinua limesema kuwa serikali imewaondoa zaidi ya raia wake 3000 nchini Vietenam.
chanzo,bbc
Naibu waziri wa maji,Amosi Makala aliyesimama akiongea na wananchi wa kijji cha Mwanjoro wilayani Meatu wakati alipokwenda kutembelea bwawa la Mwanjoro juzi,mei 16.2014

Mkurugenzi wa halimashauri ya wilaya ya Maswa akimshukuru meneja wa kanda ya mashariki wabenki ya Nmb,Agustino Abraham mara baada ya kukabidhi madawati 64 yenye thamani ya shilingi milion 5kwa shule za msingi kata ya Malampaka wilayani Maswa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu,Charles Mkumbo akionyesha bunduki zilizokamatwa katika msako unaoendelea mkoani humo

Haya ni mabaki ya nyumba iliyogongwa na bus la kampuni ya Luhuye wilayani Busega

Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Paschal Mabiti akipewa maelezo juu ya ujenzi wa benki ya CRDB wilayani Maswa.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Paschal Mabiti akijaribu kulima kwa kutumia jembe la Ngo'mbe wakati alipokuwa akikagua mashamba ya wakulima katika kijiji cha senani wilayani Maswa.

Tanki la maji wilayani meatu wananchi wameanza kunufaika na mardi wa maji

Fuvu la kichwa cha Tembo ni moja wapo ya vivuti hapa nchini

Hii ndiyo nyumba ya aliyekuwa mlemavu wa ngozi alibino,Munghu Lugata ambaye aliuwawa na watu wasiojulikana.

viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Baraidi wakitoa heshima katika kaburi la mwanamke mlemavu wa ngozi alibino ,Munghu Lugata aliyekuwa mkazi wa kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi mkoani Simiyu ambaye aliuwawa Mei 12 majira ya saa sita usiku na kicha kuondoka na viungo vyake.

Mkuu wa wilaya ya Baariadi ,erasto sima akiimba pamoja na kwaya ya walimu wa mkoa wa Simiyu kwenye maadhimisho ya juma la elimu mjini Bariadi

Add caption Wanafunzi wa shule mbalimbali wilayani Bariadi mkoani Simiyu wakiwa wamebeba mabango katika maandamano ya juma la elimu mkoani simiyu

SERIKALI KUTOIPA KAZI YA KUCHIMBA MABWAWA,KAMPUNI YA NYAKILANG’ANI

NA MWANDISHI WETU MEATU SIMIYU,MEI 18,2014.


serikali imesema kuanzia sasa haitaipa kampuni ya ujenzi Nyakirang’ani
 ya mkoani mara kazi yeyote ya kuchimba mabwawa baada ya kampuni
kushindwa kukamilisha kazi za mabwawa mbalimbali hapa nchini.


kauli  hiyo ya serikali imetolewa wilayani meatu mkoani simiyu  na naibu
waziri wa maji,amosi makala mara baada ya kutembelea bwawa la mwanjoro
ambalo lilikuwa likijengwa na kampuni hiyo.

amesema  mkandarasi huyo ameonyesha kiwango cha chini katika ujenzi wa
mabwawa anayopewa na kwamba kuanzia sasa hatapewa kazi yeyote ya
ujenzi wa mabwawa na wizara hicho hapa nchini kwani  amekuwa
mkandarasi mbabaishaji na asiye na uwezo licha ya kupewa kazi hizo na
wizara.
‘’Nimefika mwenyewe nimejionea hali halisi ilivyo na nimeacha watalaam
wa wizara yangu waweze kufanya tathimini na watuleteea kabla
hatujasoma bajeti na mkandarasi huyu nimesema yeye na wizara yetu sasa
basi hatuwezi kupata hasara kwa kuwavumilia wakandarasi
wababaishaji.’’alisema Makala



mkuu wa wilaya hiyo.Rose mary kirigini
alimueleza naibu waziri huyo bwawa hilo lilianza kujengwa tangia mwaka
2009 hadi sasa na kwamba taarifa imekuwa ikionyesha kuwa limekamilika
kwa asilimia 80 jambo ambalo si kweli.na kwamba wakati umefika sasa
,kwa wananchi wa vijiji hivyo kulitumia bwawa hilo kwani wametaabika
kwa muda mrefu sana


Awali mhandisi wa maji toka sekretalieti ya mkoa,Gibson Kisaka amesema
 hali ya upatikanaji wa maji katika mkoa huo haitoshi kutokana na
vyanzo vingi kuwa na maji yenye madini ya frolide na kwamba
wanaangalia uwezo wa kuongeza idadi ya mabwawa ili yaweze kukidhi
haja.

kwa upande wao wananchi wa vijiji vya mwanjoro  na jinamo mahali
lilipo bwawa hilo wameiomba serikali kulisimamia bwawa hilo ili liweze
kukamilika kwani wamekuwa wakipata shida ya maji.
 Wananchi hao wamesema kuwa wamekuwa wakifuta maji kwa umbalimrefu kwa
kutumia wanyama  aina ya punda na kwamba bei ya maji kijijini hapo ni
shilingi mia tano kwa ndoo moja.
Makala anatembelea maeneo mbalimbali yaliyo na kero ya maji kabla ya
kuwasilishwa kwa bajeti ya wizara hiyo  tarehe 30mwezi huu.
mwisho
Why this ad?Ads –
Uroa Bay Beach Resort Is what we do best

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad