Sunday, July 30, 2017

Ukataji miti wazidi kushamiri pori la Maswa

Vitendo vinavyoweza kutafsiriwa kama ni kuhujumu ustawi wa misitu muhimu kwa ustawi wa sekta ya utalii nchini, vimeendelea kukithiri hususan ukataji miti, ambao umekuwa ukifanywa na watu mbalimbali katika misitu mbalimbali nchini, likiwemo pori tengefu la Maswa. 

Hivi karibuni, kamera ya Serengeti Wildilife & Nature Conversation, ilitembelea pori hilo, na kushuhudia miti iliyokatwa na wananchi hao wasio na nia njema kama picha zinavyoonekana. 




Baadhi ya miti iliyokutwa imekatwa wakati wa ziara hiyo fupi ya kikazi.

Askari wa pori hilo, ambao wameelezea kusikitishwa na vitendo vua ukataji huo wa miti ambavyo vimekuwa vikifanywa kwa ujanja mkubwa katika kuwakwepa askari wanaolinda pori hilo






Serengeti Wildlife & Nature Conservation yapokea wageni

Asasi inayojihusisha na harakati za utunzaji wa rasilimali za utalii nchini ya Serengeti Wildlife & Nature Conservation, yenye makao yake makuu mkoani Simiyu, hivi karibuni ilipokea ugeni wa wadau wake toka nchi kadhaa za barani Ulaya, ambapo pamoja na kutaka kujua shighuli zinazofanywa na asasi hiyo, wageni hao pia waliweza kutembezwa katika hifadhi ya Serrengeti, na kujionea vivutio kadhaa vya utalii hifadhini humo. 

Pichani, ni wadau hao walipokuwa wameongozana na mwenyekiti wa asasi ya Serengeti Wildlife & Nature Conservation, ambaye pia ni mmiliki wa blogi hii, wakati wa ziara hiyo fupi. 





Ahukumiwa miaka 40 jela kwa kukutwa na nyama ya nyumbu

Huha Makuja Nyungi (kushoto), akiwa anaelekea mahakamani muda mfupi kabla ya kusomewa hukumu hiyo. Kulia ni mtuhumiwa mwingine katika kesi hiyo

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Simiyu, imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 40 jela mkazi mmoja wa huyo ni mkazi wa kijiji cha Girya, mkoani humo, huku Jeshi la Polisi likiwashikilia watuhumiwa wengine wawili, kutokana na kukutwa na nyara za serikali pasipokuwa na kibali cha Mkurugenzi wa wanyama pori. 

Huha Makuja Nyungi, mwenye umri wa miaka 28, alihukumiwa kifungo hicho baada ya kukiri makosa ya kuhusika na kosa la kukutwa na nyara hizo, mbele ya Hakimu Mfawidhi John Nkwabhi. 

Bw. Nyungi, pamoja na wenzake wawili ambao majina yao hayakuweza kupatikana haraka, walikamatwa kufuatia msako mkali ulioendeshwa kwa ushirikiano baina ya askari wanyamapori na taasisi ya Serengeti Wildlife and Conservation, ya mkoani Simiyu. 


Katika msako huo, mali mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 za kitanzania, vikiwemo vipande zaidi ya 500 vya nyama ya nyumbu, ziliweza kukamatwa. 


Akisoma hukumu hiyo, hakimu Nkwabhi, alisema anamhukumu mtuhumiwa adhabu hiyo ili iwe fundisho na onyo kwa watu wengine ambao wamekuwa wakijihusisha na uwindaji haramu, usiozingatia taratibu za kisheria. 

Huha Makuja Nyungi (kulia akiwa na mtuhumiwa mwingine wa kesi hiyo, ambaye alirudishwa rumande kwa kuwa alikataa kushiriki kutenda kosa hilo

Mwenyekiti Kamati ya Usalama Barabarani Simiyu ashiriki RSA Day Dodoma na kutunukiwa cheti

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani mkoa wa Simiyu, Belensi Alikadi, ambaye pia ni mmiliki wa mtandao huu, alipata fursa ya kuungana na wanaharakati mbalimbali wa masuala ya usalama barabarani, kwenye kuadhimisha Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani nchini Tanzania. 

Tukio hili ambalo lilifanyika kwa mara ya kwanza mkoani Dodoma mwaka huu, liliandaliwa na Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Barabarani nchini (RSA Tanzania), mtandao ambao Bw. Belensi ni miongoni mwa wanachama wake. 

Katika tukio hilo, aliweza kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa ngazi mbalimbali katika Jeshi la Polisi upande wa kikosi cha Usalama Barabarani, sanjari na wale kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), ambapo waliweza kubadilishana mawazo kuhusu changamoto kadhaa zinazoikabili sekta ya usafirishaji nchini, na namna ya kukabiliana nazo.

Aidha, kwa kutambuliwa mchango wake katika harakati za usalama barabarani, pamoja na kuikuza taasisi hiyo katika mkoa wa Simiyu, Bw. Alikadi, pia alitunukiwa cheti cha shukrani kwa juhudi zake hizo

Pichani, ni Mwenyekiti huyo akiwa katika matukio mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.
Akiwa na cheti cha shukrani alichotunukiwa na Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani nchini, wakati wa hafla ya kuwatambua mabalozi wenye mchango mkubwa kwa taasisi hiyo

Katika viwanja wa Mashujaa mjini Dodoma, ambapo mabalozi walikutana kwa ajili ya maadhimisho ya siku hiyo. Mwenyekiti (mwenye suti nyeusi), akifurahia jambo na mabalozi wenzake.


Mwenyekiti Belensi Alikadi (wa pili kutoka kulia), akiwa na Mkurugenzi wa Usafirishaji kwa njia ya Barabara toka SUMATRA, Johansen Kahatano mwenye shati la drafti, na mabalozi wengine wakati wa maadhimisho hayo


Mwenyekiti Belensi Alikadi (wa pili kutoka kulia), akiwa na Mkurugenzi wa Usafirishaji kwa njia ya Barabara toka SUMATRA, Johansen Kahatano mwenye shati la drafti, na mabalozi wengine wakati wa maadhimisho hayo
Wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma, kuhudhuria tukio hilo kubwa na la kihistoria kwa harakati za usalama barabarani nchini. 

Akiwa na katibu wa RSA Mkoa wa Simiyu


Tukio hilo liliambatana na michezo mbalimbali. Hapa, Bw. Alikadi akiwa na kikosi cha RSA Yanga, ambacho kilishindana na RSA Simba siku hiyo

Akiwa na Kamanda mpya wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Afande Fortunatus Musilimu wakati wa hafla hiyo

HEPATITIS B: Ugonjwa usiotibika ukiupata, unaokingika ukiuwahi.

Ugonjwa wa Hepatitis B Virus (HBV) kwa Kiswahili homa ya ini.Hivi sasa ugonjwa huu unatishia maisha ya watu wengi hasa wazima, kuliko hata ukimwi.Lakini kwa kutokuufahamu vyema,watu wengi hawauogopi kama wanavyoogopa Ukimwi. 

Ugonjwa huo unaambukiza siyo tu kwa kuchanganya damu kama ulivyo ukimwi,lakini pia kwa njia ya mate (busu),ute wa sehemu za siri na pia jasho.

Wataalamu wanasema kuanzia pale unapombukizwa hadi kuchukua uhai wa mtu ni miezi 6 tu. Ni hatari kwelikweli.

Unaua kwa kushambulia ini ambalo hubunguliwa na kuliletea magonjwa mbalimbali iliwemo kansa ya ini na ini kupukutika.

Vipimo
Kwa jijini Dar unaweza kupima HBV kwenye hospitali yoyote kubwa.Kwa upande wa Muhimbili wanachaji 85,000 kwa vipimo; kwani wao wanashauri ufanye na vipimo vingine pia ikiwemo mimengenyo ya ini yaani liver enzymes etc. Ukiwa na Bima ya Afya gharama haziumizi sana.

Hospitali za AAR wanapima kwa gharama ya 25,000/-. Pia maabala ndogo ndogo kadhaa mitaani zinapima, ikiwemo mojawapo ambayo iko jirani na kanisa la Gwajima, Ubungo ambao hupima kwa 10,000.

Ukipima,kuna mambo mawili;kukutwa nao au kukutwa negative.Ukikutwa positive,tafuta ushauri wa daktari.

Na ukikutwa negative unaenda kuchoma sindano za kinga katika hospitali yoyote hasa ya serikali.Kuna malipo.Yanatofautiana kati ya hospitali moja hadi nyingine.Habari njema ni kwamba hivi karibuni serikali imetangaza kupunguza bei ya chanjo hiyo.Lakini ziliadimika sana hapa karibuni.

Utaratibu wa kuchoma
Kinga ya kwanza: Mara baada ya kupima
Kinga ya Pili:Baada ya mwezi mmoja
Kinga ya Tatu:Baada ya miezi 6

Tujipende.Tujitunze.Tukapime.Tujilinde.Magrupu haya yasaidie na afya pia

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad