Saturday, August 5, 2017

VIDEO: wavamia msafara wa rais Magufuli, wakitaka aongee nao

Mwishoni mwa wiki hii, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, akishirikiana na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni, walizindua ujenzi wa bomba la mafuta ghafi, litakalojengwa kutokea Hoima nchini Uganda hadi kijiji cha Chongoleani, mkoani Tanga. 

Hata hivyo, akiwa njiani kuelekea Tanga kuhudhuria tukio hilo kubwa, rais Magufuli, alilazimika kusimama njiani baada ya wananchi kuusimamisha msafara wake, wakitaka aongee nao, jambo ambalo alilitekeleza, kama inavyoonekana katika video hii

MAGUFULIA NA MUSEVENI WAWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA HOIMA HADI TANGA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa pongezi na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku Viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mbalimbali waliohudhuria shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Chongoleani kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka nchini Uganda hadi Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika uwanja wa ndege wa Tanga mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono pamoja na mke wake Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakiagana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika uwanja wa ndege wa Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza ngoma ya msanja na Mama Janeth Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kumsindikiza Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika uwanja wa ndege wa Tanga.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika viwanja vya Chongoleani kabla ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wakielekea kuweka jiwe hilo la msingi.
Wasanii wakitumbuiza katika uwanja wa Chongoleani.
Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa bomba la mafuta
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii mbalimbali mara baada ya kutumbuiza.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akihutubia katika viwanja vya Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga. PICHA NA IKULU


Thursday, August 3, 2017

Matukio wakati wa RSA Day 2017, mjini Dodoma

Hivi karibuni, Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA Tanzania), uliadhimisha siku ya mabalozi wa usalama barabarani mwaka 2017, ambapo katika maadhimisho hayo, mbali ya uelimishaji wa abiria katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani tokea mjini Dodoma, maandamano na hotuba mbalimbali, pia michezo na burudani mbalimbali zilipamba maadhimisho hayo, kama inavyoonekana katika video zifuatazo.


Mmoja wa mabalozi wa Usalama Barabarani,ambaye pia ni msanii, akitumbuiza wakati wa maadhimisho hayo


Mbali ya shughuli za uelimishaji, siku hiyo ilihitimishwa na michezo kadhaa, ukiwemo huu wa kukimbiza kuku. 

IGP Sirro, atembelea Ubungo kujionea huduma za usafirishaji

Hivi karibuni, Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro, alitembelea kituo cha mabasi yaendayo mikoani kutokea jijini Dar es Salaam, Ubungo kwa ajili ya kujionea namna gani huduma za usafirishaji wa abiria zinaendeshwa kituoni hapo.

Hapa ni alichokisema IGP Sirro, baada ya ziara hiyo ambayo ilivuta hisia za abiria wengi waliokuwa kituoni hapo siku hiyo ya tukio

Watoa huduma katika hifadhi ya Serengeti

Miongoni mwa mamvo yanayoifanya hifadhi ya Serengeti, kuwa ya kwanza kuiwaza unapofikiri mahali pa kwenda kutalii, ni pamoja na watoa huduma mbalimbali, ambao wamesheheni vifaa na ukaribu wa kutosha.

Blogi hii, ilipata fursa ya kutembelea hifadhini humo hivi karibuni na kushuhudia baadhi ya wageni waliokuwa wametembelea mahali hapo wakiwa wanafurahia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za uhakika ambazo walizipata kutoka kwa makampuni ya usafiri yenye kutoa huduma za usafiri ndani ya hifadhi hiyo.


 Watoa huduma hususan za usafiri ndani ya hifadhi ni wenye magari ambayo yanakidhi mahitaji ya hali zote za hewa katika mwaka mzima, pamoja na hali ya barabara zote katika eneo la hifadhi

Miongoni mwa watia huduma za usafiri waliobobea katika shughuli hiyo, ni pamoja na kampuni ya Zara Tanzania Adventures, kama magari yao yanavyoonekana pichani. Ni yenye ubora wa hali ya juu



Wengine ni kampuni ya Altezsa, ambao nao wana magari ya uhakika miongoni mwayo yakiwa haya yenye kuonekana katika picha hizi hapa juu

Serengeti National Park, hifadhi yenye utajiri wa vivutio

Hifadhi ya Serengeti, ni miongoni mwa sehemu chache sana nchini, na pengine hata duniani, ambazo zimejaaliwa kuwa na karibu kila kitu anachoweza kuhitaji mwanadamu, ili kumfanya afurahie uwepo wake mahali hapo.

Hapa, ni mkusanyiko wa baadhi tu, ya vitu ambavyo kwa hakika vitakufanya usijutie uamuzi wako wa kutembelea hifadhi hii, iliyosheheni mambo mengi ya kujifunza.























Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad