Thursday, July 14, 2016
Serikali ya china kuwekeza katika mkoa wa simiyu
SERIKALI YA CHINA IMESEMA IKO TAYARI KUWEKEZA KATIKA MKOA WA SIMIYU KWA KUJENGA VIWANDA MBALIMBALI VIKIWEMO VYA NGUO NA MAZIWA NA NYAMA KUTOKANA NA MKOA HUO KUONYESHA KUWA NA RASILIMALI NYINGI KAMA MIFUGO NA PIA NDIO UNAONGOZA KWA KUZALISHA ZAO LA PAMBA NCHINI,
AKIONGEA NA
VIONGOZI MBALIMBALI WA MKOA WA SIMIYU KUPITIA KWA MKALIMANI WAKE,YE TIANFA BALOZI MDOGO WA CHINA NCHINI TANZANIA,ZHANG
BIAO,AMESEMA NCHI YAKE IKO TAYARI
KUWEKEZA KATIKA VIWANDA KATIKA MKOA WA SIMIYU ILI KUUSADIA MKOA HUO KUKUA KIUCHUMI IKIWA NI
PAMOJA NA KUWAPA AJIRA VIJANA WA MKOA WA
SIMIYU.
KWA UPANDE
WAKE MKUU WA MKOA WA SIMIYU ANTHONY MTAKA AMEMUHAKIKISHIA BALOZI HUYO KUWA MKOA
WA SIMIYU UKO TAYARI KUWAPOKEA WAWEKEZAJI KUTOKA NCHINI CHINA WATAKAOHITAJI KUWEKEZA KATIKA MKOA WA SIMIYU
NA PIA WATAHAKIKISHA WANAWAPA USHIRIKINO WA KUTOSHA NA ULINZI PIA,,
BAADHI YA
WADAU WA MAENDELEO WA MKOA WA SIMIYU WAMESEMA UJIO WA BALOZI HUYO NI FARAJA
KWAO KWANI HUENDA UKAFUNGUA MILANGO NA FURSA KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA
KIUCHUMI KATIKA MKOA HUU
BALOZI HUYO
AMETEMBELEA MKOA WA SIMIYU IKIWA NI MWALIKO
WA MKUU WA MKOA WA SIMIYU AMBAPO BAADA YA KUONDOKA MKOANI SIMIYU AMEELEKEA
MKOANI MWANZA,
mwisho
Tuesday, July 12, 2016
WANUNUZI WAPAMBA SIMIYU WAONYWA KUTOWEKA MAJI
BERENSICHINA,SIMIYU,JULAI
12,2016,
,wanunuzi wa
pamba wanaotia maji waonywa,
HABARI YA BIASHARA
SERIKALI MKOANI SIMIYU
HAITAPOKEA PAMBA ILIYOWEKEWA MAFUTA YA KENGE KWA MADAI YA KUONGEZA KILO
,PAMBA INAYOWEKEWA MCHANGA NA MAJI KWANI KUFANYA HIVYO KUNAPUNGUZA UBORA WA
PAMBA KATIKA SOKO LA DUNIA NA BADALA YAKE BEI KUENDELEA KUSHUKA NA HIVYO
WAKULIMA KUKATA TAMAA KULIMA ZAO HILO NA KUJIKITA KATIKA MAZAO YA CHOROKO NA
DENGU ..
AGIZO HILO LIMETOLEWA
NA MKUU WA MKOA WA SIMIYU ANTHONY MTAKA WAKATI WA MKUTANO BAINA YA WANUNUZI
WA PAMBA NA WENYEVITI WA HALMASHAURI ZA WILAYA KUELEKEA MSIMU WA
UNUNUZI WA ZAO LA PAMBA AMBAPO BAADHI YA MAKAMPUNI YAMEANZA KUNUNUA
,ILI KUJUA BEI ELEKEZI IWAPO INAZINGATIWA .
AMESEMA KUWA MKOA WA
SIMIYU UNAZALISHA ZAO LA PAMBA NCHINI KWA ASILIMIA 60 AMBAPO MWAKA JANA
ZILINUNULIWA KILO MILIONI 70 ZA PAMBA HIVYO KAMA MKOA HAWATAKUBALI KUONA ZAO
HILO LINATOWEKA KUTOKANA NA WATU WACHACHE KUJENGA MAZOEA YA KUIWEKEA
MAJI PAMBA,MAFUTA YA KENGE NA MAWE LAZIMA HATUA ZICHUKULIWE DHIDI YAO
KURUDISHA UBORA WA ZAO HILO KATIKA SOKO LA DUNIA.
AIDHA MKUU HUYO WA
MKOA AMETUMA SALAAM KWA WANUNUZI WA
ZAO HILO WANAOHARIBU MIZANI NA KUWAIBIA WAKULIMA NA KUWATAKA WAACHE MARA MOJA
KWA UPANDE WA WADAU WA
PAMBA WAMEYATAKA MAKAMPUNI YA UNUNUZI KULIPA USHURU WA AWALI KATIKA
HALMASHAURI HUSIKA KABLA YA KUANZA UNUNUZI.
MWISHO,
|
HIFADHI YA SERENGETI YAKANUSHA KUTOWAPIGA WAFUGAJI WALIOKAMATWA WAKIINGIZA MIFUGO HIFADHINI
BERENSICHINA,SERENGETI,JULAI
12,2016,.
,Hifadhi ya
Serengeti yakanusha kutowapiga wafugaji,
SIKU CHACHE
BAADA YA WAFUGAJI WILAYANI BARIADI MKOANI SIMIYU KUDAI KUPIGWA NA ASKARI WA
HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI WAKATI WA ZOEZI WA UKAMATAJI MIFUGO INAYOINGIA
HIFADHINI KINYUME CHA SHERIA,HIFADHI HIYO IMEKANUSHA TAARIFA HIZO NA KUSISITIZA
HAKUNA MFUGAJI ALIYEPIGWA NA KAMA YUPO AJITOKEZE HADHARANI,
AKIONGEA NA
WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE MKUU WA HIFADHI HIYO ,WILLIAM MWAKILEMA
AMESEMA HAKUNA MTU YEYOTE ALIYEPIGWA BALI KILICHOKAMATWA NI MIFUGO KUTOKANA NA
WAFUGAJI HAO KUBUNI MBINU MPYA YA KUINGIZA
MIFUGO USIKU NDANI YA HIFADHI KWA AJILI YA KUCHUNGA NA KWAMBA WAO WATAENDELEA
KUWAKAMATA WAFUGAJI HAO KWA SABABU WANAVUNJA SHERIA YA TANAPA,SURA NAMBA 282
KAMA ILIVYOFANYIWA MAREKEBISHO MWAKA 2002
KWA UPANDE
WAKE MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAFUGAJI KANDA YA ZIWA MLIDA MSHOTA AMBAYE
AMEONEKANA KUTOKUWA NA MSIMAMO KUHUSU SUALA HILO ALIPOHOJIWA NA ITV KUHUSIANA
NA MADAI HAYO YA WAFUGAJI AMEKIRI KUWA KUTOKANA NA UHABA WA MALISHO WAFUGAJI
HAO WAMEKUWA WAKIINGIZA MIFUGO HIFADHINI KWA AJILI YA KUCHUNGA KAMA
ANAVYOELEZA,.
BAADHI YA
VIJANA WALIOKUTWA NA CAMERA YA ITV NDANI YA HIFADHI HIYO WAMEKIRI KUTUMWA NA
WAZAZI WAO KUCHUNGIA NDANI YA HIFADHI NA KWAMBA WANAPOJARIBU KUKATAA HUPIGWA NA WAZAZI NA WALIOAJILIWA KUCHUNGA
MIFUGO HUTISHIWA KUFUKUZWA KAZI,
HIVI
KARIBUNI MAKAMU WA RAIS SAMIA SURUHU ALIWAAGIZA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA
KUHAKIKISHA WANAONDOA MABOMA YOTE YA WAFUGAJI YALIYOKARIBU NA HIFADHI ZA TAIFA
HAPA NCHINI.
Mwisho
Habari za siku nyingi wapendwa wa blog hii ni matumaini yangu kuwa hamjambo wote na mnaendelea vizuri na shughuli za kila siku,nipende kuchukuwa fursa hii kuwaomba radhi kuwa sikuwa hewani kwa muda mrefu na hii ni kutokana na kutingwa na majukumu ya kazi,lakini niwataarifu kuwa kuanzia leo niko tayari kabisa kuwaletea habari mbalimbali za mkoa wa simiyu na maeneo mengine kwa lengo la kuwahabarisha kinachojili ni matumaini yangu kuwa tutakuwa wote katika kupata kila matukio na habari motomoto za kila siku za ukweli na uhakika na siyo za kupika,
Niwatakie kila laheri katika shuguli zenu,
wasalaam
Berensichina,Alikadi,mkurugenzi wa Habari motomoto
Niwatakie kila laheri katika shuguli zenu,
wasalaam
Berensichina,Alikadi,mkurugenzi wa Habari motomoto
Subscribe to:
Posts (Atom)
Comments System
disqus
Disqus Shortname
msora
Popular Posts
-
SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – (Sehemu...
-
Huha Makuja Nyungi (kushoto), akiwa anaelekea mahakamani muda mfupi kabla ya kusomewa hukumu hiyo. Kulia ni mtuhumiwa mwingine katika ke...
-
Mwezeshaji wa mada ya kwanza kuhusu umuhimu wa TIKA, ndugu Derick Ndetabula akitoa mada kwa washirik.
Header Ads
