Safari ya kuelekea Bulyanhuru kwa ajili ya kutembelea mgodi ilianzia Mwanza saa 1:00. Fuatana nami katika picha hizi ili ujunze mambo kadhaa katika migodi ya Tanzania inayomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold.
Moja ya miradi inayofadhiliwa na mgodi wa Turawaka Wilayani Biharamulo.
Haya ni baadhi ya mashimo inakochimbwa dhahabu chini ya ardhi katika mgodi wa Turawaka.
Hawa ni wachimbaji wa Kitanzania maalufu kama Intruders wakiokota mawe ya mabaki ya dhahabu katika pembezoni mwa mgodi wa North Mara ulioko Tarime.
Magari ya mgodi wa North Mara (Tarime) yanayotumiwa na walinzi yakiwa yamepigwa mawe na wamachinga wa dhahabu.
Mojawapo ya mashine kubwa inayotumika kubeba mchanga wa dhahabu kutoka shimoni na kupeleka eneo la kusafishia.
Hii ndio sehemu ambayo dhahabu husafishwa na kupakiwa kwa ajili ya kupelekwa kwa wanaojua matumizi yake
Haya ndio maji yanayosadikiwa kuwa na sumu ambayo awali yalikuwa yanatiririka kuelekea mto Tigite huko Tarime
Wednesday, November 10, 2010
NANI KAWATUMA GREEN-GUARD KUVAA MIKANDA YA JESHI?
HOJA YANGU
NANI KAWATUMA GREEN-GUARD KUVAA MIKANDA YA JESHI?
NA Berensi Alikadi-Bunda
Niliwahi kuandika makala katika gazeti hili kuhusu hatari ya raia kuvaa nguo zinazofanana na sare za jeshi, makala ambayo naamini ilileta mabadiriko makubwa maana niliona baada ya makala hiyo kutoka watu wengi wakikamatwa waliokuwa wamevaa nguo hizo.
Pengine unaweza kujiuliza ni kwanini niliandika makala hiyo, niliamua kuandika makala hiyo baada ya kuona vitendo vingi vya ujambazi vimekithili na wale waliuokuwa wakikamatwa walikuwa wakikutwa na nguo za jeshi hali ambayo ililivunjia sana heshima ya jeshi letu la wananchi.
Wapo wengi waliojenga dhana kuwa huenda vitendo hivyo vilikuwa vikifanywa na askari wetu wa jeshi la wananchi, lakini kumbe ni kundi la watu wachache ambao walikuwa wakitumia nguo hizo kwa kufanyia uharifu.
Leo tena sitaki kuzungumzia tena suala la nguo hizo nina imani kuwa wahusika walisikia ujumbe huo na waliwashughulikia wananchi waliokuwa wanavaa mavazi hayo na kwa vile sheria ipo na amini kuwa jambo hilo halitarudia tena.
Katika makala hii leo nataka kuzungumzia suala la hawa askari wa chama cha mapinduzi maarufu kama Green Guad ambao wanavaa mikanda ya jeshi la wananchi na viatu maarufu kama buti.
Nimekuwa nikijiuliza sana kwa muda mrefu kuhusu uvaaji huu wa hawa vijana ambao wanajiita askari wa chama kwa kuruhusiwa kuvaa mavazi haya ya kijeshi huku serikali ikiwaangalia.
Green Guad hawa wamekuwa wakivaa mikanda hii katika matukio tofauti hasa kunapokuwepo na sherehe mbalimbali za kichama na pengine mara nyingi katika ziara za viongozi wakubwa mfano rais, waziri mkuu na viongozi wa juu wa chama cha mapinduzi.
Kinachonishangaza ni kwamba katika hafla hizo huwa wapo viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo wakuu wa majeshi na wa polisi ambao wanajua kuwa ni makosa kwa mtu asiye askari kuvaa sare yeyote ya kijeshi na hilo ni kosa la jinai lakini hawawachukulii hatua yeyote.
Katikasiku za hivi karibuni green guad hawa wamekuwa wakitumia mikanda hiyo kwa kupigia wananchi na kuwaumiza na hata wananchi wakienda kushitaki polisi huwa hawachukuliwi hatua.
Hivi karibuni katika mkutano mmoja wa kampeni katika jimbo la Sumve mwandishi mmoja wa habari wa gazeti la mwananchi alipigwa na green guad hawa kwa baada ya kupewa amri na mmoja wa viongozi wa chama hicho sijui kesi hii kama imeenda polisi na ni hatua gani waliyochukuliwa.
Pengine watanzania wanataka kufahamu kama hilo nao ni jeshi na kama ni jeshi liko katika ibara gani ya katiba ya Tanzania na kama siyo jeshi kwanini liruhusiewe kuvaa mikanda ya jeshi hivi wanajeshi wetu leo wamekwenda likizo?
Wakati leo hawa wanaruhusiwa kuvaa mikanda ya jeshi wapo baadhi ya askari wanavaa viatu vikiwa vimeshonwa viraka na hata wengeine wanavaa mikanda ikiwa imechanika, lakini hawa green guad leo wanamikanda mipya buti mpya sasa sijui nani kati ya hawa anastahili kuvaa sare hizo.
Mimi leo nataka wanajeshi wanijibu na wawajibu watanzania kuwa tangia lini wameanza kuvaliana nguo na green guad au ni kwa vile wao wako chama twawala hivi kweli chama kama CUF au Chadema leo vijana wake wangevaa mikanda ya jeshi sijui kama wangekuwa na hali gani
Jeshi la wananchi linapaswa kuwaeleza wananchi kuhusu uharali wa vijana hawa wa chama cha mapinduzi kuvaa sare hizi na nani iliwapa mikanda hiyo na hivyo viatu, na pia liwaambie wananchi kuwa limeanza kugawa sare zake ovyo.
Lakini pia mkuu wa majeshi atauambie kuwa green guad ni jeshi la nani na linawajibika kwa nani na linalipwa mshahara na nani na kama siyo jeshi kiharali nani analiruhusu kuvaa mikanda hiyo.
Kama jeshi letu haliwezi kuwanyang’anya vijana hawa mikanda hii basi tufahamu kuwa wao ndio wanawasapoti na kuwapa mikanda na viatu hivyo ambavyo ndivyo wanatumia katika kuwapigia wananchi hasa katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi.
Tanzania ni nchi yenye amani na inatawaliwa kwa majeshi yalikatika katiba ya jamhuri hatutaki kuona kundi la chama Fulani linajifanya kuwa na jeshi ambalo linawatisha wananchi kwa kuvaa mikanda ambayo inanuliwa kwa kodi yetu ni vema jeshi letu lifahamu hivyo na liwanyanga’nye hawa green Guad.mikanda na hizo buti.
MWALIMU NYERERE NURU YA WANYONGE ILIYOZIMIKA
MWALIMU NYERERE NURU YA WANYONGE ILIYOZIMIKA
NA Berensi Alikadi-Bunda BABA wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa Aprili 1922, katika eneo la Mwitongo, Muhunda kijijini Butiama. Baba yake, Nyerere Burito, alikuwa Chifu wa kabila dogo la Wazanaki, na alifariki dunia mwaka 1942 na kuzikwa hapo hapo kijijini Butiama. Inakisiwa kwamba, mnamo mwaka 1800, kulikuwa na kaya 80 tu za Wazanaki; mama yake aliitwa Mgaya Nyang’ombe, alifariki dunia mwaka 1997. Kama ilivyokuwa kwa watoto wengine, Kambarage alikuwa katika maisha ya dhiki, ingawa alikuwa mtoto wa chifu, alifanya kazi ya uchungaji wa mifugo na mara kadhaa alimsaidia mama yake kazi za kilimo. Mwalimu Nyerere alianza kusoma akiwa na umnri wa miaka 12, katika Shule ya Msingi Mwisenge iliyopo Musoma mjini, ingawa kuna habari kwamba Chifu Nyerere hakutaka Kambarage asome. Lakini baadaye, ilikuja kubainika kuwa mzee huyo ndiye aliyeacha wosia kwa Wanzagi Nyerere (kaka yake Mwalimu), akimtaka ahakikishe kwamba Kambarage anasoma kwa bidii. Wanafamilia wanasema kwamba, Chifu Nyerere alitoa wosia huo siku chache tu kabla ya kifo chake. Naye Wanzagi, ambaye baada ya kifo cha baba yake aliteuliwa kuwa chifu, alitekeleza wosia wa baba yake huyo. Chifu alitoa msaada kwa Kambarage, uliomwezesha kusoma na hatimaye kupata mafanikio makubwa. Baada ya kutoka Mwisenge, alichaguliwa kwenda kupata masomo ya sekondari mkoani Tabora, katika shule iliyokuwa ya watoto wa machifu. Hapo Tabora alifanya vizuri na kuchaguliwa kujiunga na masomo ya juu, katika Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda. Kutoka huko, alirejea Tabora kufundisha katika Shule ya St. Mary. Mwaka 1949 alijiunga na Chuo Kikuu cha Edinburgh, Scotland, akisomea shahada ya uzamili (MA) katika masuala ya historia na uchumi, aliyohitimu mwaka 1952. Baada ya kutoka huko, alikwenda kufundisha tena katika Shule ya Mtakatifu Francis, Pugu, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Akiwa Pugu, alianza kujihusisha kwa bidii zaidi katika masuala ya siasa, wakati mwingine alisema, alipenda sana kuwa daktari wa binadamu, lakini baadaye aliona bora awe mwalimu, ili awatoe wengi gizani. Baada ya kufanya kazi ya kufundisha kwa miaka kadhaa, aliona ajiingize moja kwa moja kwenye siasa, ili aendeshe mapambano ya kuwaondoa wakoloni, kwa msingi huo, akiwa mwalimu katika Shule ya Mtakatifu Francis, mwaka 1953 aliweza kuwa mwanachama wa chama kilichokuwa kikiitwa TAA, yaani Tanganyika African Association. Hata hivyo, awali chama hicho hakikujitambulisha moja kwa moja kisiasa kwa wananchi na serikali ya kikoloni. Mwalimu Nyerere alikuwa mwenyekiti wa chama hicho. Mwaka mmoja baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TAA, ilipofika Julai 7, 1954, chama hicho kilibadilisha jina na kuitwa Tanganyika African National Union (TANU), na Mwalimu Nyerere akawa rais wake wa kwanza. Malengo ya chama hicho, kama yalivyotangazwa na Mwalimu Nyerere, yalikuwa kuifanya Tanganyika iwe nchi huru. Pia Mwalimu akiwa na TANU alihakikisha kwamba chama hicho kinajitahidi kujenga nchi isiyokuwa na ukabila wala ubaguzi wa aina yoyote ile. Mnamo mwaka 1955, Mwalimu Nyerere alipata wakati mgumu kutoka kwa serikali ya kikoloni, kwa kuwa wakati huo wafanyakazi wa serikali hawakuruhusiwa hata kidogo kujihusisha na masuala ya siasa, hivyo alitakiwa achague moja, kati ya siasa na ualimu. Yeye akaamua kuchagua siasa, na huo ukawa ndio mwisho wake wa kuajiriwa serikalini kama mwalimu. Lakini akabaki na jina lake la Mwalimu hata leo. Julai 1957, Mwalimu Nyerere aliteuliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria (LEGCO), lakini alijiuzulu nafasi hiyo Desemba mwaka huo huo. Hata hivyo, ikumbukwe kwamba, Mwalimu alipata kuhutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, akiwa katika juhudi za kutaka Tanganyika iwe huru kutoka katika makucha ya ukoloni wa Kiingereza. Mwaka 1958, alipinga vikali mpango wa serikali ya kikoloni, wa kufanya uchaguzi wa wajumbe wa LEGCO. Alipinga mpango wa wakoloni kutoa theluthi mbili ya viti vyote kwa Wazungu na Waasia. Mabadiliko yalipofanywa, TANU ilipata kura nyingi na Mwalimu Nyerere akawa mmoja wa wajumbe wa baraza hilo. Hali kama hiyo ilijitokeza tena katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1960, aliposhinda na kutangazwa kuwa Waziri Mkuu. Mei Mosi 1960, aliapishwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika, chini ya Serikali ya Madaraka, na Desemba 9, 1961, nchi ilipata uhuru, mwenyewe akaendelea kuwa Waziri Mkuu. Miezi sita baadaye, alijiuzulu nafasi hiyo, kwa maelezo kwamba alitaka kwenda kuiimarisha TANU, na nafasi yake ikachukuliwa na Rashid Mfaume Kawawa. Mwaka 1962 Mwalimu Nyerere aliteuliwa na TANU kuwa mgombea urais. Katika uchaguzi huo, Mwalimu alipata asilimia 97 ya kura zote. Desemba 9, aliapishwa kuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika, Ikulu ikawa makazi yake rasmi kama rais wa nchi. Jitihada za Mwalimu Nyerere hazikuishia kwenye uhuru wa Tanganyika tu, bali mwaka 1964 alifanya kazi kubwa ya kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar, akishirikiana na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, ambaye pia alijua umuhimu wa kuwapo Muungano. Ndipo ikazaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Aprili 26, 1964. Hata hivyo, mwaka huo huo, yalitokea maasi ya baadhi ya askari wa jeshi lililorithiwa kutoka kwa wakoloni. Jeshi hilo lilivunjwa na kuundwa jeshi jipya – Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Mwalimu Nyerere mwenyewe akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza. Wimbi la mabadiliko chini ya uongozi wake liliendelea kujitokeza. Mwaka 1967 alitangaza Azimio la Arusha. Kutokana na azimio hilo, mali nyingi zilitaifishwa, baadhi zikiwa ni majumba, mashamba, viwanda, kampuni binafsi na kuhakikisha kwamba njia kuu za uchumi zinamilikiwa na umma. Azimio hilo ndilo lililotoa mwelekeo wa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ndoto kubwa kabisa ya Mwalimu. Aliamini sana katika ujamaa na kujitegemea, na kwamba siasa hiyo isingefanikiwa kama watu wangeendelea kuishi mbalimbali. Mwaka 1970 Tanzania ilikumbwa na tatizo kubwa la njaa. Kukawa na kupanda kwa bei ya mafuta na bidhaa nyingine nyingi, hali iliyouweka uchumi wa Tanzania katika hali mbaya. Ilitangazwa vita dhidi ya tatizo hilo. Ilikuja kutokezea kwamba, baadhi ya watu walijilimbikizia mali nyingi kinyume cha matakwa ya Mwalimu na sera za nchi, ikaanzishwa operesheni dhidi ya wahujumu uchumi. Kiongozi wa mapambano hayo, alikuwa Waziri Mkuu wa wakati huo, hayati Edward Moringe Sokoine, kipenzi cha Mwalimu na Watanzania wote. Kwa msingi huo, mwaka 1974 alitangaza Operesheni ya Vijiji vya Ujamaa. Watu walihamia kwenye vijiji vipya vya ujamaa kwa hiari yao, lakini waliopinga walihamishwa kwa nguvu. Kulikuwapo malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu utekelezwaji wa mpango huo, licha ya nia yake nzuri. Kufikia mwaka 1977, karibu asilimia 80 ya Watanzania wote walikuwa wakiishi katika vijiji vya ujamaa, huku wakiwa wameboreshewa huduma muhimu kama elimu, maji na afya – huduma za jamii, ingawa hapakuwapo mabadiliko makubwa sana kama yalivyokuwa matarajio yake. Mwaka 1977 pia, Mwalimu Nyerere alitimiza ndoto yake ya kuviunganisha vyama vya TANU na Afro Shirazi Party (ASP). Hiyo ilikuwa Februari 5, 1977. Vyama hivyo viliungana na kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mwalimu alitangaza vita dhidi ya nduli Idi Amin Dada wa Uganda mwaka 1978, aliyekuwa amevamia na kuchukua kipande cha Tanzania, akidai ni chake. Mwaka 1979 ulishuhudia majeshi ya Uganda yakiwa yameshindwa vibaya katika vita hiyo, nduli mwenyewe akang’olewa na Uganda mpya ikaanza kujengwa. Baada ya kuongoza kwa miaka mingi, hatimaye Mwalimu Nyerere alitangaza rasmi kustaafu urais, na alitimiza ahadi hiyo mwaka 1985, akimwachia jahazi mteule wake, Ali Hassan Mwinyi. Bado Tanzania iliweza kujivunia rekodi nzuri ya kutokomeza ujinga. Hadi Mwalimu Nyerere anang’atuka mwaka 1985, zaidi ya asilimia 90 ya Watanzania walikuwa wanajua kusoma na kuandika. Licha ya kustaafu urais, aliendelea na uenyekiti wa CCM hadi alipoamua pia kujing’atua, mwaka 1990 na kumkabidhi Mwinyi. Hata hivyo, aliendelea kuwa kinara wa siasa za ndani na nje ya nchi, akipata sifa kubwa kimataifa. Aliendelea na uenyekiti wa nchi za kusini hadi mauti yalipomfika. Mwalimu alikuwa mstari wa mbele kupinga mfumo mbaya wa uchumi kati ya nchi tajiri na maskini, alilalamikia pia fursa finyu na madeni makubwa kwa nchi maskini kama Tanzania. Alipigania madeni hayo yafutwe, ili fedha hizo zitumike kuandaa na kuendeleza huduma za jamii kwa mamilioni ya watu katika nchi maskini. Hadi anafariki dunia, Oktoba 14, 1999, Mwalimu Nyerere alikuwa msuluhishi wa kimataifa wa mgogoro wa Burundi na Rwanda, nafasi iliyochukuliwa baadaye na swahiba wake, Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Mwalimu leo anakumbukwa na mataifa mengi ya Afrika, kwa msimamo wake wa kupinga ubeberu, ukoloni na uonevu wa aina zote. Kwa miaka mingi, alikuwa Mwenyekiti wa Nchi Zilizo Mstari wa Mbele Katika Ukombozi Kusini mwa Afrika. Aliifanya Dar es Salaam kuwa makao makuu ya harakati hizo. Wapigania uhuru kutoka Afrika Kusini, Angola, Msumbiji, Namibia, Zimbabwe na kwingineko, waliishi Tanzania na kupewa mbinu za kuondoa tawala dhalimu nchini mwao. Mwalimu alikuwa anasema kwamba, hakuna maana kwa Tanzania kuwa huru, bila Afrika yote kujikomboa. Alisimamia, hadi wote wakakombolewa kwenye ukoloni na ubaguzi wa rangi. Makamanda na wapiganaji wa Tanzania walikwenda kushiriki katika mapigano ya kivita kwenye nchi hizo washirika, ili kuzipatia uhuru. Ni Mwalimu, ni mtoto wa chifu, ni rais, ni mwenyekiti, lakini aliishi kimaskini, maisha ya kawaida, ya kujitolea, ya kujali wengine zaidi, ya kutoa kuliko kupokea. Hakika anastahili kuitwa mwana wa kweli wa Afrika. Tunapokumbuka leo kifo chake, hatuna budi kuyaenzi aliyotenda. Mwalimu alichukua tabia ya watu kujirimbikizia mali kama ilivyo hivi sasa alikemea tabia ya viongozi wala rushwa, alikemea tabia ya viongozi walioendekeza udini na ukabila,mambo ambayo leo hii watanzania tunashuhudia hasa kuelekea uchaguzi mkuu. Wakati wa mazishi ya mwalimu wapo baadhi ya viongozi walioapa kulinda rasilimali zetu lakini wao leo ndio warafi wakubwa na ndio wanaotafuna mali za walipa kodi. Mwalimu aliona mbali na ndio maana hata alikataa madini yetu yasichimbwe leo hii nchi inaongozwa na viongozi wenye tamaa ambao wamekuwa wakihubiri uongo kuwa wanamuenzi mwalimu kwa maneno wakati wanaihujumu nchi yetu. Akiwa mtanzania mwenye uchungu na nchi yake aliona uchungu na ndipo alipoamua kuwa machimbo yetu yaachwe kwanza lakini leo tumeshuhudia migodi inavyotafunwa na wawekezaji wanatupa fadhila ya herikopta za kufanyia kampeni. Keki ya taifa inaliwa na wachache. Leo hii ukifika butiama hutaamini kama kweli ndipo alipozaliwa muasisi wa taifa hili, serikali yetu imetekeza hata nyumba ya kwanza ya mwalimu aliyojenga alipotoka Tabora, hali ya maisha ya familia ya mwalimu inatisha lakini leo viongozi wanandai wanamuenzi mwalimu hivi kweli watanzania ni wepesi wa kusahau mema yote ya mwalimu kiasi hicho. Wakati leo tunatimiza miaka 11 ya kifo chake watanzania lazima tujiulize mengi aliyotuachia mwalimu ambayo leo tunaona jinsi viongozi walioachiwa walivyoshindwa kuyatekeleza, na leo tena wanaomba ridhaa ya kuchaguliwa. Hakika mwalimu alikuwa nuru ya wanyonge na mpenda haki hakuna kiongozi atakayeweza kumfikia mwalimu kwa busara zake na maono yake, watanzania leo tumeachwa gizani hatujui tufanyeje. Kwakweli kifo chake kiliacha masikitiko makubwa kwa Watanzania, Waafrika na hata nje ya bara letu hili, kikiwaacha wanyonge, kwa kuondokewa na mtu waliyempenda mno, aliyewajali na kuwasaidia kuifanya dunia kuwa mahali pazuri zaidi pa kuishi. Apumzike kwa amani. Amina. |
MKUU WA GEREZA AACHIWA HURU
MKUU WA GEREZA AACHIWA HURU
NA Berensi Alikadi -Bunda
MAHAKAMA ya wilaya ya Bunda jana ilimuachia huru mkuu wa gereza la Matongo wilayani Bariadi mkoani Shinyanga,Maiko Maziku baada ya upande wa mashitaka kushindwa kutoa ushahidi wa kujitosheleza.
Hakimu mfawidhi mwandamizi wa mahakama ya wilaya hiyo Joacimu Tiganga alisema kuwa mshitakiwa huyo alikuwa miongoni mwa washitakiwa sita ambao walikamatwa tarehe 2/12/2009katika mbuga ya mihama iliyopo ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti ambapo walikuwa wanakabiliwa na makosa sita ya kesi ya uhujumu uchumi.
Aliyataja makosa hayo kuwa ni kula njama kwa nia ya makosa,kukutwa na nyara za serikali, kuwinda ndani ya hifadhi kwa kutumia silaha zilizokatazwa,kuingia hifadhini bila kibali, kujwindas wanyama waliokatazwa na kukutwa na silaha hifadhini bila kibali.
Hakimu alidai kuwa miongoni mwa walikamatwa alikuwemo askari wake mmoja na kwamba yeye alikamtwa kwa kile kilichodaiwa kuwa huenda yeye ndiye aliyempa ruhusa na sailaha ya kwenda kuwindia.
Alifafanua kuwa baada ya upande wa mashitaka kufunga ushahidi wake mahakama ilipitia ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na kuona kuwa wakati tukio hilo linatendeka mkuu huyo wa gereza hakuwepo na kwamba walalamikaji wameshindwa kuonyesha kama kweli mkuu huyo ndiye aliyemtuma na kumpa silaha hivyo mshitakiwa hakuwa na kesi ya kujibu.
Kufutia hali hiyo mahakama ilimuachia huru mshitakiwa huyo ambapo wenzake wanaendelea na kesi hiyo ambayo itaanza kusikilizwa tarehe 12/12/ mwaka huu.ambapo washitakiwa wengine wako nje kwa dhamana.
Kesi hiyo ilikuwa inaongoza na mawakili wa serikali,Pius Hilla toka ofisi ya mwanasheria wa serikali Mwanza na Meredi Rweyemamu toka Dare-salaam wakisaidiana na mawakili Prochas Longomba toka kikosi cha kuzuia ujangili na Elias Benjamini,na Maiko Laizer toka Tanapa.
Kwa upande wake mkuu huyo alikuwa akitetewa na mawakili, Hezron Foka na Kweka ambao ni mawakili wa kujitegemea toka jijini Mwanza.
MWENDESHA BAISKELI AFA KWA KUGONWA NA GARI
MWENDESHA BAISKELI AFA KWA KUGONGWA NA GARI
NA Berensi Alikadi-Bunda.MTU mmoja amekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari dogo aina ya Noah lililokuwa likitoka mwanza kwenda mkoani Mara likisisafilisha maiti.
Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imetokea juzi majira ya saa sita mchanakatika kijiji cha Kunzugu nje kidogo mji wa Bunda na kulihusha gari hilo lenye namba za usajili T276BDF ambalo limugonga mwendesha baiskeli aliyefahamika kwa jina la Nchambi Doto 19 mkazi wa kijiji hicho cha kunzugu.
Imeelezwa ,kuwa gari hilo ambalo lilikuwa limebeba maiti toka jijini Mwanza na kuelekea Majita wilaya ya Musoma Vijijini lilipofika eneo hilo lilitaka kulipita gari jingine aina ya Toyota Land Cruser huku likiwa mwendo kasi na kumbe kwa mble yake alikuwepo mwendesha baiskeli huyo ndipo lilipomgonga na kufa papo hapo.
Kwa mjibu wa watu walioshuhudia ajali hiyo walisema kuwa gari hilo lilimgonga vibaya na kwamba alivuja damu nyingi kabla ya kifo chake kutokanana mwendo mkali lililokuwa nao licha ya kwamba lilikuwa limebeba maiti.
Akizungumza na gazeti hili baba mdogo wa Marehemu aitwaye Alphonce Migato alisema kuwa maiti ya ndugu yao huyo imehifadhiwa katika hosptali ya DDH Bunda ikisubili taraibu za mazishi zikiandaliwa.
Hata hivyo dereva wa gari hilo alifanikiwa kutoroka baada ya ajali hiyo ambapo gari hilo linashikiliwa katika kituo cha polisi Bunda na ndugu wa marehemu aliyekuwa akisafilishwa kwenda Musoma walitafuta gari jingine na kuweka maiti hiyo na kuendelea na safari.
Hiyo ni ajali ya pili kwa muda wiki moja kwa magari aina yaNoah kugonga na kuuwa ambapo wiki iliyopita mtu mmoja Makaba Lukas mkaziwa mtaa wa Manyamanyama kugongwa na gari aina ya Noah katika eneo la Manyamanyama,gari hilo lilikuwa litoka Musoma kwendawilayani Bunda
Wakati huo huo mtu mmoja aitwaye Mwita Marwa Machugu32 mkazi wa mtaa wa Nyamakokoto juzi alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Bunda akituhumiwa na shitaka la kumbaka Binti mdogo mwenye umri wa miaka 13 jina linahifdhiwa.
Mbele ya hakimu James Manota ilidaiwa na mwendesha mashitaka wa polisi Hamza Mdogwa kuwa mnamo November 3 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili jioni huko katika mtaa wa Nyamakokoto mshitakiwa alimbaka mtoto huyo nyumbani kwake.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa siku ya tukio mshitakiwa huyo alimuta binti huyo nyumbani kwake na kuanza kumpa pombe ya Gongo na kwamba alipoona amelewa alimvutia chumbani kwake na kuanza kumbaka, hata hivyo baada ya kumaliza kumbaka alimuacha akaenda kwao baada ya kupata fahamu ndipo alipotoa taarifa kwa wakubwa wake ambao pia walitoa taarifa polisi.
Mshitakiwa huyo alikana shitaka hilo na kupelekwa rumande hadi 22Nov mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena
KANISA LAMKANA MWALIMU ALIYEDAIWA KUBAKA MWANAFUNZI
NA Berensi Alikadi -Bunda.KANISA la Angilikana wilayani Bunda limemkana mwalimu mmoja aliyekuwa akifundisha shule mmoja wa awali ya Compassion alishitakiwa kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake.
Akizungumza na Gazeti hili juzi ofsini kwake mkurugenzi wa huduma kituo cha huduma ya mtoto (TZ344) Ngai Emanuel alisema kuwa malimu huyo Amosi Julius ambaye hivi karibuni alifikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo kwa shitaka la kubaka mwanafunzi siyo mwalimu wa kituo chao bali ni mwalimu wa shule ya awali ya kanisa la moja la warokole lilliloko mtaa wa Chiringe.
Alisema kuwa kitendo cha mwalimu huyo kudai mahakamani hapo kuwa ni mwalimu wa shule ya Compassion inayomilkiwa na kanisa hilo siyo ya kweli na kwamba hata wao kama kanisa wameshangaa sana kusikia taarifa hizo kwenye vyombo vya habari kuwa mwalimu huyo alidai kuwa yeye ni mwalimu wa shule ya kanisa hilo.
''Mimi nataka nikwambie mwandishi shirika hili la Compassion linafadhili makanisa mengi na wala siyo Angilikana pekee hivyo mimi nakuhakikishia kuwa mwalimu huyo sio wetu bali anafundisha katika shule ya kanisa la hapo chiringe hivyo sisi hatuhusiki kabisa na mwalimu huyo'' alisema mkurugenzi huyo kwa msisitizo.
Naye katibu wa jimbo hilo mkoani Mara Francis Senda alisema kuwa kitendo cha mwalimu huyo kusema uongo mahakamani si cha kiungwana na kwamba hata wao wanatarajia kumfungulia mashitaka mengine ya kulichafua kanisa hilo kwa kulisingizia uongo, ambapo pia aliwatahadhalisha wananchi kuhusu mwalimu huyo.
Mnamo october22 mwaka huu mwalimu huyo alifikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo na kusomewa shitaka la kubaka mwanafunzi wa miaka 9 na mwendesha mashitaka wa polisi Hamza mdogwa, ambapo alikana kosa lake na kuomba dhamana alipoulizwa na hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya hiyo Joacimu Tiganga kuhusu kazi anayofanya ndipo alijibukuwa yeye ni mwalimu wa shule ya awali ya Compassion inayomilikiwa na kanisa Angilikana la mjini Bunda.jambo ambalo ni la uongo.
Hata hivyo mshitakiwa huyo hakupatikana tena kuhusu kutoa ufafanuzi wa kauli yake kutokana na kuwa yuko gerezani .
MWISHO
Subscribe to:
Posts (Atom)
Comments System
disqus
Disqus Shortname
msora
Popular Posts
-
SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – (Sehemu...
-
Huha Makuja Nyungi (kushoto), akiwa anaelekea mahakamani muda mfupi kabla ya kusomewa hukumu hiyo. Kulia ni mtuhumiwa mwingine katika ke...
-
Mwezeshaji wa mada ya kwanza kuhusu umuhimu wa TIKA, ndugu Derick Ndetabula akitoa mada kwa washirik.
Header Ads
