Friday, August 31, 2012

Kibonzo cha leo

LOS CONSEJOS DE BENITUS
 Mbwa akiwa amejilaza huku akiwa amevaa miwani.picha kwa hisani ya mitandao ya kijamii



Viongozi wa LHRC wakiwa na wanaharakati mjini Shinyanga

 Viongozi wa kituo cha sheria na haki za binadamu ,Katikati  Kutoka kushoto Leticia Petro na Rose Mwalongo wakiwa katika picha ya pamoja  na wanaharakati  wakati wa mkutano wa waangalizi wa haki za binadamu uliofanyika katika hotel ya Karena mjini Shinyanga.-picha na Berensi Alikadi

Wanaharakati wa haki za binadamu wakiwa pichani mjini Shinyanga

 Hawa ni baadhi ya wanaharakati wa haki za binadamu ambao walishiriki katika mkutano wa waangalizi wa haki za binadamu ulioandaliwa na kituo cha sheria na haki za binadamu ,mkutano uliofanyika katika hotel ya Karena iliyoko mjini Shinyanga .picha na Belensi China

Wageni kutoka Canada waliotembelea kituo cha kuwajengea uwezo kuhusu haki za binadamu kilichoko wilayani Bunda

 Hawa ni wageni kutoka Canada ambao wanafanya kazi za asasi za watetezi wa haki za binadamu walipotembelea ofisi yetu  iliyoko wilyani Bunda  mkoani Mara -picha na Berensi Alikadi.A

Wakimbiza Mwenge Kiwilaya Bunda mwaka 2012 pichani

 Hawa ni vijana wanne waliokuwa wakikimbiza mwenge Kiwilaya ,wilayani Bunda  wakiwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bunda Muda mchache kabla ya kushiriki mbio hizo -picha na Berensi Alikadi.

Waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mafunzo ya siku nne juu yaliyokuwa yakihusu online journalism

Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mara wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mafunzo ya siku nne ya online jourlism yaliyokuwa yakifanyika katika ukumbi wa hotel ya Orange Tree mjini Musoma -picha na Berensi Alikadi

Polisi Morogoro wakiwa katika doria siku ya mkutano wa Chadema








Polisi Mkoani Morogoro wakiwa katika doria siku ya mkutano wa Chadema
picha kwa idhini ya Kapipi Blogy.com

Mbuyu Twite usipime Dar


na Dina Ismail

Aidha, fulana zenye rangi ya kijani na njano zilizoandikwa jina la Twite, ziliuzwa kwa wingi uwanjani hapo kwa kati ya sh 10,000 hadi 15,000.
HATIMAYE mzizi wa fitina umekatwa, beki wa kimataifa wa Yanga, Mbuyu Twite ametua rasmi nchini na kupokewa kwa kishindo na shangwe za aina yake, hivyo kuhitimisha filamu ya ujio wake.
Twite ambaye usajili wake umezua gumzo kutokana na kujisajili pia kwa mahasimu wao wa jadi nchini, Simba, alitua Uwanja wa kimataifa wa JK Nyerere majira ya saa 10 alasiri na ndege ya Rwanda Air, akitokea mjini Kigali.
Hata hivyo, Simba ambayo ilidai ingemkamata nyota huyo baada tu ya kutua nchini kwamba ina taarifa ya kumsaka nyota huyo (RB), aliyekuwa akikipiga APR ya Rwanda kwa mkopo akitokea FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ilishindwa kufanya hivyo.
Simba ilitangaza kumkamata Twite kwa madai ya kuwatapeli dola 30,000 za Marekani ilizompa kama dau la usajili, kabla ya Yanga kumuongeza dau la dola 50,000 na hatimaye kufanikiwa kunasa saini yake.
Mara baada ya kutokeza katika lango la watu mashuhuri uwanjani hapo, Twite alivalishwa jezi namba 4 ya Yanga, ambayo nyuma iliandikwa jina la Mwenyekiti wa Simba, Rage (Alhaj Ismail Aden Rage).
Akizungumza uwanjani hapo, Twite alisema amekuja Tanzania kwa ajili ya kuitumikia Yanga na si kingine, hivyo mashabiki wasubiri mambo mazuri kutoka kwake.
Hata hivyo, Twite aligoma kuzungumzia hatua yake ya kusaini Simba na baadaye Yanga kwa madai kwamba ni habari ndefu na watu wanazungumza sana, hivyo ni kulipotezea tu.
“Siwezi kulizungumzia suala hilo (kusaini Simba), kwani maneno mengi yanasema na yataendelea kusemwa,” alisema Twite.
Katika mapokezi hayo, umati mkubwa wa mashabiki wa Yanga, ulifurika uwanjani hapo kwa lengo la kumlaki nyota huyo ambako walikuwa wakifurahi kwa kuimba kucheza na kupiga matarumbeta.
Kama hiyo haitoshi, mashabiki hao ambao wakiwa wamevalia jezi zilizoandikwa ‘Twite,’ walionesha mapenzi yao kwa mchezaji huyo, baada ya kumbeba kwa mita kadhaa baada ya kutoka nje ya uwanja kabla ya kumuacha na kupanda gari la klabu.
Aidha, fulana zenye rangi ya kijani na njano zilizoandikwa jina la Twite, ziliuzwa kwa wingi uwanjani hapo kwa kati ya sh 10,000 hadi 15,000.
Katika hatua nyingine, mashabiki hao wa Yanga, walimchania fulana ya Simba kijana mmoja ambaye alifika uwanjani hapo kwa shughuli zake binafsi.


Polisi Mara kumfikisha mahakamani aliyemshikia panga karani wa sensa




JESHI la polisi mkoani Mara linatarajia kumfikisha mahakamani mtu mmoja aitwaye Issa Ibrahimu 30 mkazi wa kamunyonge katika manspaa ya Musoma kwa kosa la kumshikia panga karani wa Sensa

Akiongea na waandishi wa habari jana ofisini kwake kwa niaba ya kamanda wa polisi,mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Mara Emanuel Lukula alisema kuwa  mtuhumiwa huyo alikamatwa Agost 26 mwaka huu baada ya kumshikia  panga karani wa Sensa na kumfukuza huku akidai kuwa imani ya dini yake ya kiislam haimuruhusu yeye pamoja na familia yake kuhesabiwa.

Lukula alisema kuwa baada ya karani huyo kupata vitisho hivyo alienda hadi katika kituo cha polisi ambapo alitoa taarifa na ndipo polisi walienda na kumakamata na kumfungulia mashitaka na kwamba upelelezi ukikamilika watamfikisha mahakamani ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabiri.

Kaimu kamanda huyo alisema kuwa hadi jana ofisi yake ilikuwa haijapata taarifa kuhusu watu wengeine ambao wanatuhumiwa kuvuruga zoezi la Sensa katika mkoa mzima wa Mara na hivyo akatoa wito kwa wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa ambao wanaendelea na zoezi hilo hivi sasa.

‘’Kwakweli hatujapokea taarifa nyingine ikiacha hii na nyingine kule wilayani Bunda ambako alikamatwa mwenyekiti wa kitongoji ambaye tayari ameshafikishwa mahakamani kwa kosa kama hili kwa hiyo ni matumaini yetu kuwa zoezi litaenda vizuri’’alisema Lukula.

Aliongeza kuwa jeshi la polisi mkoani humo halitamuea aibu mtu yeyote atakayejaribu kuvuruga zoezi la Sensa ya watu na makazi linaloendelea hivi sasa na kwamba atakayejaribu atakamatwa anafikishwa mahakamani kwa mjibu wa sheria ya Takwimu.


Thursday, August 30, 2012

wachimba migodi kufunguliwa mashitaka




Wachimba migodi wa Marikana waliokamatwa
Wendesha mashtaka wa serikali nchini Afrika Kusini wanasema kuwa wanajianda kuwafungulia mashtaka ya mauaji wachimba migodi wa mgodi wa Marikana.
Ripoti zinasema pia, wachimba migodi hao, wanakabiliwa na mashtaka mengine ikiwemo jaribio la mauaji ya wachimba migodi thelathini na wanne ambao waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Msemaji wa ofisi ya kiongozi wa mashtaka nchini humo, amesema ikiwa watu, ambao baadhi yao wamejihami wakiwakabili polisi na kutokee mauaji, wale watakaoshikwa na polisi watafunguliwa mashtaka ya mauaji, bila kujali wale waliofyatua risasi.
Polisi waliwapiga risasi wachimba migodi hao kufuatia ghasia na maandamano kuhusu mishahara.
Maafisa wawili wa polisi waliuawa kwenye machafuko hayo.
Habari hii ni kwa idhini ya idhaa ya kiswahili ya BBC

Wachimba migodi watoweka nchini china


Wachimba migodi ishirini na nane hawajulikani waliko kusini magharibi mwa Uchina baada ya mlipuko kutokea na kuwaua wafanyikazi wenzao kumi na tisa.
Shirika la habari la kitaifa nchini humo limesema kuwa makundi ya waokoaji kutoka migodi mingine waliweza kuwaokoa zaidi ya watu mia moja baada ya mlipuko wa gesi katika machimbo ya Sichuan .
Takwimu rasmi za serikali zinasema kuwa takriban watu elfu mbili wameuawa katika ajali za migodi nchini Uchina ambazo zimetajwa kuwa hatari zaidi duniani.
Vifo hivyo pia vinasemekana kupungua katika miaka ya hivi karibuni japo waandishi wanasema kuwa huenda baadhi ya ajali zinakosa kuripotiwa.

Hapo vipi

  usishngaae ndo mambo ya dunia vioja/vitimbi





Michezo

Fulham yazikubali senti za Tottenham


Moussa Dembele
Mchezaji wa Ubelgiji Moussa Dembele kuichezea Tottenham
Klabu ya Tottenham imepata idhini ya kuendelea mbele na mipango yake ya kushauriana na kiungo cha kati wa klabu ya Fulham, Moussa Dembele, kufuatia vilabu hivyo kuafikiana juu ya malipo ya kumnunua mchezaji huyo.
Mchezaji huyo wa Ubelgiji yumo katika hali ya kuhudumu mwaka wake wa mwisho katika mkataba na timu hiyo ya Fulham inayochezea uwanja wa Craven Cottage, na hakushiriki katika mechi ya kombe la Capital One dhidi ya Sheffield Wednesday, wakati timu yake iliposhindwa.
Meneja wa Fulham, Martin Jol, amesema Dembele, mwenye umri wa miaka 25, yumo katika hali ya kupimwa hali yake ya afya katika klabu ya Tottenham.
Dembele aliingia Fulham kutoka klabu ya Uholanzi ya AZ Alkmaar, kwa gharama ya pauni milioni 5, mwaka 2010.
Hayo yakiendelea, Fulham imekuwa katika hali ya kushauriana na Kieran Richardson, baada ya kuelewana na Sunderland kuhusu kitita kinachohitajika kumpata mlinzi huyo.
Meneja wa Sunderland, Martin O'Neill alithibitisha kwamba tayari wamekubaliana juu ya kiwango cha pesa ambazo Fulham watatoa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.
Habari hii kwa hisani ya idhaa ya Kiswahili ya BBC 

Serikali ya Syria inatumia mabavu

Serikali ya Syria inatumia mabavu' asema Morsi


Rais Mohammed Morsi
Rais wa Misri, Mohammed Morsi, ameikashifu serikali ya Syria na kusema kuwa inatumia mabavu.
Rais Morsi aliyasema hayo katika hotuba yake nchini Iran ambayo ni mshirika mkubwa wa Syria.
Morsi alisema kuwa ni wajibu wa kila mtu kuunga mkono upinzani nchini Syria ili uungane dhidi ya kile alichokitaja kama utawala wa kimabavu.
Katika hotuba yake katika mkutano maalum mjini Tehran, bwana Morsi alisema kuwa ni jukumu lao kimaadili kuunga mkono upinzani nchini Syria sawa na kuwa mkakati sawa wa kisiasa
Waziri wa mambo ya nje wa Syria, Walid Mouallem, alisema kuwa wajumbe wa Syria waliondoka kwenye mkutano huo wakati wa hotuba ya rais Morsi, ambayo aliitaja kama ya uchochezi wa kuendelea kumwaga damu ya wanachi wa Syria.
Ziara ya rais Morsini ya kwanza ya afisaa mkuu wa Misri, tangu mapinduzi ya kiisilamu mwaka 1979.

Magwegwe na mke wake wakiwa katika hosptal ya Musoma ambako wamelazwa

Magwewe akiwa na mke wake Chausiku  ambapo wote wamelazwa katika hosptal ya mkoa wa Mara baada  ya kuvamia na majambazi na kisha kuporwa shilingi laki tisa -picha na Berensi AlikadiAdd caption

MAJAMBAZI YAVAMIA NA KUPORA LAKI TISA



NA Berensi Alikadi-Musoma

MKAZI mmoja wa kijiji cha Maneke kilichoko kata ya Tegeruka wilaya ya Musoma,Magwegwe Chiriso 36 amelazwa katika hospital ya mkoa wa Mara baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na kisha kumpora kiasi cha shilingi laki tisa.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi  jana katika wodi namba 8 lililopo katika hosptali hiyo Magwegwe amesema kuwa tukio hilo limetokea Agost 20 mwaka huu majira ya saa 6 usiku  ghafula alisikia mlango ukikongwa na jiwe kubwa maarufu kama Fatuma.

Alisema kuwa baada ya majambazi hao kubomoa mlango huo waliingia ndani  majambazi wawili wakiwa na silaha za jadi ambapo walimuamilisha yeye na mke wake wake wawape pesa kiasi cha shilingi laki saba huku wakiwakata kata kwa mapanga.

Magwegwe alifafanua kuwa baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya aliwaambia kuwa pesa ziko sandukuni ambapo walibomoa sanduku na kuchukuwa kiasi cha shilingi laki tisa na kisha wakaotokomea kusikojulikana.

Alifafanua kuwa baada ya kuona wameondoka yeye na mke wake walipiga yowe ambapo majirani walifika na kuwachukuwa hadi katika kituo cha polisi Musoma ambako walipewa fomu namba 3 na kisha kwenda kutibiwa katika hospital hiyo ambako amelazwa yeye na mke wake. Wakiendelea na matibabu.

Mhudumu wa zamu katika wodi hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa madai kuwa yeye si msemaji wa hospital hiyo amesema kuwa hali za watu hao zinaendelea vizuri.

Akizungumzia tukio hilo kwa niaba ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara,mkuu wa upelelezi wa mkoa huo Emanuel Lukula amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa polisi bado wanaendelea kufanya upelelezi ili kuwabaini wale wote waliohusika na tukio hilo ili waweze kufikishwa mahakamani.

MWISHO

Human Right wartch yataka upelelezi zaidi ufanyike

Polisi wa 
Mombasa, Kenya

Matukio ya Afrika

Human Rights Watch yataka upelelezi ufanyike

Kufuatia kuuawa kwa mhubiri Aboud Rogo mjini Mombasa, shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch sasa limeitaka serikali ya Kenya ifanye uchunguzi juu ya mauaji hayo na ghasia zilizozuka.
Aboud Rogo, aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka ya kumiliki silaha kimagendo na kutafuta watu wa kujiunga na kundi la waislamu wenye itikadi kali la al-Shabaab, aliuliwa siku ya Jumatatu kwa kupigwa risasi alipokuwa akiendesha gari lake nje ya mji wa Mombasa. Kufuatia mazishi yake yaliyofanyika siku hiyo ya Jumatatu, machafuko yalizuka katikati ya mji wa Mombasa na kuendelea hadi leo. Magari yalichomwa moto, makanisa yalivamiwa na watu wasiopungua wawili waliuwawa. Mmoja wao alikuwa afisa wa magereza aliyekuwa akishirikiana na polisi kutuliza ghasia na wa pili alikuwa raia wa kawaida aliyeuwawa na waandamanaji. Polisi wa mjini Mombasa waliwaambia waandishi wa habari kwamba wamewakamata watu 23 wanaotuhumiwa kuhusika na machafuko yaliyotokea.

Aboud Rogo alipokuwa katika mahakama kuu jijini Nairobi Aboud Rogo alipokuwa katika mahakama kuu jijini Nairobi
Akizungumza na DW kwa njia ya simu, Ben Rawlence wa shirika la Human Rights Watch ambaye kwa sasa yuko Mombasa, Kenya, alisema kwamba Rogo aliwaeleza polisi kwamba alikuwa akihofia usalama wake. "Aliomba kulindwa na serikali," alisema Rawlence. "Hata kama mtu yuko katika orodha ya magaidi bado kuna sheria inayotakiwa ifuatwe na ilipaswa Rogo aende mahakamani na si kuuliwa mtaani."
Naye Leslie Lefkow, ambaye ni naibu mkurugenzi wa Human Rights Watch barani Afrika, amewataka polisi wa nchini Kenya wazingatie sheria katika kudhibiti ghasia zilizotokea baada ya kifo cha Rogo.
Washukiwa wengine wametekwa au kuuawa
Kifo hicho kimekuja baada ya visa vingine vya utekaji nyara na hata mauaji ya watu walioshukiwa kutafuta wapiganaji wa kujiunga na kundi la al-Shabaab na kufanya makosa mengine yanayohusishwa na kundi hilo.

Gari alilokuwa akiendesha Rogo aliposhambuliwa na risasi Gari alilokuwa akiendesha Rogo aliposhambuliwa na risasi
Mwezi Machi mwaka huu, Samir Khan, ambaye pia ameshtakiwa kwa makosa hayo, pamoja na rafiki yake Mohammed Kassim, walitolewa kwa nguvu kutoka katika basi moja mjini Mombasa. Wakili wa Khan, Bw. Mbugua Mureithi, ameeleza kwamba waliolisimamisha basi hilo ni watu waliojitambulisha kuwa polisi. Siku chache baadaye, maiti ya Khan iliyokuwa imeharibiwa vibaya, ilikutwa katika mbunga ya wanyama ya Tsavo.
Mpaka sasa haifahamiki Mohammed Kassim alipo. Kabla ya kutolewa katika basi, mwezi Februari mwaka huu, Kassim alitekwa nyara na kuachiwa baada ya kuhojiwa na wale waliomteka. Polisi walifanya mkutano na waandishi wa habari na kuarifu kwamba Kassim alikuwa ametekwa na polisi wa kupambana na ugaidi. Hata hivyo, polisi hao baadaye walikanusha kuhusika na utekaji nyara uliofanyika.
Mwandishi: Elizabeth Shoo/HWR
Mhariri: Josephat Charo
  • T
Habari zote kwa idhini ya sauti ya ujerumani

opresheni kali dhidi ya wapiganaji Sinai


Operesheni kali dhidi ya wapigananaji Sinai



Ulinzi mkali Sinai
Maafisa wa usalama nchini Misri, wamewaua wapiganaji kumi na moja tangu kuanzisha operesheni kali dhidi ya wapiganaji hao katika rasi ya Sinai, mapema mwezi huu . Hii ni kwa mujibu wa taarifa za wizara ya ulinzi nchini Misri.
Operesheni hiyo, iliyoanzishwa baada ya kuuawa kwa walinzi kumi na sita wa mpakani katika shambulizi lililofanywa tarehe tano mwezi huu, pia imewezesha kukamatwa kwa washukiwa 23 na hata kunasa silaha.
Maafisa wengine wa ulinzi walitarajiwa kepelekwa huko hii mnamo Jumatano kuweza kukamilisha msako wa washukiwa wa ugaidi.
Hata hivyo, hatua ya kuongeza idadi ya wanajeshi mpakani tayari imeweza kuzua wasiwasi kwa serikali ya Israel.
Tangu mwaka 1982, wakati wanajeshi wa Israel walipoondoka mpakani eneo la sinai limesalia chini ya ulinzi mkali, kufuatia makubaliano ya amani kati ya nchi hizo mbili ambayo yalisainiwa mwaka 1979, ambayo yanazuia Misri kutumia nguvu za kijeshi katika eneo hilo.
Mnamo siku ya Jumatatu,rais wa Misri, Mohammed Mursi alisisitiza kuwa nchi yake itatii mikataba yote ya kimataifa na bila ya kutaja Israel ikasema kuwa hakuna nchi zingine zinapaswa kuwa na wasiwasi kuhusu hatua zake huko Sinai.
Misri ilianzisha operesheni yake ya usalama kwa jina "Operation Eagle", ambayo imehusisha maelfu ya wanajeshi wakisaidiwa na vifaru na silaha zingine nzito baada ya walinzi kumi na sita kuuawa katika operesheni dhidi ya kambi yao karibu na ukanda wa Gaza.
Baada ya kuwaua wanajeshi, wapiganaji hao walivuka mpaka na Israel katika jariibio lao kufanya shambulizi lengine. Ingawa waliuawa katiakmashambulizi ya angani yaliyofanywa na Israel.
Hata hivyo yeyote amewajibika na mashambulizi hayo ingawa wanaoshukiwa sana kuhusika ni makundi ya wapiganaji ambayo yanajulikana kwa kuendesha shughuli zao mashariki mwa Sinai.
Katika siku za kwanza za operesheni hiyo majeshi yalifanya msako mkali katika maficho ya wapiganaji hao.

Kwa habari zaidi  soma BBC Swahili.

Aina mpya ya binadamu wa kale Kenya



hominid
Kwa mujibu wa ushahidi wa visukuku vilivyopatikana Kaskazini mwa Kenya kuna aina mpya ya binadamu walioishi huko takriban miaka milioni mbili iliyopita, wamesema wataalamu.
Uvumbuzi huu unaibua hisia kuwa aina tatu za viumbe waliishi kwa wakati mmoja barani Afrika. Utafiti huu unaongezea ushahidi mwingine ambao haukubaliani na dhana maarufu kuwa asili ya mwanadamu wa leo alitokana na nyani.
Utafiti huu umechapishwa kwenye jarida la Nature.
Wana athropolojia ama wataalamu wanaotafiti masuala ya kale wamegundua mabaki au visukuku(fossils) vya binadamu vyenye umri wa miaka iliyo kati ya milioni 1.78 na milioni 1.95. Visukuku hivi ni vya uso ukiwa na mifupa ya taya miwili ikiwa na meno yake.
Natural History Museum, London
Ugunduzi huu unakubaliana na mtazamo kuwa fuvu lililopatikana mnamo mwaka 1972 lilikua la aina ya binadamu tofauti anayejulikana kama Homo rudolfensis. Fuvu hili lililkua tafauti na mengine ya nyakati hizo na haikua rahisi kubaini kama kiumbe huyu alikua na tafauti au ni kiumbe tofauti wa aina mpya ya viumbe.
Mafuvu mapya
Kwa kipindi cha miaka 40 fuvu hili ndiyo mfano pekee uliokuepo wa kiumbe kwa hiyo haikua rahisi kubaini kama kiumbe huyu alikua wa kipekee au mmoja wa viumbe wapya.
Kwa ugunduzi wa visukuku wapya watatu wataalamu sasa wanaweza kusema bila kusita kwamba H.rudolfensis kweli alikua aina tofauti ya kiumbe binadamu aliyeishi takriban miaka milioni mbili iliyopita sambamba na aina nyingine za binadamu.
Kwa mda mrefu babu wa binadamu aliyefahamika alidhaniwa kua aina kutoka nyani, wanaodhaniwa kua waliishi miaka milioni 1.8 iliyopita wakijulikana kama Homo erectus. Walikua na vichwa vyembamba, nyusi zilizotanda na walisimama wima.
Lakini miaka 50 iliyopita, wataalamu waligundua mifano iliyoishi kabla ya hapo na iliyoishi kama nyani ikijulikana kama Homo habilis ambayo huenda iliishi wakati mmoja na H.erectus. Ushahidi wa sasa unaonyesha kua wakati huo H. rudolfensis alikuepo pia na kuleta dalili za kua huenda ikawa aina nyingine ya binadamu waliishi wakati huo.
Uvumbuzi wa sasa ni ushahidi unaozidi kufuta dhana ya kwamba sisi tulianza mwendo wa kubadili maumbile yetu kutoka nyani anayekwenda kwa kujikongoja taratibu hadi tulipoinuka kusimama kama binadamu wa leo.
Badala yake, kwa mujibu wa Dr Meave Leakey wa chuo cha Turkana Basin mjini Nairobi, aliyeongoza utafiti huo anasema kua uvumbuzi huu tofauti ilikuepo mapema katika kubadilika kwetu kama viumbe.
Dr.Leakey ameiambia BBC kuwa kama viumbe tumepitia mabadiliko kwa njiia moja na wanyama wengine walivyobadilika. Hatukua na tofauti yoyote hadi tulipoanza kuunda vifaa vya mawe''
Katika aina nyingine za wanyama, kila mmoja amepitia mabadiliko mbalimbali, kila moja wao na aina mpya ya tabia maumbile, kama mabawa, au miguu yenye kucha zisizo baini kucha. Ikiwa aina mpya ya maumbile haikidhi mahitaji na kuendana na mazingira basi kiumbe mpya ataendelea kuishi vinginevyo anatoweka kabisa.
Kwa mujibu wa Profesa Chris Stringer wa jumba la kumbukumbu au Natural History Museum mjini London, ushahidi wa visukuku na mafuvu unazidi kuonyesha kua mabadiliko ya viumbe yalifuata mkondo mmoja.

Vurugu za mombsa baada ya kifocha Aboud Rogo

Vurugu za mombasa baada ya kifo cha Aboud Rogo

Ghasia zilizozuka baada ya kuuawa kwa mhubiri mashuhuri mjini Mombasa Aboud Rogo. Vurugu zilitokea siku mbili mfululizo katika maeneo ya Mombasa mjini.

Wednesday, August 29, 2012

Porisi watatu wafariki katika ghasia Mombasa





Fujo zaendelea Mombasa kwa siku ya pili mfululizo
Hali ya wasiwasi ingali imetanda mjini Mombasa kwa siku ya tatu baada ya ghasia za siku mbili kufuatia kifo cha mhubiri wa kiisilamu Sheikh Aboud Rogo siku ya Jumatatu.
Inaarifiwa vijana wanalenga kufanya mashambulizi ya kuvizia wakirusha matairi na vifaa vingine barabarani na kisha kutoroka, licha ya kuwa polisi wanashika doria.
Polisi wawili wamethibitishwa kufariki kutokana na majeraha yao baada ya shambulio la guruneti dhidi ya gari lao mjini Mombasa hapo jana.
Hadi kufikia sasa polisi watatu wamefariki tangu kuanza kwa ghasia zilizotokea baada ya kifo cha mhubri wa kiisilamu mwenye siasa kali Sheikh Aboud Rogo siku ya Jumatatu.
Kwa siku mbili, vijana wa kiisilamu wamekuwa wakipambana na polisi katika barabara za Mombasa wakifanya uharibifu kuchoma magari na kupora maduka pamoja na kuvamia makanisa mjini humo. Watu wengine kumi na tatu walijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo.
Mhubiri Aboud Rogo Mohammed, alikuwa mshukiwa wa ugaidi na pia alishukiwa kufadhili kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia.
Wakati huohuo, watu 12 wamekamatwa na polisi kufuatia makabiliano kati ya polisi na vijana wanaofanya vurugu kufuatia kuuwawa kwa kiongozi wa kidini Sheikh Aboud Rogo siku ya jumatatu.
Katika siku ya pili ya vurugu hizo, wengi ya vijana hao wamekamatwa nje ya Msikiti Musa iliyo eneo la Majengo visiwani Mombasa.
Wakati wa makabiliano hayo polisi walitumia gesi ya kuolisitoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa na ghadhabu.
Hata hivyo katika eneo moja polisi walilazimika kutumia risasi za mpira kuwatawanya vijana waliokuwa wakiwasha matairi barabarini na kufanya uporaji.
Bwana mmoja alichomwa kisu katika karakana yake na kulazimika kupewa huduma ya kwanza na wafuasi wa dhehebu la Jeshi la wokovu.
Na wakati Mombasa ikiwaka moto, wapiganaji wa Al shabaab wametuma ujumbe katika mtandao wao wakiwasihi waislamu wa Kenya "wachukuwe kila hatua zinazostahili kulinda dini yao"
" Waislamu lazima wachukue sheria mikononi mwao, na wasimame kidete dhidi ya makafiri na kuchukua kila hatua kuilinda dini yao, heshima yao ,mali yao na maisha yao kutoka kwa maadui wa waislamu" , Al shabaab wamenukuliwa wakisema hayo katika taarifa yao.
Kiongozi huyo wa kidini Sheikh Aboud Rogo ,aliyepigwa risasi na kuuwa siku ya jumatatu alikuwa ametajwa na Marekani pamoja na Umoja wa Mataifa kama mtua anayewasajili baadhi ya vijana wa Kenya wkenda kujiunga na wapiganaji wa Al Shabaab.
Sheikh Aboud Rogo pia anadaiwa kuwa alikuwa mfadhili wa kundi hilo la Al shabaab.

Habari hii ni kwa hisani ya idhaa ya kiswahili ya BBC

MWALIMU WA KIISLAMU KOTINI KWA KUGOMA KUHESABIWA

Kortini kwa kugoma kuhesabiwa

na Jovither Kaijage, Ukerewe

MWALIMU wa dini ya Kiislamu, Mohamed Iddi (25), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ukerewe, Mwanza akikabiliwa na shitaka la kupinga kuhesabiwa.
Iddi, mkazi wa Kiloleli, alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Rouben Luhasha.
Akimsomea shitaka hilo, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Samwel Onyongo, alidai Agosti 26 mwaka huu, katika nyumba ya kulala wageni ya Baba Kapaya iliyoko kitongoji cha Mviringo A, mjini Nansio, mshitakiwa kwa makusudi alikataa kutoa taarifa zake kwa karani wa sensa ya watu na makazi, John Msafiri aliyepewa wajibu huo kwa mujibu wa sheria.
Mshitakiwa alikana tuhuma hizo na amepelekwa rumande baada ya kukosa wadhamini. Kesi itatajwa Septemba 11, mwaka huu.
Kwa mujibu wa sheria, mtu akithibitika kutenda kosa hilo na mengine ya namna hiyo atahukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya sh 600,000 au adhabu zote mbili kwa pamoja.
Katika tukio jingine, baadhi ya makarani wa sensa wilayani Ukerewe, wameishiwa vifaa hasa fomu za kujaza taarifa za watu, hali inayoweza kuwa kikwazo kingine katika kufanikisha sensa hiyo.
Mratibu wa sensa wa wilaya hiyo, alisema hayo jana alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya maendeleo ya sensa.
Alivitaja vifaa ambavyo vimeisha kuwa ni nakala 7,500 za dodoso refu na dodoso fupi nakala 10,000 ambapo baadhi ya vifaa zikiwemo kalamu 950 za wino wa bluu hazijapelekwa kabisa.
Alivitaja vifaa vingine vilivyopungua kuwa ni sare 875 za makarani wa sensa, vibao 50 vya kusiliba fomu pamoja na kalamu 50 zenye wino mwekundu.


kwa habari zaidi soma Tanzania daima  Agost 31

Habari za kimataifa

Assad ahitaji muda zaidi kushinda vita



Rais Bashr Al Assad
Rais wa Syria Bashar al-Assad amesema kuwa serikali yake inahitaji muda wa ziada kuweza kushinda vita dhidi ya waasi nchini humo.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha televisheni kinachounga mkono serikali ya Assad,
rais huyo pia alipuuza tamko kuwa haiwezekani kutenga maeneo ya kutolea misaada katika maeneo ya mipaka nchini humo,
Wanaharakati wa upinzani wanadai kuwa jeshi limefanya mashambulizi katika maeneo mengi ya nchi hiyo kutaka kudhibiti maeneo yaliyotekwa na waasi.
Mapambano makali yaliripotiwa kutokea siku ya Jumanne katika mji mkuu Damascus, Aleppo na mkoa wa kaskazini masharibi wa Idlib.
Bwana Assad amesema kuwa serikali yake iko kwenye vita ndani na nje ya nchi.
Athari za vita , mtoto wa Syria akiwa mpakani mwa nchi hiyo na Uturuki
"bila shaka tunahitaji muda zaidi kuweza kumaliza vita hivi katika njia inayofaa. Lakini ninachoweza kusema ka neno moja tu ni tunapiga hatua''. Bwana Assad alisema.
"hali kwa sasa angalau ni nzuri, lakini bado hatujafika mwisho. Hilo bila shaka linahitaji muda zaidi'' alisema Assad
''Maafisa wa ulinzi wanafanya kitendo ha ushujaa kwa kila hali. Lakini waasi hawataruhusiwa kueleza hofu wala hawataruhusiwa kiufanya hivyo.'' aliongeza rais Assad.
Kila mtu hapa nchini ana wasiwasi kuhusu hali ya nchi yetu, hilo ni jambo la kawaida.Ninawaambia wananchi wa Syria, mustakabali a nchi hii uko mikononi mwenu, wala sio mikononi mwa watu wengine''.
Rais aliwakejeli maafisa wakuu wa serikali na jeshi ambao wameasi serikali katika miezi ya hivi karibuni akisema kuwa hatua hiyo iliweza kuisafi serikali mwanzo na kisha nchi kwa ujumla.

Chanzo BBC Swahili.



MAZISHI YA JOHN ATTA MILLS

vifo vya mapema kwa marais barani Afrika! kwa nini?



Mazishi ya John Atta Mills
Ni nadra kwa kiongozi wa nchi yoyote kufariki akiwa angali madarakani.
Tangu mwaka 2008, hili limefanyika mara kumi na tatu kote duniani -lakini kumi kati ya viongozi hao wamekuwa marais wa nchi za afrika.
Kwa nini vifo kama hivi vinatokea sana barani Afrika?
Makundi makubwa ya watu walikusanyika kushuhudia jeneza la hayati waziri mkuu wa Ethiopia meles Zenawi
lilipokuwa likipitishwa katikati mwa mji mkuu Addis Ababa, mnamo siku ya Jumanne wiki iliyopita. Alifariki akiwa na umri wa miaka 57, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Meles Zenawi
Mapema mwezi huu, maelfu ya wananchi wa Ghana walihudhuria mazishi ya hayati rais, John Atta Mills, aliyefariki ghafla akiwa na umri wa miaka 68.
Miezi minne kabla ya kifo cha Atta Mills, siku ya kitaifa ilitangazwa nchini Malawi kuwezesha maelfu ya watu kuhudhuria mazishi ya hayati rais Bingu wa Mutharika, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 78 kutokana na mshtuko wa moyo.
Na mnamo mwezi Januari, rais wa Guinea Bissau, Malam Bacai Sanha, alifariki katika hospitali ya kijeshi mjini paris baada ya kuugua kwa muda mrefu. Alikuwa na umri wa miaka 64.
Kwa hivyo viongozi wanne wa Afrika wamefariki mwaka huu pekee . Bila shaka ni pigo kwa nchi husika na huzuni kubwa kwa familia za viongozi hao. Lakini je mwandishi wa habari atafsiri vipi matukio haya?

Bingu wa Mutharika
"Kila usiku Napata simu nyingi kutoka kwa watu wengi kuniambia rais wa Afrika ameaga dunia" anasema
Simon Allison, mwandishi habari wa mtandao wa habari wa Daily Maverick nchini Afrika Kusini. "Kwa nini viongozi wengi wa Afrika wanafariki sana wakati huu? anahoji Simon.
Swali hili bila shaka linasababisha tathmini ya maisha ya viongozi hao.
" Ukitafakari kidogo orodha ya viongozi wa Afrika waliofariki bila shaka ni ndefu'' anasemaAllison. Tangu mwaka 2008, viongozi 10 wa Afrika wamefariki wakiwa madarakani.
Viongozi wengine wa Afrika waliofariki wakiwa madarakani ni pamoja na Muammar Gaddafi akiwa na miaka 69. Aliauawa wakati wa mapinduzi ya kiraia nchini Libya Oktoba mwaka 2011

Muamar Gadaffi
Aliyekuwa rais wa Nigeria Umaru Yar'Adua aliaga akiwa na miaka 58 mwezi Mei mwaka 2010 kutokana na maradhi ya figo pamoja na moyo.
Omar Bongo wa Gabon akiwa na miaka 73 alifariki mwaka 2009
Raia wa Guinea Bissau president, J B Vieira umri wa miaka 69 aliuawa mwezi Machi mwaka 2009
Rais wa Guinea Lansana Conte aliaga akiwa na miaka 74 mwaka 2008, kutokana na sababu zisizojulikana.

Levy Mwanawasa
Aliyekuwa rais wa Zambia , Levy Mwanawasa akiwa na miaka 59 mwaka 2008, kutokana na kiharusi.
Bila shaka ni kweli kuwa viongozi wengi wa Afrika wanaaga dunia wakiwa wangali madarakani kuliko katika bara lengine lolote duniani. Katika kipindi hicho ni viongozi watatu pekee waliofariki wakiwa wangali madarakani kwingineko duniani.
Kim Jong Il wa Korea kaskazini , rais wa Poland, Lech Kaczynski, aliyefariki katika ajali ya ndege na David Thomson wa Barbados, aliyefariki kutokana na saratani.
Jibu la wazi ni kuwa marais wa Afrioka ndio wakongwe zaidi kuliko marais wa mabara mengine.Tathmini inayotolewa hapa ni kuwa waafrika wanapenda wenyewe kuwa na viongozi wazee kwani kulingana na utamaduni , wanapata heshima kubwa kutoka kwa jamii.
Muda mrefu zaidi ambao marais wa Afrika wanaweza kuishi inakadariwa kuwa miaka 61 sawa na bara Asia. Viongozi wa bara la Afrika, umri wao unakakadiriwa kuwa miaka 55 wakati barani Afrika rais mkongwe zaidi anakadiriwa kuwa na miaka 59.
Lakini kitu kingine cha kutafakari ni umri mrefu zaidi wanaoishi watu wa bara hilo ikikadiriwa kuwa chini sana barani Afrika ikilinganishwa na mabara mengine kama Uropa, Amerika ya kusini na barani Asia.
Sababu kuu hapa ikiwa ni janga la ukimwi, na pia miundo msingi duni ya afya ambayo inachangia idadi kubwa ya vifo hasa miongoni mwa watoto wachanga.
Lakini umaskini katika maisha ya ujana na kwa watoto wachanga pia zinaathiri kubwa katika umri wa mtu kulingana na daktari George Leeson wa chuo kikuu cha Oxford.
"marais wa Afrika kabla ya kuchaguliwa huenda waliishi maisha ambayo sio mazuri sana na bila shaka hilo litaathiri maisha yao uzeeni'' anasema daktari Leeson.
Kwa hivyo wakati wanapoingia madarakani, licha ya kuwa sasa wanaishi maisha ya kifahari zaidi kuliko siku zao za utotoni, bado athari za maisha duni walipokuwa wachanga huwaandama
Lakini hii haimaanishi kuwa viongozi wote wa Afrika waliishi maisha duni walipokuwa wadogo. Kuna mambo mengine chungu nzima ya kuzingatia. Mfano, siasa, dhana kwamba, viongozi wa afrika wanapenda kung'ang'ania madarakani, hadi watapofariki. Lakini dhana hii ingali kuthibitishwa.
Lakini kunao viongozi waliong'ang'ania madaraka hadi wakafa, kama vile Omar Bongo, Conte na Gaddafi, kulingana na tathmini mbali mbali. Lakini wengine kama Meles Zenawi waligandia tu madarakani , kwa sababu kama Zenawi, alikuwa na miaka 57 pakee.
Hata hivyo ni muhimu kujua kuwa tathmini hii ni ya viongoiz tu waliofariki wakiwa ofisini tangu mwaka 2008.

Baadhi ya wanyama wakiwa katika hifadhi ya Serengeti


Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad