Thursday, September 17, 2015
13 wauwawa kwa bomu Baghdad
Kiasi watu 13, ikiwa ni pamoja na mshambuliaji wa kujitoa muhanga , wamekufa leo katika mashambulizi mawili tofauti katikati ya mji mkuu wa Iraq Baghdad.
polisi imesema shambulio la kwanza lilitokea katika wilaya ya kibiashara ya Bab al-Sharj ambako bomu liliripuka katika gari iliyoegeshwa. Watu wanane waliuwawa na wengine 40 wamejeruhiwa.
Mshambuliaji wa kujitoa muhanga , akivalia mkanda wa miripuko , alijiripua katika eneo la Wathba , akijiuwa binafsi na watu wengine wanne. Maafisa wa polisi ni miongoni mwa waliouwawa.
Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo hadi sasa. Mashambulizi ya hapo kabla yamedaiwa kutekelezwa na kundi la Dola la Kiislamu, ambalo linadhibiti maeneo makubwa kaskazini na magharibi ya Iraq.
CHANZO BBC
Wanajeshi wamkamata rais na waziri mkuu Burkina Faso
Kikosi cha ulinzi wa rais nchini Burkina Faso kimetangaza mapinduzi leo siku moja baada ya kuwakamata rais wa mpito na waziri mkuu jana, wakati nchi hiyo ikijitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa kwanza tangu kupinduliwa kwa kiongozi wa nchi hiyo Blaise Compaore.
Akitangaza mapinduzi luteni kanali Mamadou Bamba amesema mazungumzo yanafanyika hivi sasa kuunda serikali itakayoiongoza nchi hiyo katika uchaguzi wa amani.
Kumekuwa na maandamano mitaani nje ya Ikulu ya rais na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limeshutumu vikali kukamatwa kwa viongozi hao na kutaka waachiliwe haraka.
Wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa rais wenye mafungamano na rais wa zamani Blaise Compaore waliingia katika mkutano wa baraza la mawaziri jana na kumkamata rais Michel Kafando, waziri mkuu Isaac Zida na mawaziri wengine wawili.
Kaimu spika wa bunge la Burkina Faso Cherif Sy ameshutumu vikali leo kile alichosema kuwa ni mapinduzi nchini Burkina Faso.
CHANZO BBC
Wahamiaji wamiminika Croatia
:
Mamlaka nchini Croatia zimesema zinaunda bodi maalumu ya kukabiliana na umiminikaji huwo wa wakimbizi. Waziri wa mambo ya ndani Ranko Ostojic ameseme hadi sasa Croatia imeweza kuidhibiti hali hiyo ila alionya kuwa pale wimbi la wakimbizi kutokea Serbia litakapoanza kuingia nchini humo basi hatua mpya zitahitajika kutumika.
Hapa Ujerumani msemaji mkuu wa Polisi amesema leo idadi ya wahamiaji walioingia nchini tangu jana imeongezeka marudufu hadi kufikia watu 7,266. Naye kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema leo kuwa Ujerumani inazingati njia za kuwasaidia wahamiaji kuzoea maisha ya Kijerumani na maadili ya nchi:
CHANZO BBC

Maelfu ya wakimbizi wameanza kumiminika nchini Croatia leo hii baada ya
kurushiwa mabomu ya machozi nchini Hungary. Idadi ya wakimbizi hao
walioingia Ujerumani jana pia imeripotiwa kuongezeka maradufu.
Wahamiaji nchini Croatia
Maelfu ya wakimbizi wanamiminika nchini Croatia kama njia mpya ya
kuingilia Ulaya ya magharibi baada ya kufukuzwa nchini Hungary kwa
kurushiwa mabomu ya kutoa machozi pamoja na maji ya kuwasha. Polisi wa
Croatia imesema wahamiaji 5,650 wameingia nchini humo leo hii, lakini
kundi la mwanzo la wahamiaji lilianza kuingia nchini humo mapema jana.
Mamlaka husika zimekuwa zikitumia mabasi pamoja na treni kuwasafirisha
na kuwapeleka katika vituo vya wakimbizi.Mamlaka nchini Croatia zimesema zinaunda bodi maalumu ya kukabiliana na umiminikaji huwo wa wakimbizi. Waziri wa mambo ya ndani Ranko Ostojic ameseme hadi sasa Croatia imeweza kuidhibiti hali hiyo ila alionya kuwa pale wimbi la wakimbizi kutokea Serbia litakapoanza kuingia nchini humo basi hatua mpya zitahitajika kutumika.
Hapa Ujerumani msemaji mkuu wa Polisi amesema leo idadi ya wahamiaji walioingia nchini tangu jana imeongezeka marudufu hadi kufikia watu 7,266. Naye kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema leo kuwa Ujerumani inazingati njia za kuwasaidia wahamiaji kuzoea maisha ya Kijerumani na maadili ya nchi:
CHANZO BBC
Serikali ya mpito Burkina faso yapindult
Kumefanyika mapinduzi nchini Burkina Fasso.
Kikosi
cha walinzi wa rais kimetangaza katika runinga ya taifa kwamba
kimevunjilia mbali kile ilichokitaja kuwa serikali ya mpito
isiyoambilika.Mwanachama wa kikosi hicho jenerali Gilbert Diendere ametajwa kuwa kiongozi mpya wa mpito.

Kikosi cha walinzi wa rais kimefyatua risasi hewani katika mji mkuu wa Ouagadougou huku watu wakikongamana kufanya maandamano.
Rais wa mpito Michel Kafando amepokonywa madaraka yake huku serikali yake ikivunjiliwa mbali, kwa mujibu wa afisa mmoja wa jeshi aliyezungumza katika runinga ya taifa nchini humo RTB.

Hatua hiyo inajiri baada ya viongozi wa serikali hiyo ya mpito nchini Burkina Faso kuzuiliwa na walinzi wanaomtii aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Blaise Campaore aliyeng'atuliwa mamlakani.
Hakuna majeraha yalioripotiwa lakini kumedaiwa kuwepo kwa hali ya wasiwasi huku maduka yakifunga biashara mapema na raia wengi kuelekea majumbani mwao.

Bwana kafando na luteni kanali Zida walipewa jukumu la kuandaa uchaguzi mpya wa urais mwezi ujao.
Wao pamoja na maafisa wengine walitekwa nyara na walinzi wa RSP, mkuu wa bunge la mpito Moumina Cherrif Sy,alisema katika taarifa.
chanzo BBC
Wednesday, September 16, 2015
Wanasiasa 7 wafurushwa serikalini DRC

Wanasiasa saba waandamizi
wamefurushwa kutoka kwa serikali ya muungano katika Jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo baada ya kumuandikia rais wakimtaka kutokwamilia
madaraka, kulingana na maafisa.
Katika barua kwa Joseph
Kabila,viongozi wa G7,kundi lenye vyama ndani ya muungano huo lilitaka
hatua kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kufikia mwezi
Novemba.Mda wa kikatiba wa rais Kabila unakamilika mwaka ujao,lakini amekataa kuthibitisha kwamba hatowania muhula mwengine.
Upinzani pia unahofia kwamba uchaguzi huo utacheleweshwa.
Jumba refu zaidi Afrika mashariki lafunguliwa TZ

azinduliwa Tanzania
Jengo refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati lazinduliwa nchini Tanzania.
PSPF
Towers ni moja ya majengo machache marefu barani Afrika na ndiyo jengo
refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati, likiwa na urefu wa
mita 147.Majengo mengine marefu Afrika ni Carlton Centre (mita 223) lililopo Afrika Kusini, Hassan II Mosque (mita 210) lililopo Moroko, Ponte City (mita 173) lililopo Afrika Kusini, Necon House (Mita 160) lililopo Nigeria, Marble Tower (mita 152), Pear dawn (mita 152), Pear dawn (mita 152), Met Life Centre (mita 150) na 88 on field (mita 147) yote ya Afrika ya kusini.
Jengo hilo lililozinduliwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ujenzi wake ulitumia miaka minne tangu mwaka 2011 hadi 2015 limegharimu shilingi bilioni 139.20 za Tanzania lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi 88. Pia katika jengo hili kuna sehemu ya mgahawa, mabenki, bwawa la kuogelea, Sehemu za kufanyia mazoezi, maegesho ya magari na sehemu nyingine muhimu.
Kudumu kwa rekodi ya urefu ya PSPF Towers lenye minara miwili na ukubwa wa mita za mraba 73,000, kutategemea kukamilika kwa majengo mengine yanayochipua kwa kasi katika Afrika.
CHANZO BBC
Chile yapigwa na tetemeko

Tetemeko kubwa la ardhi limeipiga
Chile na kusababisha tishio la kutokea kwa tsunami, katika eneo lake la
pwani na maeneo mengine ya bahari ya Pacific.
Tetemeko hilo lenye
ukubwa wa 8.3 katika vipimo vya ritcha, lilipiga maeneo ya pwani na
kuenea kwa kilomita 250 kaskazini magharibi wa mji mkuu Santiago.Nchi hiyo imewahamisha wakazi milioni moja katika eneo la pwani, Rais wa Chile amethbitisha watu watano wamepoteza maisha baada ya tetemeko hilo kupiga
Kumeshuhudiwa matetemeko mingine midogomidogo katika eneo hilo.
ijuwe hifadhi ya serengeti

Eneo lake ni 14,763 km² na kijiografia inaendelea ndani ya Kenya inapoitwa Hifadhi ya Masai Mara.
Kuna idadi kubwa ya wanyamapori. Serengeti pamoja na Masai Mara inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aina nyingi nyingine za wanyama, kati yao "watano wakubwa" wanaovuta watalii hasa yaani tembo, simba, chui, fisi, kifaru na nyati.
Eneo la hifadhi ya Ngorongoro liliwahi kuwa sehemu ya Serengeti hadi kutengwa kama hifadhi ya pekee. Bonde la Olduvai ambako mabaki ya zamadamu yalipatikana liko ndani ya Serengeti.
Mazingira ya Serengeti ni kanda ya kijiografia katika kaskazini-magharibi mwa Tanzania na inaenea kusini-magharibi mwa Kenya kati ya latitude 1 na 3 Kusini na longitude 34 na 36 Mashariki. Inaenea kiwango cha mraba kilometa 30,000 2.
Serengeti ina gura/uhamiaji ya wanyama kwenye ardhi kubwa na ndefu zaidi duniani,[1] ambao hua ni tukio wa nusu mwaka . Uhamiaji huo ni moja ya maajabu kumi ya asili ya ulimwengu ya kusafiri.
Kanda hii ina hifadhi za taifa na hifadhi mchezo kadhaa. Jina Serengeti limechukuliwa kutoka lugha ya Kimasai hasa, "Serengit" kumaanisha "Kiwara kisichoisha". [2] [3]
Inakadiriwa mamalia 70 kubwa na baadhi ya spishi 500 avifauna (yaani ndege) hupatikana huko. Tofauti hii ya juu upande wa spishi ni shughuli makazi mbalimbali kuanzia misitu ya riverine, mabwawa, kopjes mbuga na misitu. [4] Nyumbu bluu, swara, punda milia na nyati ni baadhi ya mamalia kubwa ambao kwa kawaida hupatikana katika kanda hii.
Karibu Oktoba, karibu wanyama wanaokula majani (si nyama) milioni 2 husafiri kutoka milima ya kaskazini kuelekea nyanda za kusini na kuvuka mto wa Mara katika harakati za mvua. Katika mwezi Aprili, wao hurejea kaskazini kwa kupitia magharibi, na kwa mara nyingine tena kuvuka Mto wa Mara. Jambo hili la mara kwa mara huitwa kwa Kiingereza "Circular migration" yaani uhamiaji mviringo. Nyumbu zaidi ya 250,000 pekee watakufa safarini kutoka Tanzania kwenda katika mbuga ya wanyama ya Masai Mara huko Kenya pande za juu, ambayo ni jumla ya maili 500. Kifo mara nyingi unasababishwa na maudhi au uchovu. [1] Uhamiaji huu umeonyeshwa katika filamu na programu nyingi za televisheni kote duniani.
Historia
Mvulana wa kimaasai (Moran au askari) anatembea ndani ya Serengeti na miinuko ya Ngorongoro iko nyuma.
Wamasai walijulikana kama shujaa wakali, na waliishi pamoja na wanyamapori huku wakila mifugo yao pekee.
Nguvu zao na sifa zilisababisha wasafiri kutoka Ulaya kutotumia wanyama na rasilimali ya nchi yao vibaya.
Janga la "rinderpest" na ukame wakati wa 1890 ulisababisha kupungua kwa idadi ya Wamasai na wanyama. Uwindaji haramu wa wanyamapori na ukosefu wa moto, ambayo yalikuwa matokeo ya shughuli za binadamu, yaliweka hatua ya maendeleo ya misitu na vichaka kwa miaka 30-50 ijayo.
Uongezekaji wa chafuo sasa ulisababisha kutokuwa kwa makazi ya binadamu katika eneo hili.
Moto, tembo, na nyumbu walikuwa na ushawishi mkubwa katika kuamua sasa muundo wa Serengeti. [5]
Mnamo miaka ya 1960, idadi ya binadamu ilivyoongezeka, moto, aidha kuwashwa kwa makusudi na Wamaasai ili kuongeza eneo ya malisho ya mifugo, au kwa ajali, ulisababisha kuchomeka kwa miche mipya ya miti.
Mvua nzito ilichangia ukuaji wa majani, ambao ulikuwa kama mafuta kwa moto wakati wa misimu mikavu ifuatayo. Miti mizee ya Acacia, ambayo huishi tu miaka 60-70, ilianza kufa. Awali tembo, ambao hula miti michanga na mizee, walilaumiwa kwa kumaliza misitu. Lakini majaribio yalionyesha kulikuwa na sababu nyingine muhimu zaidi. Wakati huo huo, idadi ya tembo ilipunguzwa kutoka 2,460 mwaka 1970 hadi 467 katika mwaka 1986 kutokana na uwindaji haramu. [6]
Mnamo miaka ya 1970 idadi ya nyumbu na nyati wa Afrika ilikuwa imeongezeka, na walikuwa wakipunguza idadi ya majani kwa kasi, na kusababisha upungufu wa mafuta ya kusambazaa moto. [7] kupunguka kwa ukali wa moto umesababisha Acacia kuwa imara tena. [5]
Hifadhi ya mazingira
Bara la Maasai lina mbuga ya wanyama bora zaidi Afrika Mashariki. [8] Serikali za Tanzania na Kenya hutunza idadi kadhaa ya maeneo yaliyochunwa: mbuga, maeneo ya hifadhi, mapori ya akiba, n.k., ambayo hutoa ulinzi wa kisheria kwa zaidi ya 80% ya Serengeti. [9]Ol Doinyo Lengai, ikiwapo volkeno hai katika eneo la Serengeti, ni mlima wa moto pekee ambao bado hutoa "carbonatite lava". "Carbonatite lava", unapofichuliwa kutoka kwa hewa, hubadilisha rangi kutoka samawati hadi nyeusi na kufanana na "washing soda". Tabaka zito la jivu linaweza kugeuka kuwa hardpan iliotajirika na kalsiamu ngumu kama saruji baada ya kunyeshewa. Mizizi ya mti haiwezi kupenya safu hii, na kimsingi tambarare bila miti ya Serengeti, ambayo iko magharibi na upepo chini ya Ol Doinyo Lengai, ni matokeo. [10]
Miinuko ya mwamba, au "koppes", katika tambarare ya Serengeti.
Baadhi ya 70 km magharibi, misitu ya Acacia huonekana ghafla na kunyoosha magharibi kuelekea ziwa Victoria na kaskazini kuelekea katika tambarare za Loita, kaskazini mwa mbuga ya wanyama ya kitaifa ya Maasai Mara. Aina 16 tofauti ya Acacia zipo katika msitu huu, usambazaji wake ukiamuliwa na hali "edaphic" na urefu wa udongo.
Karibu na Ziwa Victoria kuna tambarare yenye mafuriko yaliyotokana na "lakebeds" za kale. Katika kaskazini magharibi, misitu ya Acacia imebadilishwa na misitu ya "Terminalia-Combretum" yenye majani mapana, uliodhamiria kutokana na mabadiliko katika jiolojia. Eneo hili lina kiwango cha juu zaidi cha mvua katika mfumo na huunda kimbilio kwa wanyama wanaohama mwisho wa msimu wa kiangazi. [11]
Mwinuko katika Serengeti huanzia mita 920 hadi 1850 na joto wastani kuanzia digrii 15 hadi digrii 25 "Celsius". Ingawa kwa kawaida hali ya hewa huwa ya joto na kavu, mvua hutokea katika misimu miwili ya mvua: Machi-Mei, na msimu mfupi katika Oktoba na Novemba. Kiasi cha mvua inatofautiana kutoka kiwango cha chini cha 508 mm katika upande wa "lee" ya miinuko ya Ngorongoro na kiwango cha juu cha 1,200 mm katika pwani ya Ziwa Victoria. [12] Nyanda za juu, ambazo ni baridi kuliko tambarare na kufunikwa na misitu ya "montane", ndiyo alama ya mpaka wa mashariki ya bonde ambayo Serengeti uko.
Tambarare wazi ya Serengeti ina miinuko ya "granite" inayojulikana kama "koppes". Miinuko hiyo ni matokeo ya volkeno. "Koppies" hutoa makazi madogo kwa nyanda zisizo wanyamapori. "Koppe" moja inayoweza kuonekana kwa wageni huko Serengeti ni Simba Koppe (Lion Koppe). Serengeti ilitumika kama jukwaa kutengeneza filamu ya "Disney" ya The Lion King na baadaye uvumbuaji wa filamu za jukwaa.
Eneo hilo pia ni nyumbani kwa eneo lililohifadhiwa la Ngorongoro ambalo lina "Olduvai Gorge", ambapo baadhi ya "hominid fossils" kongwe hupatikana, vilevile pia "Ngorongoro Crater", caldera ya volkeno kubwa zaidi ulimwenguni.
.
Boko Haram ‘wameua watu 380’ Cameroon

Shirika
la kutetea haki za kibinadamu la Amnesty International limesema raia
380 wameuawa na wapiganaji wa Boko Haram kaskazini mwa Cameroon mwaka
huu.
Ripoti iliyotolewa leo na shirika hilo inasema kuna wanajeshi
kadha waliouawa na wapiganaji hao ambao wamelazimisha watu 80,000
kutoroka makwao.Wanajeshi na polisi wa Cameroon nao wanadaiwa kujibu mashambulio ya kundi hilo kwa kuwakamata watu zaidi ya 1,000, wengi wao vijana.
Ripoti hiyo kwa jina "Cameroon human rights under fire", inasema baadhi ya waliokamatwa na maafisa wa usalama wameuawa au kufariki kutokana na hali mbaya gerezani, hasa katika mji wa Maroua.
Shirika hilo linasema watu 200 waliokamatwa na maafisa wa usalama kwenye operesheni Desemba kwa sasa hawajulikani waliko.
Amnesty wanaamini Cameroon inaweza kujifunza mengi kutokana na makosa yaliyofanywa na taifa jirani la Nigeria ambako wanajeshi wametuhumiwa kutekeleza dhuluma dhidi ya raia kwa muda mrefu.
Kundi hilo linasema yaliyotokea Nigeria yanaonyesha kukosa kuheshimu haki za kibinadamu na sheria za kimataifa kuhudu ubinadamu katika vita dhidi ya Boko Haram kuna madhara makubwa.
Katika kisa kimoja kaskazini mwa Cameroon, shirika hilo la haki za kibinadamu linasema maafisa wa usalama walishambulia shule za Kiislamu ambazo ziliaminika kuwa kambi za mafunzo za Boko Haram.
Watoto 84 na wanaume zaidi ya 43, wakiwemo walimu wengi, walizuiliwa kwa miezi sita bila kufunguliwa mashtaka, shirika hilo linasema.
Katika visa vingine, wanajeshi wa Cameroon wanadaiwa kupora mali na kuteketeza nyumba za watu.
chanzo BBC
Umoja mataifa yahofia Burundi kuingia tena kwenye mzozo
Pablo de Greiff, mchunguzi maalum wa umoja mataifa kwa ukiukaji mkubwa, anasema mengi yametokea tangu alipoitembelea Burundi mwezi December, na hamna lilo zuri. Anasema ,Burundi imejiondoa kwenye njia ya amani ambayo imeifuata tangu mwaka 2000, pale makubaliano ya Arusha yalipomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Anasema serikali ya rais Pierre Nkuruzinza haijaribu tena kujenga jamii kutokana na kanuni za sheria, na kwamba utamaduni wa kutokhifia kushtakiwa kutoka miongo iliyopita umejikita zaidi na unatumiwa kama nyenzo ya ukandamizaji na ghasia.
De Greiff anasema amewasilisha wasiwasi wake kwa baraza la haki za binadam la umoja mataifa kwa matarajio nchi kuwa nchi wanachama watafahamu ukubwa wa hali inayojitokeza nchini Burundi na kuchukuwa hatua ili kuepuka janga kutokea.
De Grieff anasema, anataka kuwa muwazi, na kujaribu kutowa wito wa haraka na wito wa tahadhari kwa jumuiya ya kimataifa, wasisubiri hadi tufikwe na janga jingine mikononi mwetu kabla ya kuchukuwa hatua.
Takriban watu laki 3 waliuwawa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi.
Taifa hilo lilikuwa na Amani katika miaka ya karibuni hadi mwishoni mwa mwezi Aprili, pale rais Nkuruzinza alipotangaza kuwania muhula wa tatu madarakani. Tangu wakati huo, De Greiff anasema, kumekuwepo na Zaidi ya mauwaji mia 1, mamia ya ukamataji holela na kesi nyingi za mateso na kutendewa vibaya.
Anasema hamna kesi inayochunguzwa ila moja inayohusisha afisa wa serikali.
Rais alichaguliwa tena mwezi July, lakini mivutano bado ipo baina ya wafuasi wake na wale wanaosema amekiuka katiba ambayo imeweka kiwango cha mihula miwili tu kwa rais kuwepo madarakani.
Mchunguzi huyo wa umoja mataifa anasema jumuiya ya kimataifa na serikali za kikanda haziwezi kumudu kukaa na kusubiri ukatili mpya utokee tena nchini Burundi. Anaonya kuwa hii inahatarisha mzozo mkubwa kuweza kutokea katika eneo la maziwa makuu, na matokeo ambayo yanatisha na yasiyojulikana
Papa Francis kutembelea Kenya na Uganda
Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis atatembelea Kenya Novemba 25 kabla ya kuelekea Uganda siku mbili baadaye.
Mwezi Juni kiongozi huyo mzaliwa wa Argentina alieleza kikao cha makasisi kutoka kote ulimwenguni kuwa alikusudia kufanya ziara yake ya kwanza barani Afrika kwa kutembelea Kenya ingawaje ziara hiyo haikuwa imedhibitishwa wakati huo kutokana na matatizo ya kimipango.
Papa Francis hakufafanua matatizo hayo lakini alikuwa akizungumza miezi miwili baada ya kundi la wanamgambo kutoka Somalia la Al-Shabaab kushambulia wakristo kwenye chuo kikuu karibu na mji wa Garissa ambapo wanafunzi 148 waliuwawa. Nchi ya Kenya imeshuhudia mashambulizi ya kigaidi ya mara kwa mara kutoka wanamgambo wa Al-Shaabab..
chanzo sauti ya amerika
Serikali ya Kenya yalaumiwa kufanya ukiukaji wa haki za binadamu
Tume ilisema katika ripoti mpya ya Jumanne kwamba ukiukaji wa haki za binadamu umesambaa na uliratibiwa vyema. Wachunguzi wanasema waliambiwa kwenye kesi mbali mbali za washukiwa kwamba walikamatwa kiholela na kuwekwa jela kuanzia saa kadhaa hadi siku nyingi katika hali ya msongamano mkubwa na hali duni.
Kuna shutuma za mateso, kupigwa, kumwagiwa maji na kuchomwa na nyaya za umeme. Baadhi ya washukiwa walining’inizwa kwenye miti na wengine waliachwa wakang’atwe na wadudu.
Ripoti hiyo ilisema watu wenye asili ya kisomali na waislam wamekuwa walengwa wakubwa. Familia zinatafuta taarifa juu ya kupotea kwa jamaa zao na wanapata msaada kidogo kutoka kwa maafisa.
Tume hiyo ilisema huku ikitambua changamoto kubwa zinazoikabili serikali ya Kenya katika kupambana na msimamo mkali na ugaidi, lazima hilo lifanyike kisheria na kulingana na viwango vinavyokubalika ulimwenguni vya haki za binadamu.
Maafisa wa Kenya bado hawajajibu lolote juu ya ripoti hiyo.
chanzo,sauti ya amerika
Wanakoishi matajiri wakubwa wa Kiafrika
Afrika Kusini
Nchi ya Kiafrika iliyo na idadi kubwa kabisa ya mamilionea ni Afrika Kusini. Kuna matajiri wa hali ya juu 46,800 wanoishi baina ya miji ya Cape Town na Johannesburg - na bado wanatarajiwa kuengezeka. Ikilinganishwa idadi hiyo na barani Ulaya, nchini Uingereza kwa sasa kuna mamilionea 840,000.Wahamiaji wapata njia mpya Croatia

Kundi la kwanza la
wahamiaji limewasili nchini Croatia ,ambayo ni njia mpya ya kuelekea
mataifa ya Ulaya yaliopo kaskazini ,siku moja baada ya Hungary kufunga
mpaka wake na Serbia.
Takriban wahamiaji 150 walivuka na kuingia katika mataifa ya muungano wa Ulaya kutoka Serbia.Croatia inasema kuwa iko tayari kuwapokea moja kwa moja ama kuwaelekeza kule wanakotaka kwenda.
Wahamiaji wengi kutoka Syria wana matumaini ya kuelekea Ujerumani.
Muswaada wa kupinga ushoga kusainiwa Uganda
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema atasaini muswaada tata unaopinga ushoga na kuwa sheria kamili.
Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni onyo kwa wanaotetea vitendo vya mahusiano ya jinsia moja kuwa watashughulikiwa vikali nchini humo.
Mwezi uliopita kiongozi huyo alipanga kuachana na muswaada huo ambao umekuwa ukikosolewa vikali na wahisani kutoka mataifa ya Magharibi na wanaharakati wa haki za binaadamu tangu ulipowasilishwa mwaka 2009. Mapenzi ya jinsia moja ni mwiko katika mataifa ya Afrika na kinyume cha sheria kwa mataifa 37.
Wasiwasi wa mashoga wa Afrika
Wanaharakati wa haki za binaadamu wanasema Waafrika wachache waliojitangaza kuwa mashoga, wanahofu ya kufungwa, kukabiliwa na vurugu na kupoteza ajira zao.
Wakati wa mkutano wake na chama tawala nchini Uganda NRM kundi la wanasayasi liliwasilisha utafiti wao kuhusu mapenzi ya jinsia moja kwa rais Museveni. Msemaji wa mkutano huo, wa NRA Anite Evelyn katika taarifa yake alisema kuwa "Museveni alitangaza atasaini muswaada huo kwa vile swali lile la iwapo mtu anaweza kuzaliwa shoga au hapana limejibiwa".
Uchunguzi wa mawaziri
Katika taarifa yake kamati ya mawaziri iliyokuwa ikilifanyia uchunguzi suala hilo ilisema Ijumaa (14.02.2014) hakuna vinasaba vya mapenzi ya jinsia moja na kwa hivyo si ugonjwa lakini ni tabia isiyo ya kawaida ambapo mtu anaweza kujifunza tu kwa kupitia uzoefu katika maisha.
Katika mkutano na chama tawala cha NRM, Mshauri wa Rais katika masuala ya Kisayansi, Dokta Richard Tushemereirwe alimwambia kwamba "mapenzi ya jinsia moja yana athari kubwa kwa afya za watu kwa hivyo si jambo la kuachwa liendelee hata kidogo".
Muswaada wa kupinga uhusiano wa jinsia moja uliwasilishwa bungeni mwaka 2009, ambapo awali ulikuwa ukipendekeza adhabu ya kifo kwa wanaoshiriki vitendo vya ngono kwa watu wa jinisia moja, lakini ukafanyiwa marekebisho kwa kuweka adhabu ya vifungo vya awamu gerezani na maisha kwa kile kilichotajwa kuwa mapenzi ya jinsia moja ya kuchochewa.
Rais Museveni alisisitiza kuwa , wahamasishaji, wanaojionesha na wote wanaoshiriki vitendo vya ngono kwa watu wa jinsia moja kwa sababu za ukaidi wa kutumwa , hawatavumiliwa na watakabiliwa vikali.
chanzo,idhaa ya kiswahili ya sauti ya ujerumani

Makundi ya mgambo yatishia amani Uganda
Ikiwa imesalia miezi mitano kuelekea uchaguzi mkuu nchini Uganda,
taarifa zimeenea kuhusu kuundwa kwa makundi ya vijana wanaoandaliwa
kufanya vurugu, hali hii imevishtua vyombo vya usalama nchini humo.
Wapigakura nchini Uganda watakwenda vituoni mwezi Februari kumchagua
rais pamoja na wabunge, uchaguzi ambao matokeo yake yanajulikana. Rais
wa sasa Yoweri Museveni, alieko madarakani kwa karibu miaka 30 sasa,
anaamini kuwa nchi yake bado inamhitaji ili kuiletea maedeleo ya
kiuchumi na tayari ametangaza kugombea tena wadhifa huo. Upande wa
upinzani yuko Kizza Besigye ambaye tangu mwaka 2001 amekuwa mpinzani
mkuu wa Museveni.
Lakini hali ni ya wasiwasi kuelekea uchaguzi huo, na hofu inazidi kutanda kuhusu uwezekano wa kutokea vurugu katika uchaguzi huo. Katika siku za karibuni kumekuwa na taarifa kwamba chama tawala - NRM kimekuwa kikitoa mafunzo ya mgambo kwa kundi la vijana, mhusika mkuu wa kundi akiwa mshauri wa rais na afisa wa zamani wa jeshi Meja Roland Kakooza Mutale, ambaye anaelezwa kuwa kiongozi wa kundi la vijana wapatao 500, walioendesha vurugu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2006.
NRM yamkana Kakooza Mutale
Chama tawala cha NRM kimekanusha kuhusika kwa vyovyote vile na harakati za Mutale. Katika mahojiano na DW, waziri wa mawasiliano wa Uganda Jim Muhwezi, alisema sheria laazima izingatiwe, na kwamba yeyote anaekwenda kinyume atawajibishwa kisheria, na kuongeza kuwa vipo vyombo vya dola vya kutosha kushughulikia masuala ya usalama wakati wa kipindi cha uchaguzi mkuu.
Baada ya picha za kambi ya mafunzo ya Kakooza Mutale kuonyeshwa kwenye televisheni nchini Uganda, wanasiasa wa upinzani walionyesha ghadhabu. Lakini mwanasiasa wa chama cha upinzani cha Democratic DP, Erias Lukwago ambaye pia ni meya wa jiji la Kampala, hakutaka mambo yaishie hapo tu. Naye alianzisha kundi lake la vijana alillolitaja kama kundi lao la kujihami na kuiambia DW kuwa maisha yao yalikuwa hatarini.
Matukio hayo yamezusha hasira miongoni mwa raia wa Uganda, na hofu inazidi kuongezeka kwamba makundi hayo huenda yakaitumbukiza nchi katika machafuko. Kutokana na hali hiyo, polisi imewaita Mutale na Lukwago kuwahoji na msemaji wa jeshi la polisi Fred Enanga alitahadharisha kuwa yeyote mwenye mpango wa kuunda makundi kama hayo atawajibishwa.
Zipo fununu pia kuwa waziri mkuu wa zamani na mshirika wa rais wa rais Yoweri Museveni Amama Mbabazi, anapanga kuanzisha kundi lake la mgambo. Mbabazi alifukuzwa kutoka chama cha NRM mwishoni mwa mwezi Julai kufuatia mzozo wa ndani kuhusu uteuzi wa mgombea urais, na sasa anataka kusimama kama mgombea binafsi. Mwanasheria huyo ni miongoni mwa wanasiasa wenye mvuto nchini Uganda, na wangalizi wanasema anaweza kutoa upinzani mkali kwa rais Museveni katika uchaguzi wa Februari.
Viongozi wa dini watahadharisha
Wakati huo, baraza la viongozi wa dini nchini Uganda limejiunga pia na mjadala huo. Wajumbe wa baraza hilo wamewatolea wito wanasiasa kuzuwia kuibuka kwa makundi ya wanamgambo. Mufti Mkuu Sheikh Shaban Mubajje aliwaonya katika taarifa ya wawakilishi wa baraza hilo kuwa makundi hayo ni hatari kwa mustakabali wa taifa, na kulitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua kali wote wanaohusika na uanzishwaji wa makundi hayo.
Uundwaji wa makundi ya vurugu kuelekea uchaguzi nchini Uganda ni utamaduni unaozidi kukita mizizi. Mwaka 2011, polisi ilisema kulikwepo na makundi saba ya wanamgambo yaliyojipa yenyewe jukumu la kutoa ulinzi, lakini polisi ilifanikiwa kuyavunja makundi hayo kabla ya uchaguzi. Inahofiwa kuwa vurugu zinaweza kutokea, ikiwa mamlaka hazitachukuwa hatua za haraka kushughulikia tatizo hilo.

Merkel aliyasema hayo katika mkutano wa pamoja na kansela wa Austria
Werner Faymann mjini Berlin siku ya Jumanne, huku Hungary ikitangaza
hali ya hatari na kufunga mpaka wake na Serbia kuzuwia mmiminiko wa
wakimbizi zaidi.
Amesema Ulaya iko katika hali ngumu sana, na kuutaja mgogoro wa wakimbizi kuwa ndiyo changamoto kubwa zaidi iliyoukumba umoja wa ulaya katika kipindi cha miongo kadhaa, huku akisisitiza kuwa changamoto hiyo itatatuliwa tu kwa matazamo sawa.
"Hili ni tatizo na Ulaya nzima na linaweza tu kutatuliwa kwa ushirikiano wa mataifa yote ya Umoja wa Ulaya. Ni jukumu la umoja wote wa Ulaya na ndiyo maana tumekubaliana kuwa na mkutano maalumu wa kilele wa Umoja wa Ulaya wiki ijayo," alisema Merkel.
Wakimbizi wakisota nje ya mpaka wa Hungary na Serbia, baada ya
Hungary kukamilisha uzio wa nyenyenge kuwazuwia kukanyaga ardhi yake.
Ujerumani na Austria zilirejesha ukaguzi wa mipakani wiki hii kupunguza
mtiririko wa wakimbizi wanaowasili kutoka Hungary, ambayo leo nayo
imetangaza hatua za dharura kuwazuwia wahamiaji kuvuka mpaka wake na
Serbia, ambako imekamilisha ujenzi wa uzio.
Ukaguzi kuendelea
Merkel amesema ukaguzi wa mipakani, ambao kimsingi unasitisha mkataba wa Schengeni kuhusu uhuru wa kusafiri katika mataifa 26 ya Ulaya, vitaendelea kuwepo hadi usalama urejeshwe. Serikali ya Ujerumani ilitangaza kurejesha kwa udhibiti wa mipakani siku ya Jumapili, baada ya maafisa kulalamika kuwa hawawezi tena kumudu mmiminiko wa wakimbizi, ambao ulivunja rekodi mwishoni mwa wiki.
Naibu Kansela Sigmar Gabriel, amesema leo kuwa Ulaya imejidhalilisha baada ya mawaziri wa mambo ya ndani kushindwa kufikia muafaka kuhusu mpango wa mgawanyo wa wakimbizi wapatao 120,000, na kusema mataifa ya Umoja wa Ulaya yanapaswa kufahamu kuwa Ulaya iko hatarini, na kwamba kinachoshuhudiwa hivi sasa kinalitishia bara hilo kuliko hata mgogoro wa madeni ya Ugiriki.
Gabriel pia amesema Umoja wa Ulaya unapaswa kuzingatia shinikizo la kifedha kwa mataifa yanayokataa kuwapokea wakimbizi.
"Ni wazi kuwa tusipofikia makubaliano, mipango w amuda wa kati ya Ulaya haitokuwa chochote zaidi ya moshi na vioo. Ujerumani haitakuwa tayari kuwa mlipaji mkuu wa Ulaya," alisema naibu huyo wa Merkel na kuongeza kuwa "kila mtu anashiriki wakipata pesa, lakini hakuna anaeshiriki linapokuja suala la kuwajibika. Huo ndiyo utakuwa mwisho wa msingi wa ufadhili ikiwa hali hii itaendelea."
Czech, Slovakia zaibeza Ujerumani
Matumaini ya kufikiwa muafaka wa kugawana wakimbizi 120,000 kutoka mataifa yaliyozidiwa ya Ugiriki, Italia na Hungary, miongoni mwa mataifa yote wanachama wa Umoja wa Ulaya, yalififia siku ya Jumatano kutokana na upinzani mkali kutoka kwa Hungary yenyewe, Jamhuri ya Czech, Slovakia na Romania.
Lakini afisa wa serikali ya Jamhuri ya Czech ameikosoa Ujerumani kwa kile alichosema ni kutoa vitisho visivyo na mashiko, huku Slovakia ikisema ikiwa vitisho hivyo vitatekelezwa basi huo ndiyo utakuwa miwsho wa Umoja wa Ulaya.
Serikali ya mrengo mkali wa kulia nchini Hungary, imefunga njia kuu ya kuingilia wakimbizi kutoka nchini jirani ya Serbia leo, kukataa maobi 16 ya hifadhi, huku watu 171 wakiripotiwa kukamatwa wakati wanajaribu kuvuka mpaka kinyume na sheria.
Wakati huo huo, Uswisi imesema itakubali viwango vya mgawanyo wa wakimbizi vilivyopendekezwa na Umoja wa Ulaya, amesema rais wake Simonetta Sommaruga, huku rais wa Slovenia Borut Pahor naye akielezea kuunga mkono mpango huo, huku akisema mgogoro wa wakimbizi unaweza kuwa changamoto kubwa zaidi kwa Umoja wa Ulaya kuliko mgogor wa kifedha uliyoanza mwaka 2008,
Idhaa ya kiswahili ya sauti ya ujerumani
Amesema Ulaya iko katika hali ngumu sana, na kuutaja mgogoro wa wakimbizi kuwa ndiyo changamoto kubwa zaidi iliyoukumba umoja wa ulaya katika kipindi cha miongo kadhaa, huku akisisitiza kuwa changamoto hiyo itatatuliwa tu kwa matazamo sawa.
"Hili ni tatizo na Ulaya nzima na linaweza tu kutatuliwa kwa ushirikiano wa mataifa yote ya Umoja wa Ulaya. Ni jukumu la umoja wote wa Ulaya na ndiyo maana tumekubaliana kuwa na mkutano maalumu wa kilele wa Umoja wa Ulaya wiki ijayo," alisema Merkel.

Ukaguzi kuendelea
Merkel amesema ukaguzi wa mipakani, ambao kimsingi unasitisha mkataba wa Schengeni kuhusu uhuru wa kusafiri katika mataifa 26 ya Ulaya, vitaendelea kuwepo hadi usalama urejeshwe. Serikali ya Ujerumani ilitangaza kurejesha kwa udhibiti wa mipakani siku ya Jumapili, baada ya maafisa kulalamika kuwa hawawezi tena kumudu mmiminiko wa wakimbizi, ambao ulivunja rekodi mwishoni mwa wiki.
Naibu Kansela Sigmar Gabriel, amesema leo kuwa Ulaya imejidhalilisha baada ya mawaziri wa mambo ya ndani kushindwa kufikia muafaka kuhusu mpango wa mgawanyo wa wakimbizi wapatao 120,000, na kusema mataifa ya Umoja wa Ulaya yanapaswa kufahamu kuwa Ulaya iko hatarini, na kwamba kinachoshuhudiwa hivi sasa kinalitishia bara hilo kuliko hata mgogoro wa madeni ya Ugiriki.
Gabriel pia amesema Umoja wa Ulaya unapaswa kuzingatia shinikizo la kifedha kwa mataifa yanayokataa kuwapokea wakimbizi.
"Ni wazi kuwa tusipofikia makubaliano, mipango w amuda wa kati ya Ulaya haitokuwa chochote zaidi ya moshi na vioo. Ujerumani haitakuwa tayari kuwa mlipaji mkuu wa Ulaya," alisema naibu huyo wa Merkel na kuongeza kuwa "kila mtu anashiriki wakipata pesa, lakini hakuna anaeshiriki linapokuja suala la kuwajibika. Huo ndiyo utakuwa mwisho wa msingi wa ufadhili ikiwa hali hii itaendelea."
Czech, Slovakia zaibeza Ujerumani
Matumaini ya kufikiwa muafaka wa kugawana wakimbizi 120,000 kutoka mataifa yaliyozidiwa ya Ugiriki, Italia na Hungary, miongoni mwa mataifa yote wanachama wa Umoja wa Ulaya, yalififia siku ya Jumatano kutokana na upinzani mkali kutoka kwa Hungary yenyewe, Jamhuri ya Czech, Slovakia na Romania.
Lakini afisa wa serikali ya Jamhuri ya Czech ameikosoa Ujerumani kwa kile alichosema ni kutoa vitisho visivyo na mashiko, huku Slovakia ikisema ikiwa vitisho hivyo vitatekelezwa basi huo ndiyo utakuwa miwsho wa Umoja wa Ulaya.
Serikali ya mrengo mkali wa kulia nchini Hungary, imefunga njia kuu ya kuingilia wakimbizi kutoka nchini jirani ya Serbia leo, kukataa maobi 16 ya hifadhi, huku watu 171 wakiripotiwa kukamatwa wakati wanajaribu kuvuka mpaka kinyume na sheria.
Wakati huo huo, Uswisi imesema itakubali viwango vya mgawanyo wa wakimbizi vilivyopendekezwa na Umoja wa Ulaya, amesema rais wake Simonetta Sommaruga, huku rais wa Slovenia Borut Pahor naye akielezea kuunga mkono mpango huo, huku akisema mgogoro wa wakimbizi unaweza kuwa changamoto kubwa zaidi kwa Umoja wa Ulaya kuliko mgogor wa kifedha uliyoanza mwaka 2008,
Idhaa ya kiswahili ya sauti ya ujerumani
Thursday, September 3, 2015
SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE (Sehemu ya II)
Majuzi tuliona jinsi Wenge kuanzia Mwanzo ilivyoaanza mpaka ilipofikia kumeguka kwa JB Mpiana na Werason (Kama uliikosa bofya hapa), Leo hii tunaanza kuiangalai Wenge BCBG ya JB Mpiana. Endelea…
Shukrani za kipekee kwa Hadji Le Jbnique kwa kukokotoa na kutohoa habari hii mpaka leo unaisoma wewe, Respect Grand Rapids nakati ya USA.
Adolph Dominguez, Blaise Bulla, Werrason, Didie Masela na Allain Makaba
walikuja kushtuka na kugundua Kina werra hawako nao tena wenge ilipopata contract kwa jitihada za SIPE kwenda kutumbuiza Ulaya Katika ukumbi wa BATACLAN,Paris na wakati huo huo kuitumia nafasi hiyo kwenye kufanya album ya TITANIC huko huko Paris
Wenge BCBG ilizaliwa JB Mpiana akiwa kiongozi wa
bendi,Blaize Bula akiwa Chef d’orchestre,Alain “Prince” Makaba akiwa
artistic Director na SIMON SIPE akiwa producer. Waimbaji wakiwa JB
mwenyewe, Alain Mpela, Aimelia Lyase Demingongo na Blaize Bula, wapiga
guitar Alain Makaba,Burkinafaso Mbokalia na Japonais(solo &
rhythm),Patient Kusangila(rhythm & Bass), Titina(Drums), Ali Mbonda,
Seguin Mignon(Tumba), Theo Bidens (keyboard), na Powerful AtalakUs toka
kwao Roberto Ekokota “Le Grand Chibuta na Tutu Caluggi.
Kundi la Wenge Musica BCBG 1987, Kwenye Mic ni Werrason na JB Mpiana, Picha na Wikipedia
Mwanzoni wanamuziki wengi wa kawaida kundini humo
akiwemo Alain Mpela ambae amekiri walikua hawajui kinachoendelea walikua
wakidhani bado ni wenge musica ileile moja kwa kuwa mpaka nyimbo za
album ya TITANIC walizifanyia mazoezi pamoja (nadhani ndio maana hata
tukisikiliza kwa makini TITANIC na FORCE INTERVENTION RAPIDE zinavyoanza
ni kama zinafanana)na kwa wenge walivyokuwa wanafanya kazi,ilikua ni
kawaida kwao wakati mwingine kupiga show hasa local wakiwa
hawajakamilika wote,sometimes wanaweza kuwepo wote akamiss labda makaba
na blaize bula au hao wakawepo akamiss werrason, au wote wakawepo
akamiss JB,
Hivyo basi kitendo cha werra,adolphe na didier masela
hakikuwashangaza na kuwafanya wahisi labda kuna mgawanyiko wa bendi
tayari,wakajua ni utamaduni wa wenge wa kawaida si unajua mastaa wakiwa
kundi moja tena,japo walikua wanajua mitafaruku imekuwa ikiendelea mara
kwa mara katika maisha ya wenge lakini si yakufikia kuzigawa bendi.
Lakini walikuja kushtuka na kugundua Kina werra
hawako nao tena wenge ilipopata contract kwa jitihada za SIPE kwenda
kutumbuiza Ulaya Katika ukumbi wa BATACLAN,Paris na wakati huo huo
kuitumia nafasi hiyo kwenye kufanya album ya TITANIC huko huko
Paris.,ndipo katika hali isiyo ya kawaida wakiwa na katika maandalizi ya
ziara hiyo ambayo hupewa kipaumbele sana na wanamuziki wa congo wakawa
wanashangaa mbona jamaa hawaonekani hata mazoezini wakati kuna safari
nzito kama hiyo!na ilikua ni katika kipandi hicho hicho pia ambapo Ali
Mbonda akaingia kwenye historia ya kuwa mwanamuziki wa kwanza kuitosa
bendi mpya ya WENGE BCBG kwenda kwa kina WERRASON baada ya jina lake
kutokuwemo kwenye trip nyeti kama hiyo huku jina la msaidizi wake
chipukizi wakati huo katika kupiga mbonda (tumba) Seguin Mignon
likichukua nafasi yake(Seguin sasa hivi ndio mpiga drums namba moja wa
BCBG).
Kwa hiyo hiyo ndio ikawa safari yao ya kwanza ulaya
bila kina werrason,wakapiga show hiyo hapo chini kama wanavyoonekana
huku wakihitajika kutoa maelezo ya kina kwa mashabiki kuwaeleza
kilichotokea huko nyumbani Kinshasa na kupelekea kujiweka pembeni na
wenzao(werra,adolphe na masela),Ekokota yupo kundini hapo anaonekana
akifanya kazi na Tutu Caludji “no.1”.
na
Baada ya Ali Mbonda kujiondoa kundini baada ya
kukerwa na kutojumuishwa kwenye safari ya ulaya jambo ambalo limekua la
kawaida mno kwa Ali na wanamuziki wengi offcourse wa congo wanapokosa
kuwemo kwenye tour za Ulaya,Mtu wa pili kujiondoa BCBG akawa ROBERTO
EKOKOTA mara baada ya concert hiyo ya BATACLAN hapo juu aliamua
kupumzika kutokana na matatizo ya kiafya hali iliyomfanya ashindwe hata
kuweka Atalaku zake kwenye album ya TITANIC na kumuacha Tutu Caludji
amalize kila kitu mwenyewe,ndio vile tunaisikia TITANIC mpaka leo,pale
ni bila le Grand Chibuta Ekokota,angeshiriki sijui ingekuwaje,mi sijui
tuwaachie wenyewe!.
Baada ya kumaliza recording ya TITANIC walirejea
nyumbani congo wakimuacha Alain Makaba huko ulaya kwake ambako alishakua
amehamia. Walipofika Congo wakawakuta kina werrason ndio
wameshaitengeneza bendi yao wanajiandaa Force Intervention Rapide(Lakini
walikua bado hawajaipa hilo jina, maana nalo lina hadithi yake halikuja
tu kama mvua),Baada ya mapumziko mafupi ya safari ya ulaya kazi ikaanza
kwa Chef d’Orchestre Blaize Bulla Kuanza kutafuta vijana wa kuwa
recruit. Hapa walihitaji mpiga bass yani pure bassist atakaeziba pengo
la Didier Masela badala ya kumtegemea Patien Kusangila ambae kiasili
alikua ni mtu wa rhythm guitar,pia walihitaji atalaku ataeziba pengo la
Ekokota,kwa upande wa bass Blaize Bulla akaanza kumchokonoa Koffi kwa
kuvamia ngome yake na kufanikiwa kumshawishi Sunda Bass ambae hata hivyo
hakua na nafasi huko Quartier latin, alikua ni under ground bassist
nyuma ya Fally Tyson na mwingine pia.
Engineer Blaise Bula, Alishiriki kwa Kiasi kikubwa kuiunda Wenge BCBG ya sasa.
Hivyo Sunda Bass akawa mtu wa kwanza kuwa
recruited,baada ya hapo chini wenge bcbg chini ya Blaize Bulla ambae
alipania kuisuka bendi upya ikawaita ma-atalaku wa tatu kuwafanyia
majaribio ili wampate mmoja atakaemsaidia Tutu Caludji,miongoni mwa
walioitwa ni Bidjana ambae baadae alienda zaiko huyu Genta Lisimo “Anti
biotique” ambae wakati huo alikua akitokea Anti Choc kwa mzee Bozi
Boziana,Tutu Caludji akamkubali zaidi Genta ambae nafasi yake kule kwa
Bozi ikazibwa na Theo Mbala toka Big Stars ya Defao.
Engeneer Blaize Bula hakuishia hapo katika harakati
zake za kuijenga BCBG, akaona kuna haja pia ya kuimarisha safu ya
uimbaji kwa kuongeza waimbaji wachache,ndipo akawasiliana na rafiki yake
na muandishi wa nyimbo zake wa siku nyingi toka enzi za wenge musica
original ambae pia alikua muandishi wa nyimbo wa CHOC STARS na si
mwingine bali ni JULES KIBENGA MAKIESE a.k.a. Jules Kibens(najua wengi
mtashangaa lakini ndio ukweli),pia akamtafuta RIO KAZADI “rIO de
janeiro” ambae alikua Chef D’ Orchestre katika bendi iitwayo JOLINO
akiwa na akina KABOSE, CHAI NGENGE na baadae BILL CLINTON Pia alikua
chini yake hapo JOLINO.
Hata Rais Kabila pichani amejaribu kwa uwezo wake kuwapatanisha wanamuziki wa Congo, kama ilivyo kwa picha hii.
Rio nae akamwambia Blaize Bulla kwamba kama anamtaka
yeye basi pia amchukue na rafiki yake Chai Ngenge,Blaize akakubali hivyo
wote wakajiunga BCBG,Pia kutokana na kutomuamini Burkinafaso kutokana
na tabia yake ya kuhamahama Bulla aliamua pia kumchukua ALBA ACCOMPA aje
asaidiane nae na kwa kuwa wote kundini walimjua ALBA kutokana na kwamba
alishajaribiwa kundini wenge oariginal na kuonekana anafaa lakini akawa
amechelewa wakati anajiandaa kujiunga na bendi ndio ikawa inavunjika.Baada
ya hapo ikawa ni mazoezi tu na show za ndani,then wakapata contract
nyingine kubwa ya kupiga kusafiri kwenda ulaya kupiga ZENITH na
OLYMPIA,Safari ambayo ilizua mtafaruku mkubwa ulioitingisha sana BCBG
Katika historia ya maisha yake,mtafaruku uliosababisha JB awe kama
alivyo hivi tunavyomuona sasa na BCBG yake.
Je nini kilitokea….twende pamoja siku ya
Ijumaa tutakapo kuwa tunakamilisha makala hii ya Historia ya kuvunjika
kwa Wenge Musica na miaka mitatu ya mwanzo ya JB Mpiana na Werrason.
Kama una maoni usisite kuniandikia kwa piusmicky@yahoo.co.uk au SMS ONLY 0713 666616.
This entry was posted on Wednesday, August 31st, 2011 at 2:58 am and is filed under Bolingo/Ngwasuma, Burudani, Muziki, Sanaa. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0 feed.
You can leave a response, or trackback from your own site.
24 Responses to SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE (Sehemu ya II)
Subscribe to:
Posts (Atom)
Comments System
disqus
Disqus Shortname
msora
Popular Posts
-
SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – (Sehemu...
-
Huha Makuja Nyungi (kushoto), akiwa anaelekea mahakamani muda mfupi kabla ya kusomewa hukumu hiyo. Kulia ni mtuhumiwa mwingine katika ke...
-
Mwezeshaji wa mada ya kwanza kuhusu umuhimu wa TIKA, ndugu Derick Ndetabula akitoa mada kwa washirik.
Header Ads

NAWAPENDA BATANZANIE NA HII BLOG NAIPENDAGA SASA
BANDIA BANDA – BUJUMBURA
MDAU UK
Mdau Brussels,